Jumatano, 4 Januari 2017

Maumivu Wakati Wa tendo la ndoa Kwa Wanawake.

Maumivu wakati wa kufanya mapenzi ni hali inayojitokeza hasa kwa wanawake. Hujulikana kwa kitaalamu kama. dyspareunia. Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa kufanya tendo la ndoa au baada ya tendo hilo. Sababu kuu za maumivu haya mara nyingi ni magonjwa ya zinaa na kupungua kwa majimaji ukeni wakati wa tendo lenyewe.

Maumivu Wakati Wa tendo la ndoa
Unaweza kuwa unapata maumivu wakati tendo la ndoa linaendelea. Mara nyingi maumivu haya huwa kwenye kuta za uke, shingo ya uzazi au chini ya kitovu. Sababu za maumivu haya ni;


  1. Kuchubuka ukeni kutokana na maji ya uke kupungua. Inawezekana kutokana na kutoandaliwa vizuri wakati wa tendo au uke kutotoa majimaji ya kutosha.
  2. Magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, vaginitis.
  3. Maambukizi ya shingo ya uzazi (cervicitis)
  4. Maambukizi kwenye mirija ya uzazi. Mara nyingi maumivu hutokea chini ya kitovu au kiuononi.
  5. Maumivu Baada ya Kufanya tendo

Baada ya kukutana na mwenzi wako kingono, unaweza kuanza kupata maumivu dakika chache mpaka siku kadhaa toka mlipokutana. Maumivu ya kawaida huwa ni kwenye uke kutokana na kuchubuka wakati wa kufanya tendo la ndoa. Unaweza kuyahisi vizuri hasa pale unapojisafisha kwa maji au wakati wa kukojoa ikiwa njia ya mkojo imechubuliwa.

Maumivu ndani ya uke kabisa, kiunoni au chini ya kitovu baada ya kufanya tendo la ndoa mara nyingi huonesha dalili za

  • Maambukizi ya shingo ya uzazi
  • Maambukizi ya mirija ya uzazi
  • Saratani ya shingo ya kizazi

Dalili hii inaweza kuambatana na hali ya homa, kutokwa damu ukeni baada ya kufanya tendo la ndoa , kutoa uchafu ukeni, kutapika na kichefuchefu.

Matibabu
Unapopata hali hii jichunguze vizuri. Kama maumivu hayajatokana na michubuko wakati wa tendo la ndoa , basi onana na daktari haraka iwezekanavyo. Maambukizi ya shingo ya uzazi na mirija ya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease – PID) huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii. Matibabu ya haraka ni muhimu ili kupunguza madhara ya magonjwa hayo.

Michubuko kutokana na kufanya tendo la ndoa hupona yenyewe polepole. Jioshe vizuri kwa maji safi. Usipake dawa zozote mpaka uambiwe na daktari wako.
 
NB:  Likini pia unaweza kutufikia katika clinic zetu za lupimo sanitarium clinic tukakupima kwanza ili kujua ugonjwa huo umekuathiri kiasi gani na hapo utaanza matibabu mara moja na utapona kwani dawa zetu zinafanya kazi kwa muda mfupi zaidi unaweza kuwasiliana nami kwa namba 0759324414 au 0742120577

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni