Jumatatu, 23 Januari 2017


Mwanamke kusikia maumivu wakati na baada ya tendo la ndoa


Happy-couple-bed-008.jpgWAPO ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata furaha, wao wanasikia maumivu, wanaume ni mara chache sana kulinganisha na wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili.
Mwanamke anaweza kukosa kuhisi furaha na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni, ukeni au kwa ndani zaidi. Maumivu haya pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni maumivu wakati wa tendo la ndoa ambapo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya tendo.
KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO
Maumivu haya hutokea pale mwanamke anapoanza kukutana kimwili na mwanaume na mara nyingi hutokana na uke kuwa mkavu.
Hii inaweza kusababishwa na maandalizi hafifu ya kabla ya tendo lenyewe na matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko wa hamu ya tendo hilo. Kubana kwa misuli ya uke pia nako kunachangia sana ingawa tatizo hili zaidi ni la kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo kutokana na kumbukumbu mbaya za nyuma.
Kuwa na makovu ukeni kutokana na athari za kukeketwa, uwepo wa michubuko na vidonda au maambukizi ukeni mfano kama fangasi za muda  mrefu na maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono nayo husababisha.
Uvimbe ukeni au uwepo wa jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia ya kawaida endapo hukupona vizuri pia huchangia.
MAUMIVU BAADA YA TENDO
Maumivu haya hutokea muda mfupi baada ya tendo la ndoa kumalizika. Mwanamke atahisi maumivu makali kwa ndani zaidi ya uke au chini ya tumbo lake. Maumivu haya huwa makali na huchukua muda mrefu kupoa.
Maumivu ya chini na ndani zaidi ya uke huleta hisia kama muwasho mkali wa pilipili au kama unakatwakatwa na viwembe na ukinawa unazidi kupata maumivu.

Sasa basi lupimo sanitarium tufanya nini kuhusu tatizo hili, sisi lupimo sanitarium clinic tunazo dawa nzuri kabisa za kumaliza tatizo hili ambapo utakapotufikia tutakupima kwaza katika vipimo vyetu vya kupima mwili mzima ili kujua zaidi chanzo cha tatizo hilo na hapo sasa utaanza matibabu ambapo pia gharama zetu ni nafuu kabisa ambapo utaruhusiwa kulipa kidogokidogo huku ukiendelea na matibabu, zaidi unaweza kunipigia simu namba 0759324414 karibu sana lupimo sanitarium clinic kwa matibabu ya afya yako.

Alhamisi, 12 Januari 2017

            Matatizo Ya Njia Ya Mkojo kwa Wanawake

Magonjwa ya mfumo wa njia ya mkojo na figo ni kati ya maradhi yanayowasumbua watu wengi duniani. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kukojoa mkojo wenye harufu mbaya au mkojo wenye rangi ya maziwa au damu.

Mgonjwa pia hupata maumivu ya kiuno na tumbo chini ya kitovu, kukojoa mkojo kidogo mara kwa mara na kupata hisia za maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo.

Kukojoa damu ingawa ni mojawapo ya dalili za ugonjwa huu, lakini mara nyingi husababishwa na ugonjwa wa kichocho au mawe katika kibofu au katika figo. Ugonjwa wa kifua kikuu katika mfumo wa mkojo pia unaweza kusababisha dalili hii. Dalili nyingine hasa kwa watoto ni mwili kuwa na homa kali kama ile ya malaria.

Utambuzi wa tatizo hili kwa wasichana na wanawake wengi unaweza kuwa mgumu hasa pale wanapojihusisha na ngono hatarishi.

Wanawake wengi wa rika mbalimbali kuanzia vichanga hadi watu wazima na vikongwe wanaweza wakakabiliwa na tatizo hili. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 10 ya wanawake wote duniani hupata tatizo la maradhi ya ngono kila mwaka.

Takwimu zingine za afya ya jamii zinaonyesha kuwa, tatizo la ugonjwa wa uambukizo katika njia ya mkojo huwapata wanawake takribani mara kumi zaidi ya wanaume.

Wachunguzi wa masuala ya afya ya wanawake wanaongeza kusema kwamba wanawake wenye umri kati ya miaka 16 na 35 ndiyo wanaopata maradhi haya mara kwa mara.

Wengi wao hushindwa kuwaeleza madaktari kuhusu hali zao kuhusiana na tatizo hili kutokana na kuona aibu au kuwa na hofu ya kushukiwa kuwa ni wazinifu.
 

Madaktari wa Magonjwa ya Kuambukiza wanasema “Ugonjwa wa uambukizo katika njia ya mkojo ni tatizo linalojitokeza mara kwa mara kwa wanawake waliokoma kupata damu ya hedhi”

Katika utafiti mwingine uliofanywa hapa nchini Tanzania na kuchapishwa mwaka 2009 na A. Masinde pamoja na wenzake kutoka katika Kitengo cha Magonjwa ya Wanawake cha Hospitali ya Bugando Mwanza, ilibainika kuwa wanawake wengi wajawazito wanakabiliwa na tatizo hili. Na miongoni mwao wengi huwa hawaonyeshi dalili za moja kwa moja za maradhi haya.

Wanawake wengi wanaopata tatizo la uambukizo katika njia ya mkojo, hawana habari za kutosha zilizo sahihi juu ya vyanzo na madhara ya tatizo hili linalosumbua mamilioni ya wanawake duniani.
 

Hii huwafanya wengi wachelewe kupata huduma sahihi za matibabu, jambo ambalo huambatana na athari nyingi za kiafya na kiuchumi kwa familia zao na taifa kwa ujumla.

Magonjwa ya njia ya mkojo mara nyingi hutokana na uambukizo wa bakteria katika njia ya  mfumo wa mkojo. Bakteria hawa hushambulia figo, mirija miwili inayotoa mkojo ndani ya figo kupeleka katika kibofu cha mkojo.

Mara nyingi uambukizo huo unaotokana na bakteria huanzia katika uke na kuingia ndani ya njia ya mkojo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba njia ya mkojo ya mwanamke kutoka ukeni hadi ndani ya kibofu ni fupi sana na inakaribiana na njia ya haja kubwa.

Ufupi wa njia hii huwezesha bakteria kuingia kwa urahisi zaidi katika kibofu cha mkojo na kusababisha uambukizo katika mfumo wa mkojo.

Baadhi ya bakteria wanaosababisha uambukizo katika njia hii kwa kawaida huishi ndani ya matumbo yetu na hutoka nje pamoja na kinyesi wakati tunapojisaidia haja kubwa.

Sababu zingine zinazochangia kutokea kwa ugonjwa huu ni pamoja na wanawake wengi kutozingatia usafi wa sehemu za siri hasa wakati wa kujisaidia.

Wasichana  na wanawake wengi wanapomaliza kujisaidia haja kubwa, hujisafisha katika njia ya haja kubwa kabla ya kusafisha ukeni. Jambo hilo husababisha bakteria kuchukuliwa kwa mikono toka katika njia ya haja kubwa na kuwaingiza ukeni.

Kufanya tendo la ngono kwa muda mrefu au kushikashika viungo vya kike bila kunawa kwa maji safi na sabuni, kunaweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia. Kufanya hivyo husababisha bakteria waingie kwa urahisi ndani ya kibofu na kuleta uambukizo.

Wataalamu wa masuala ya afya ya wanawake wanakadiria kuwa kati ya asilimia 75 hadi 90 ya maambukizi katika njia ya mkojo kwa wasichana na wanawake wanaoshiriki tendo la kujamiiana hutokana na kufanya ngono mara kwa mara.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa L.E.Nicolle wa mwaka 2008 uliochapishwa katika jarida la The Urologic Clinics of North America. Nicolle ni mtaalamu wa sayansi ya maikrobailojia katika Chuo Kikuu cha Manitoba, nchini Canada.

Jambo lingine linalowaweka wanawake wengi katika hatari hii, ni kunawa kwa maji yenye povu jingi la sabuni au kutumia sabuni yenye kemikali kali kusafisha ukeni. Sabuni zenye kemikali husababisha uvimbe ndani ya njia ya mkojo na husababisha athari katika njia ya mkojo.

Ukeketaji wa wanawake au wasichana, kuumia kwa uti wa mgongo, ulemavu katika maumbile ya njia ya mkojo pamoja na kutokupata choo vizuri pia ni baadhi ya sababu zinazochangia kutokea kwa tatizo hili.

Lingine linalosababisha ukubwa wa tatizo hili kwa wanawake ni ile tabia ya kutokunywa maji ya kutosha.

Tabia nyingine hatarishi kwa wanawake na wasichana ni kukaa na mkojo kwa muda mrefu bila kwenda kujisaidia hasa wawapo safarini.

Mkojo unapokaa katika kibofu kwa muda mrefu hutoa nafasi kwa bakteria kuzaliana kwa wingi na kusababisha kibofu kishindwe kufanya kazi zake vizuri.

Kukaa na mkojo kwa kipindi kirefu pia huwapa nafasi bakteria kupanda juu katika mirija inayotoa mkojo ndani ya figo na kufanya mashambulizi.

Kukaa kwa muda mrefu na vitambaa vya kukinga damu ya hedhi bila kubadilisha pia huchangia kwa kiwango kikubwa kutokea kwa tatizo hili.

Baadhi ya wanawake hutumia vitambaa ambavyo si salama kwa afya kiasi kwamba huwawia vigumu kuepuka tatizo hili kila mara wawapo katika siku za hedhi.

Magonjwa ya njia na mfumo wa mkojo kwa wasichana na wanawake kwa ujumla ni chanzo kikubwa cha upotevu wa mapato ya familia kutokana na ununuzi wa dawa na kulipia gharama za matibabu na pengine kulazwa hospitalini mara kwa mara.

Mwanamke anayelazwa hospitalini kutokana na matatizo yatokanayo na maradhi katika njia ya mkojo anatazamiwa kukaa hospitalini kati ya siku nne hadi sita akiendelea kupata matibabu.

Hiki ni kipindi kirefu hasa katika nyakati hizi ambapo hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kiuchumi. Lakini pia magonjwa mengine yanayoshambulia mfumo wa mkojo yanaweza kushambulia mfumo wa uzazi wa mwanamke na kusababisha matatizo kama vile ugumba, kuharibika kwa figo au shinikizo la damu na kiharusi.

Ni vema jambo hili likaeleweka vyema miongoni mwa wasichana na wanawake kwa ujumla ili tahadhari zichukuliwe mapema.

Pale msichana au mwanamke anapogundua kuwa ana ugonjwa katika njia ya mkojo, asichelewe kupata huduma za tiba.




NB: Kwa matibabu na ushauri unaweza pia ukatufikia lupimo sanitarium clinic tukakupatia matibabu ya tatizo hilo na matatizo mengine zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0759324414,0769368546 au 0672666601

Jumatano, 4 Januari 2017

Maumivu Wakati Wa tendo la ndoa Kwa Wanawake.

Maumivu wakati wa kufanya mapenzi ni hali inayojitokeza hasa kwa wanawake. Hujulikana kwa kitaalamu kama. dyspareunia. Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa kufanya tendo la ndoa au baada ya tendo hilo. Sababu kuu za maumivu haya mara nyingi ni magonjwa ya zinaa na kupungua kwa majimaji ukeni wakati wa tendo lenyewe.

Maumivu Wakati Wa tendo la ndoa
Unaweza kuwa unapata maumivu wakati tendo la ndoa linaendelea. Mara nyingi maumivu haya huwa kwenye kuta za uke, shingo ya uzazi au chini ya kitovu. Sababu za maumivu haya ni;


  1. Kuchubuka ukeni kutokana na maji ya uke kupungua. Inawezekana kutokana na kutoandaliwa vizuri wakati wa tendo au uke kutotoa majimaji ya kutosha.
  2. Magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, vaginitis.
  3. Maambukizi ya shingo ya uzazi (cervicitis)
  4. Maambukizi kwenye mirija ya uzazi. Mara nyingi maumivu hutokea chini ya kitovu au kiuononi.
  5. Maumivu Baada ya Kufanya tendo

Baada ya kukutana na mwenzi wako kingono, unaweza kuanza kupata maumivu dakika chache mpaka siku kadhaa toka mlipokutana. Maumivu ya kawaida huwa ni kwenye uke kutokana na kuchubuka wakati wa kufanya tendo la ndoa. Unaweza kuyahisi vizuri hasa pale unapojisafisha kwa maji au wakati wa kukojoa ikiwa njia ya mkojo imechubuliwa.

Maumivu ndani ya uke kabisa, kiunoni au chini ya kitovu baada ya kufanya tendo la ndoa mara nyingi huonesha dalili za

  • Maambukizi ya shingo ya uzazi
  • Maambukizi ya mirija ya uzazi
  • Saratani ya shingo ya kizazi

Dalili hii inaweza kuambatana na hali ya homa, kutokwa damu ukeni baada ya kufanya tendo la ndoa , kutoa uchafu ukeni, kutapika na kichefuchefu.

Matibabu
Unapopata hali hii jichunguze vizuri. Kama maumivu hayajatokana na michubuko wakati wa tendo la ndoa , basi onana na daktari haraka iwezekanavyo. Maambukizi ya shingo ya uzazi na mirija ya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease – PID) huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii. Matibabu ya haraka ni muhimu ili kupunguza madhara ya magonjwa hayo.

Michubuko kutokana na kufanya tendo la ndoa hupona yenyewe polepole. Jioshe vizuri kwa maji safi. Usipake dawa zozote mpaka uambiwe na daktari wako.
 
NB:  Likini pia unaweza kutufikia katika clinic zetu za lupimo sanitarium clinic tukakupima kwanza ili kujua ugonjwa huo umekuathiri kiasi gani na hapo utaanza matibabu mara moja na utapona kwani dawa zetu zinafanya kazi kwa muda mfupi zaidi unaweza kuwasiliana nami kwa namba 0759324414 au 0742120577

Alhamisi, 29 Desemba 2016

     Tatizo la kutopata Ujauzito / Mimba

Mtu anaposema tatizo la kutopata ujauzito, ana maana mume na mke walio katika uhusiano wa kutafuta mtoto ndani ya mwaka mmoja, lakini wameshindwa.

Inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani wa kiwango cha chini ni mwaka mmoja.

Ni tatizo kubwa katika jamii kwani kila mmoja anataka afikie malengo ya kuwa na familia.

Mwanamke na mwanamume wote wanahusika katika tatizo hili japo mara nyingi huonekana ni la mwanamke. Kutoshika mimba kwa muda mrefu ni ugumba au infertility kwa kitaalamu. Mwanamke au mwanaume anaweza kuwa mgumba.

Ugumba umegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kwanza ni ‘primary infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kuwa na mimba wala mwanaume hana historia ya kumpa mwanamke mimba.

Ugumba wa aina ya pili ni ‘secondary infertility’ ambapo mwanamke anayo historia ya kuwahi kupata ujauzito, haijalishi kama alizaaa au mimba ilitoka na mwanamume anayo historia ya kumpa mwanamke mimba na pia haijalishi kama mtoto alizaliwa au mimba ilitoka.

Tatizo la mwanamume kutoweza kumpa mwanamke mimba linaweza kusababishwa na kukosa nguvu za kiume hivyo kushindwa kufanya tendo la ndoa.

Hali hii ya kukosa nguvu inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali kwani yenyewe si ugonjwa.

Kwa hiyo kitu cha msingi siyo kuongeza nguvu bali ni kufanya uchunguzi kuona tatizo ni nini na kulipatia ufumbuzi.

Tatizo lingine kwa mwanamume ni kutotoa mbegu za kiume za kutosha au kutoa mbegu zisizo na ubora.

Hii ni baada ya kupima kipimo cha mbegu za kiume. Mbegu zinaweza zisizalishwe au zikazalishwa pasipo na ubora unaostahili kurutubisha yai la mwanamke.

Matatizo mbalimbali yanaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume kama uvutaji wa sigara,  unywaji wa pombe kali, maumivu ya korodani na utumiaji wa dawa za kulevya kama mirungi na bangi.

Mazingira ya joto katika korodani pia huathiri uzalishaji wa mbegu. Kutofahamu mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kipindi gani mwanaume anaweza kumpa mimba ni changamoto nyingine kwa upande wa mwanaume.

Kwa upande wa mwanamke zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha awe na tatizo la kutopata ujauzito.

Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni. Mwili wa mwanamke hutawaliwa na hizi homoni ambazo ni kemikali za asili ndani ya mwili.

Mabadiliko madogo yakitokea wakati wa kuzalishwa kwake au kuzalishwa wakati ambao si muafaka huweza kusababisha ashindwe kupata ujauzito.

Lipo pia tatizo la mwanamke kuwa na uzito mdogo au mkubwa kupita kiasi kutokana na mfumo wa ulaji na mazoezi ya mwili. Mambo haya huathiri uzalishaji wa kawaida wa homoni.

Ikumbukwe pia kuwa uwezo wa kupata ujauzito hupungua kadri umri unavyozidi kuongezeka tangu kipindi anapovunja ungo.

Hii hutokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni husika. Kuanzia miaka 35 na kuendelea huwa kunakuwa na tatizo la kupata ujauzito kwa wanawake wengi hasa wale ambao hawajawahi kabisa kupata mimba.

Umri wa ukomo wa kupata hedhi kwa asilimia 80 ya wanawake ni miaka 45. Wapo wachache kati ya asilimia 20, ambao ukomo wao wa kupata hedhi huwa juu au chini ya miaka 45 na kwa nadra sana wapo wanawake kwenye asilimia hizo ambao angalau huweza kupata ujauzito.

Kuziba kwa mirija ni hali nyingine ambayo huweza kumzuia mwanamke kupata ujauzito. Hali hii huwa mbaya zaidi kama mirija yote miwili imeziba baada ya kuthibitishwa na kipimo maalumu.

Kuziba kwa mirija husababishwa na maradhi yaambikizwayo katika nyonga ya mwanamke. Mengi ya maradhi haya ni yale yatokanayo na kujamiiana ambayo hayakugundulika mapema ili yapate tiba kama vile kisonono.Mirija pia inaweza kuziba baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo unaohusu au usiohusu sehemu ya nyonga.

Mara nyingi wanawake ambao mirija yao imeziba huwa hawaonyeshi dalili zozote za kuziba huko. Ni mpaka kipimo maalumu cha mirija kifanyike ili kujua uwepo wa hali hiyo.

Katika hali ya kawaida, ute unaopatikana kwenye kizazi cha mwanamke huwa na sifa ya kuruhusu mbegu za kiume ziweze kusafiri kwa urahisi na kulifikia yai ili kulirutubisha.

Hali hii hufanyika ndani ya mirija ya uzazi. Kwa baadhi ya wanawake ute huu huwa na uzito na kemikali ambazo ni vigumu kwa mbegu za kiume kupita kwa urahisi.

Wakati mwingine mwili wa mwanamke huzalisha sumu ambazo huziua mbegu za kiume. Haya yote husababisha kukutana kwa yai na mbegu za kiume kusitokee na hivyo mwanamke kutokupata ujauzito.

Zipo pia sababu za kimaumbile na uwepo wa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi na via vya uzazi kwa ujumla.

Hali hii hujitokeza zaidi kwa wanawake wenye umri mkubwa wa kuanzia miaka 30 na kuendelea. Uwezo wa kupata, kutunza au kupata na kutoka kwa ujauzito hutegemea aina ya uvimbe, sehemu ulipo, idadi na ukubwa wa uvimbe.

Hivyo, si wanawake wote wenye uvimbe au vimbe ambao hushindwa kupata ujauzito. Vilevile sio wote wanaopata ujauzito wakiwa na uvimbe. Mara nyingi akiwa na uvimbe ujauzito huishia kutoka au kutunga nje ya mfuko wa mimba.

Matibabu ya saratani pia huweza kuathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito. Hali hii hutegemea aina ya tiba inayohusika kama ni matumizi ya dawa, mionzi, upasuaji au mchanganyiko wa njia mbili au zote kati ya hizo.

Asilimia kubwa ya matatizo ya mwanamke kutokuwa na uwezo wa kupata ujauzito huweza kutibika iwapo njia sahihi za utatuzi zitafuatwa.

Mengi ya matatizo haya huhitaji uchunguzi na ufuatiliaji wa kina. Ni vizuri kuonana na wataalamu wa afya ana kwa ana mapema ili kujua chanzo cha tatizo na kupatiwa msaada unaostahili. 

NB: Kwa upande wa lupimo sanitaium clinic tunafanya nini ili kukabili tatizo hilo, sisi tunazo dawa nzuri za kumaliza tatizo hilo la kutokupata mimba na tumewatibu watu wengi waliokuwa na tatizo hilo na wakafanikiwa lakini kama una uvimbe katika kizazi tutakupa dawa ya kuyeyusha huo uvimbe bila kufanyiwa upasuaji, lakini pia kama mirija ya uzazi imeziba tunayo pia dawa ya kuzibua mirija ya uzazi na kuwa salama kabisa na mimba utapata kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0759324414 au 0742120577 asanteni sana, 

Alhamisi, 22 Desemba 2016

              JE UNAYO MAWE KWENYE FIGO?

UGONJWA wa mawe kwenye figo siyo mgeni miongoni mwa watu hivi sasa, hasa wenye umri mkubwa. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaamu linajulikana kama ‘Gallstones’.

Mawe ya kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo na wakati mwingine huwa vikubwa mfano wa dole gumba. Hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.

Tiba ya tatizo la mawe kwenye figo, mara nyingi huwa ni upasuaji wa kuvitoa na hugharimu fedha nyingi na pia husababisha maumivu wakati wa kufanya oparesheni hiyo. Lakini kwa kutumia tiba mbadala ya vyakula, unaweza kuondoa mawe hayo bila kufanya oparesheni.

Maelezo haya huwezi kuambiwa na daktari hospitali hata siku moja lakini kwa kusoma makala kama haya utajifunza njia nyingine ya kuutibu mwili wako kwa njia ya vyakula. Kama mawe yaliingia tumboni kwa njia ya vyakula, bila shaka yanaweza kutoka pia kwa vyakula.

JINSI YA KUONDOA MAWE KWENYE FIGO
Kuna tiba mbadala za aina nyingi, lakini katika makala yangu ya leo nitawajulisha njia mbili unazoweza kuchagua moja wapo. Moja ni kufanya kwa muda wa siku sita mfululizo na nyingine ni ya kufanya kwa siku moja tu, chaguo ni lako.

NJIA YA SIKU SITA
Katika siku tano za kwanza, kunywa juisi halisi ya Tufaha(pure apple juice) glasi kubwa nne kila siku kwa siku tano mfululizo. Au kula tufaha nzuri tano badala ya juisi. Ili kuwa na uhakika na juisi halisi, ni vyema ukanunua tufaha za kijani (green apple) na ukatengeneza juisi mwenywe. Juisi hii au matufaha hayo yatafanya kazi ya kulainisha kwanza mawe tumboni.

Siku ya sita, anza siku yako kwa kula mlo wako wa kawaida hadi saa nane mchana, kuanzia saa nane utatakiwa ufunge usile kitu chochote mpaka asubuhi siku inayofuata ndiyo ule chakula chako.

Ifikapo saa 12 jioni, kunywa kikombe au glasi moja kubwa ya maji uliyochanganya na kijiko kimoja kidogo cha ‘Magnesium Sulphate’ . Weka maji kwenye glasi au kikombe, chukua ‘Magnesium Sulphate’, chota kijiko kimoja kidogo, tia kwenye maji hayo na changanya, kisha unywe mara moja. ‘Magnesium’ husaidia kufungua njia.

Ifikapo saa mbili usiku, rudia kunywa mchanganyiko huo wa maji na ‘Magnesium’. Baadaye saa 4 usiku, changanya nusu kikombe cha juisi halisi ya limau (fresh lemon juice) na nusu kikombe cha mafuta halisi ya mzaituni (pure olive Oil). Hiki ndiyo kitakuwa kinywaji chako cha mwisho kwa usiku huo, kisha nenda kalale.

Vinywaji hivyo vitasaidia mawe kutoka kwa njia ya haja kubwa bila shida. Usiku huo huo, unaweza kusikia haja ya kwenda chooni, au vinginevyo utasikia asubuhi.

NJIA YA SIKU MOJA
Ukisha kula chakula chako cha usiku, usile kitu kingine tena hadi kesho yake asubuhi ambapo utakunywa glasi kubwa tatu za juisi ya tufaha za kijani. Usile kitu kingine hadi mchana unywe tena juisi ya tufaha 3. Usile kitu kingine tena hadi usiku wakati wa chakula cha usiku, unywe tena juisi ya tufaha kubwa 3 za kijani kama mlo wako wa usiku.

Iwapo utashindwa kutengeneza juisi mwenywe, basi bora ule tufaha zenyewe kiasi kilichotajwa. Katikati ya mlo na mlo, utaruhusiwa kunywa maji ya kawaida tu na siyo kitu kingine. Hii ina maana utafunga siku moja kwa kula tufaha na maji tu.

Muda mfupi kabla ya kwenda kitandani, tengeneza juisi halisi ya malimau matatu, changanya na nusu kikombe cha mafuta ya mzaituni (Pure olive oil) kunywa kisha panda kitandani, kinywaji kinaweza kisiwe na ladha nzuri, lakini usijali, ndiyo dawa.

Ukiwa kitandani, lalia ubavu wako wa kulia na ukunje magoti kadiri uwezavyo na ulale hivyo kwa muda utakaoweza au hadi hapo utakapopitiwa na usingizi. Ulalaji wa aina hii huwezesha utokaji wa mawe kwenye figo na kwenda tumboni kwa ajili ya kutoka kwa njia ya haja kubwa.

Ukijisikia haja ya kwenda chooni, fanya hivyo haraka, vinginevyo utalala hadi asubuhi ndiyo utakwenda chooni. Ili kuona kama vimawe vimetoka, weka utaratibu wa kukagua haja yako na utaona vitu rangi ya kijivu au kijani vinavyong’aa na hapo utakuwa umefanikiwa.

NB: Kwa maelezo zaidi au unaswali lolote nipigie simu sasa hivi kwa namba 0759324414, 0769368546, na 0742120577 

Jumanne, 20 Desemba 2016

Vyakula hivi vinasababisha saratani ! Jihadharani navyo !

Ugonjwa  wa  saratani  ama  kansa  unatajwa  kuwa  ndio  ugonjwa  wa  hatari  zaidi  duniani  na  unaoua   watu  wengi  zaidi  duniani.  Ugonjwa  huu  unasababishwa  na  mambo  mbalimbali  ikiwa  ni  pamoja  na  ulaji  wa  vyakula   vya aina  mbalimbali. Vifuatavyo  ni  baadhi  ya  vyakula  ambavyo  vimetajwa  katika  tafiti  mbalimbali  kuwa  visababishi  vya  ugonjwa  wa  saratani.

VYAKULA VYA KUKAANGA
Vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya na miongoni mw a madhara hayo ni pamoja na kusababisha kansa ya kwenye mfuko wa uzazi. Vyakula hivyo ni pamoja na chips na vyakula vingine vinavyopikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.

VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI
Vyakula vyenye chumvi nyingi vimebainika navyo kusababisha kansa. Vile vile inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa kansa tumboni. Kansa ya tumbo inadaiwa kuua watu wengi nchini Japan kutokana na jamii hiyo kupenda sana vyakula vyenye chumvi nyingi. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni vile vya kusindika, kama vile nyama za makopo, maharage, n.k

SUKARI
Matumizi mabaya ya sukari yanaelezwa kusababisha kansa. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa kwenye vinywaji mbalimbali, zikiwemo soda, juisi za ladha ya matunda ambazo huwa na kiwango kingi cha ‘fructose’ ambayo inaelezwa kusababisha saratani ya kongosho.

Vile vile sukari kwa ujumla wake hairuhusiwi kutumiwa na mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na kansa kwa sababu chakula cha chembechembe za saratani mara nyingi huwa ni sukari. Kwa matumizi mengine ya kawaida, sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula tunavyotumia, tofauti na baadhai ya watu wanavyoweka sukari nyingi ili kupata utamu zaidi.

NYAMA ILIYOIVA SANA
Upikaji wa nyama kwa muda mrefu na kwenye moto mkali (high temperatures) husababisha aina fulani ya kemikali inayojulikana kitaalamu kama ‘heterocyclic aromatic amines’. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah (University of Utah), umeonesha kwamba watu wanaopenda kula nyama zilizoiva sana, wako hatarini zaidi kupatwa na saratani ya njia ya haja kubwa (Rectal Cancer). Hivyo inashauriwa unapopika nyama, usipike kwenye moto mkali na kuiva kupita kiasi.

POMBE
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake kwa waume. Aina ya saratani zinazodaiwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya mdomo, ini, utumbo na koromeo, ambazo ndizo zinazoua watu wengi hivi sasa nchini Marekani.

NYAMA NA MAFUTA
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja. Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.

Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu husababisha saratani pia. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa ya saratani.

VYAKULA VYA UNGA MWEUPE
Vyakula vyote vinavyopikwa kutokana na unga uliokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake vyote na kuwa mweupe, vinaelezwa kuchangia magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘donati’ (doughnuts), maandazi, mkate mweupe, n.k

Mwisho, licha ya kuepuka ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu, unatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. Utaona kwamba adui mkubwa wa afya zetu ni vyakula vyote vya kusindika na vile vya kutengenezwa viwandani au vile ambavyo wakati wa utayarisjaji wake huondolewa virutubisho vyake vya asili.
NB: kwa maelezo zaidi unaweza kunipigia sasa hivi kwa namba 0759324414 au 0673750475.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

       Tatizo La Kupoteza Kumbukumbu

Kupoteza kumbukumbu ni ugonjwa unaoingia kwa kasi, ugonjwa huu Umetajwa sasa unakuja juu kuliko maradhi sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na saratani
 

Kupoteza kumbukumbu hutokea pale eneo la ubongo linalohusika katika kuhifadhi taarifa linapoathirika.

Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu kwa kawaida unawapata wazee. Uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1906 na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili, Alois Alzheimer.

Dk Alzheimer, ambaye ni Mjerumani, alipata mgonjwa mwenye tatizo hilo ambaye alikuwa anapoteza kumbukumbu, kuchanganyikiwa na kupata ugumu wa kuelewa maswali anayoulizwa.


Mgonjwa huyo alifariki dunia na ndipo Dk Alzheimer alipofanya uchunguzi katika ubongo wa marehemu na kubaini kuwa kulikuwa na hitilafu katika baadhi ya seli za ubongo wake.

Hivyo, akawa daktari wa kwanza kubaini ugonjwa huo wa kupoteza kumbukumbu na kulifanya Shirika la Afya Duniani (WHO) limpe heshima kwa kuuita ugonjwa huo jina la daktari huyo. Ugonjwa huo unafahamika kama Alzheimer.

Ugonjwa huu ni moja ya matatizo makubwa ya kiafya yanaoikabili dunia hasa katika kipindi hiki ambacho kuna ongezeko la wazee hasa katika nchi zilizoendelea.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, mnamo mwaka 2010 ugonjwa huu ulishika namba ya sita kati ya magonjwa yanayosababisha vifo nchini Marekani.

Ripoti WHO kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ugonjwa wa Alzheimer (ADI), inakadiria kuwa idadi ya wagonjwa wa tatizo hili itaongezeka mara tatu zaidi ifikapo mwaka 2050 na kuifanya dunia kuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 135.

WEWE NI MIONGONI MWA WATU HAO? Siyo jambo la ajabu lakini unapaswa kutunza afya yako.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kwa sasa kuna watu 44 milioni wanaougua maradhi haya hatari duniani kote. Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 22 ya wagonjwa 35.6 milioni waliokuwa na maradhi haya miaka mitatu iliyopita.

Ugonjwa huu ni janga la kimataifa na hali inazidi kuwa mbaya. Tunapoangalia hali ya siku za usoni, tunaona kuwa idadi ya wagonjwa itaongezeka sana.” ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu miongoni mwa wazee, ni moja ya magonjwa yanayowakabili watu wenye umri zaidi ya miaka 55 na unasababisha upotevu wa mapato kuliko saratani, kiharusi na magonjwa ya moyo kwa pamoja.

Ugonjwa huu wa wazee, unasababisha mtu kupoteza kumbukumbu ya matukio ya karibuni na kadri ugonjwa unavyoendelea mtu anaweza kushindwa kuzungumza vizuri. Tatizo jingine ni kupoteza uwezo wa kuelewa mazingira anayoishi, kushindwa kujihudumia na kupata mabadiliko ya kitabia kama vile kujitenga na watu wa familia au jamii.

Ingawa hali hii hujitokeza taratibu, lakini inaweza kusababisha kifo ndani ya kipindi cha miaka mitatu hadi tisa. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa S. Todd na wenzake uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la International Geriatric Psychiatry, toleo la 28 (11).

Ingawa chanzo halisi cha maradhi haya hakijulikani bayana, baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa ugonjwa huu unatokana na changamoto za mazingira pamoja na matatizo ya urithi wa vinasaba vya kijenetiki vyenye mwelekeo wa kupata tatizo hili.

chembe za urithi zinachangia kutokea kwa maradhi haya kwa asilimia 70. Katika utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la kisayansi la Nature Genetics, ilibainika kuwa kuna takriban aina 20 za vinasaba vya kijenetiki vinavyochangia mtu kupata maradhi haya.

Timu ya watafiti wa taasisi ya Pasteur ya nchini Ufaransa iliyoongozwa na Philippe Amouyel ilipata ushahidi kutoka kwa washiriki wa utafiti zaidi ya 74,000 kutoka nchi 15 sehemu mbalimbali duniani na kubaini kuwa wagonjwa wenye maradhi haya, DNA zao zilikuwa na matatizo yanayofanana.

Mambo mengine  yanayochangia mtu kupata maradhi haya ni pamoja na shinikizo la damu, msongo wa mawazo pamoja na ajali zinazohusisha kichwa.

Maradhi haya yanaweza kugundulika kwa daktari kuchukua maelezo ya tatizo, historia ya kitabibu, kufanya jaribio la kupima uwezo wa mtu wa kiakili, kupima damu na vipimo vyingine vya uchunguzi kwa kutumia mionzi kama vile MRI.
 

Mazoezi ya mwili ni muhimu katika programu ya tiba ya wagonjwa wa namna hii ili kuzuia hali isiwe mbaya haraka na kumkinga mgonjwa dhidi ya maradhi yanayowanyemelea watu.

Ulaji wa matunda, mbogamboga, kokwa na nafaka zisizokobolewa pamoja na vyakula vingine ambavyo havijasindikwa, inaweza kuwa njia bora ya kukabili vyanzo vya tatizo hili. 


NB: Kwa upande wa lupimo sanitarium clinic tunazo dawa nzuri kabi za kumaliza tatizo, japo utafiti unaonyesha kuwa wazee ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo lakini pia kwa upande mwingine nao vijana wanaweza kuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili zaidi unweza kutufikia lupimo sanitarium clinic kupata matibabu ya tatizo hilo.


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic