Ijumaa, 20 Mei 2016

FAHAMU SABABU ZA MAUMIVU YA MGONGO NA TIBA YAKE ASILI HAPA

Hali ya maumivu ya mgongo huwatesa watu wengi hasa wale wenye umri miubwa jambo ambalo husababisha awatu hao kutojisikia vizuri au kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako.

Moja ya sababu za maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama huchangia sana maumivu ya mgongo. 

Sababu nyingine ni ubebaji wa mizigo mizito usiozingatia afya ya mgongo na hata kulalia matandiko (magodoro) laini wakati wa kulala.

Uzito wa kupita kiasi (ujauzito, kitambi) huweza kusababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimama. 

Sababu nyingine ni pamoja na  magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo, lakini pia kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ajali  huweza kuwa sababu pia ya maumivu ya mgongo.

Mbali na sababu hizo pia umri wa uzeeni ni mojawapo ya sababu ya maumivu ya mgongo, kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabadiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa na misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.

Sasa baada ya kufahamu sababu hizo ambazo huchangia maumivu ya mgongo ni vyema ikafahamika kwamba kuna baadhi ya vitu asili huweza kutumika kutibu matatizo haya ya maumivu ya mgongo.

Hapa napenda kukwambia kwamba kitunguu swaumu huweza kutuliza maumivu ya mgongo ambapo utahitajika kusaga punje za kitunguu swaumu kisha tumia lojo lojo yake kuchua ile sehemu yenye maumivu. Fanya zoezi hilo asubuhi na jioni kila siku kwa muda wa wiki mbili na utaona mabadiliko.

kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni