Jumapili, 22 Mei 2016

         FAHAMU HATUA NNE ZA VIDONDA VYA TUMBO


Na TABIBU JOHN LUPIMO Simu:0719097574 AU 0672666601

Mgonjwa asipopata tiba, tindikali nyingi iliyozalishwa hushuka na kuingia kwenye utumbo mdogo na kuharibu mfumo wa mmeng’enyo au usagaji wa chakula kwa kuwa vimengíenyo vya utumbo mdogo hushindwa kufanya kazi kwenye mazingira ya tindikali.

Hali hii husababisha kuharibika kwa uteute wa sehemu hii ambao ndiyo ulinzi wa utumbo mdogo na matokeo yake ni mtu kuwa na vidonda tumboni pia kwenye utumbo mdogo yaani (duodenal ulcers).
Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoathiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum.
Dalili ya mwanzo  kabisa ya ugonjwa ni ule uvimbe tuliosema unajitokeza  sehemu ya ndani ya tumbo, ambao huambatana na maumivu makali ya tumbo ya mara kwa mara, tumbo kujaa gesi, kichefuchefu cha mara kwa mara, kiungulia kikali pia kutapika kwa baadhi ya wagonjwa.
HATUA YA PILI
Hatua ya pili vidonda hujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hivyo huongezeka na kuwa vikubwa. Ni katika hatua hii mgonjwa huwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu, tumbo kujaa gesi wakati wote, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu.
Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu hujulikana kama chronic dispepsia-yaani kushindwa kufanyakazi kwa mfumo wa kusaga au kumeng’enya chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni.
Tindikali nyingi inayozalishwa tumboni huingia kwenye mzunguko wa damu, mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha mara kwa mara, homa hasa nyakati za jioni na pia mgonjwa hupoteza uzito wa mwili Katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na figo kwa kuwa tayari iko katika mfumo mzima wa mwili kupitia mzunguko wa damu.
HATUA YA TATU
Hatua ya tatu ambayo ni ya hatari ni kwamba vidonda vikubwa hupasua mishipa midogo ya damu na kusabababisha damu kuvia tumboni na kubadilisha rangi ya choo cha mgonjwa kuwa ya kahawia.
Damu nyingi ikivia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu, hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu mara kwa mara, maumivu makali ya tumbo huongezeka, homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya chakula.
HATUA YA NNE
Hatua ya nne ya vidonda vya tumbo ni mtu kukumbwa na saratani ya utumbo na ni hatua ambayo ni ya hatari sana kwa kuwa vidonda hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo muhimu vya ndani na matokeo yake ni saratani au kansa ya utumbo
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni