Jumapili, 4 Novemba 2018

KWA MAGONJWA SUGU, TUMIA DAWA HIZI MPYA KUTOKA LUPIMO SANITARIUM CLINIC.



Lupimo sanitarium clinic ni clinic inayojishughulisha na tiba ya magonjwa mbalimbali  kwa dawa zilizotengenezwa hapa nchini tanzania, kwa kutumia mimea asili.

Lupimo sanitarium clinic wamekuletea dawa iitwayo FIWEMU HERBS ambayo husaidia tatizo la ugumba kwa wanawake, husaidia mimba isiharibike, vilevile hupunguza maumivu wakati wa hedhi .

na kwa upande wa  wananume lupimo sanitarium clinic wamekuletea dawa iitwayo JC HERBS ambayo husaidia kupunguza mapungufu yaliomo katika mfumo wa uzazi wa mwanaume, husaidia kupunguza tatizo la kupata haja ndogo kwa shida (tezi dume), na pia husaidia kupunguza magonjwa yaenezwayo kwa njia ya kujamiiana.

Dawa hizi zimesajiliwa na baraza la tiba asili na tiba mbadala kuwa hazina madhara kwa mtumiaji na zinapatikana nchi nzima katika vituo vya lupimo sanitaruim clinic.

Kwa mawasialino zaidi tupigie kwa namba 0672666601 au 0742120577
Karibu lupimo sanitarium clinic uhudumiwe.

Ijumaa, 24 Novemba 2017

Zijue sababu za Watoto kukosa Hamu ya kula Chakula

Zijue sababu za Watoto kukosa Hamu ya kula Chakula


Kukosa hamu ya kula ni tatizo la kawaida kwa watoto ambalo hupelekea wazazi wengi kuwa na wasiwasi juu ya afya ya watoto wao. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha  kukosa hamu ya kula na tatizo hili linapojitokeza tunatakiwa kuwa watulivu na kujaribu kuchunguza kwa makini ni kwa nini mtoto anakosa hamu ya kula. Baadhi ya sababu zaweza kutatuliwa na mzazi au mlezi lakini sababu nyingine kama zisababishwazo na magonjwa zitahitaji msaada wa wataalam wa afya.

Moja ya sababu kubwa ambayo huwakosesha watoto hamu ya kula ni aina mbalimbali za magonjwa. Magonjwa kama Malaria, kuhara, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa, magonjwa ya kinywa na koo, homa na mafua au dalili nyinginezo ambazo humkosesha mtoto raha hupelekea watoto kukosa hamu ya kula.

Matatizo ya kifamilia na msongo ni sababu nyingine ambayo huwakosesha watoto raha na hamu ya kula. Kama walivyo watu wazima watoto pia hukumbana na matatizo ya kifamilia kama kupoteza ndugu au vitu wavipendavyo. Lakini pia watoto hukumbana pia na changamoto mbalimbali za kimaisha kama majukumu ya shule au pengine kukumbana na unyanyasaji kama kuzomewa na mambo mengine mengi yanayokiuka haki zao.

Kwa hiyo ili kumuepusha mtoto na ukosefu wa hamu ya kula, wazazi na walezi hawana budi kuwa makini endapo wataona mabadiliko yoyote ya kitabia ya mtoto. Kugundua na kuweza kuziondoa sababu zinazomsababishia mtoto msongo, tutaweza kuwarudisha katika hali ya kawaida na hamu ya kula itarejea tena.

Lakini pia wakati mwingine hali hii hutokana na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula ujulikanao kitaalam kama Anorexia nervosa. Watoto wenye ugonjwa huu huweza kukaa muda mrefu bila kula ingawa hawana tatizo jingine, na endapo watapewa chakula huchagua aina fulani tu ya chakula jambo ambalo hupelekea kutopata mlo ulio kamili na hii hupelekea kupungua uzito pamoja na kudhoofu kwa afya zao .

Jambo hili linapojitokeza ni vyema kumpeleka mtoto kwa wataalam wa afya wa masuala ya lishe ambao watakuwa msaada mkubwa katika kumsaidia mtoto wako kurejesha tena hamu ya kula.

Kiwango kidogo cha ukuaji wa mtoto huchangia  kupungua kwa hamu ya kula. Katika mwaka wa kwanza wa maisha ya watoto, watoto hukua haraka lakini baada ya mwaka mmoja kiwango cha ukuaji hupungua na kiwango cha chakula wanachokula pia hupungua. Katika wakati huo, hali hiyo ni ya kawaida katika maisha ya watoto.

Sababu nyingine ambazo huchangia watoto kukosa hamu ya kula ni kama maudhi ya dawa, upungufu wa damu, uambukizi wa minyoo na matatizo ya mmeng'enyo mfano mtoto kutopata choo.

Maudhi ya dawa mbalimbali ambazo hutumika kutibu magonjwa kwa watoto yanaweza kuchangia watoto kukosa hamu ya kula. Mfano daktari akimwandikia mtoto dawa za antibiotiki, zaweza kusababisha tazizo la kukosa hamu ya kula. Kupoteza hamu ya kula kwa watoto wanaotumia antibiotiki ni maudhi ya dawa ambayo huwapata watoto wengi. Dawa nyingine pia zaweza kupelekea kupata maudhi ya dawa kama kichefuchefu na kutapika. Tatizo hili humalizika mtoto anapomaliza dawa na endapo atakuwa amepona.

Uambukizi wa minyoo huchangia tatizo hili. Minyoo huingia katika mfumo wa mmeng'enyo wa watoto na kusababisha upotevu wa damu. Minyoo hutegemea ufyonzaji wa damu kama chakula chao, na katika uambukizi sugu hupelekea kuvuja kwa damu,upungufu wa damu, kuhara, kichefuchefu, kutapika na kukosa hamu ya kula. Endapo mtoto ataonyesha dalili za umbukizi wa minyoo, ni vyema kuwaona wataalam wa afya ili kuweza kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu.

Ugonjwa wa upungufu wa damu ambao kwa kitaalam hujulikana kama anemia, husababishia watoto tatizo hili. Kiwango kidogo cha madini ya chuma katika damu, huwapata watoto ambao hawapati lishe ya kutosha yenye madini haya. Lakini pia anemia yaweza kusababishwa na uambukizi wa minyoo au hata magonjwa mengine. Watoto wenye anemia huwa wadhaifu na wasio wachangamfu, na kama ugonjwa usipotibiwa utaathiri afya ya mtoto hata maendeleo yake shuleni. Ni vyema mtoto akafanyiwa vipimo vya damu endapo utahisi au ataonyesha dalili za ugonjwa wa anemia.

Kwa watoto hasa wadogo, kukosa choo hupelekea kukosa hamu ya kula. Kwa hiyo inapotokea basi ni vyema kupata msaada wa wataalam ili mtoto aweze kuondokana na tatizo hilo.

Wazazi na walezi wazingatie yafuatayo ili kuboresha hamu ya kula ya watoto wao:


  • Kuwa na ratiba nzuri ya kumpa mtoto chakula, na mtoto apewa chakula anapokuwa na njaa.
  • Usiwagombeze au kutoa maonyo makali kwa watoto wakati wa kula.
  • Kuwa na milo midogo kati ya milo mikubwa.
  • Mpe mtoto kiasi kidogo cha chakula lakini mara nyingi kwa siku na siyo kumshindilia kwa wakati mmoja.
  • Usimlazimishe mtoto kula kama hana njaa.
  • Hakisha mtoto anashiriki katika michezo, kwa kuwa michezo huusisha matumizi ya nishati ya mwili na kuboresha mifumo mbalimbali ya mwili.
  • Wakati mwingine mpe nafasi mtoto wa uchaguzi wa chakula akipendacho, lakini chini ya uangalilizi wa mzazi au mlezi ili afanye uchaguzi ulio sahihi.
Wakati wote  wazazi na walezi tukumbuke kuwa tatizo la kukosa hamu ya kula ni la kawaida kwa watoto wengi, na tatizo linapojitokeza hatuhitajiki kuwa na wasiwasi kila wakati. Kama mtoto wako ana afya njema, anapata usingizi vizuri na ni mwenye furaha, hauna sababu ya kuwa na wasiwasi. Lakini kama tatizo litaendelea kwa muda mrefu, basi hatuna budi kuonana na wataalam wa afya kwa msaada zaidi.

Huu ndiyo Ugonjwa Utokanao na Msongo wa Mawazo


Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi.

Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi.

Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe  na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo.

Ufuatayo ni ugonjwa unaosabishwa na msongo:

Magonjwa ya moyo
Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo. Magonjwa haya ya moyo ni kama shinikizo la juu la damu, moyo kwenda mbio na mengineyo.

Matabibu wanafahamu kuwa, msongo wa ghafla waweza kusababisha magonjwa hatari ya moyo kama shambulizi la moyo. Watu wenye matatizo ya moyo hawana budi kuepuka hali ya msongo na kujifunza jinsi ya kukabiliana na maisha katika hali ya utulivu kwa kadiri iwezekanavyo.

Hivyo ili uweze kuepuka ugonjwa huu unachoptakiwa kufanya ni kuhakisha unaepuka visababishi vyote vya ugonjwa  huu vya msongo, ambavyo nimekwisha vielezea hapo awali.

Jumatano, 27 Septemba 2017

LUPIMO SANITARIUM CLINIC YAUNGA MKONO SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA KUTENGENEZA KIWANDA CHA KUZALISHA DAWA ZA ASILI , KWA KUTUMIA MIMEA, MATUNDA NA MBOGAMBOGA.

Haya ni maboresho makubwa ambayo clinic ya lupimo sanitarium imeyafanya, kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza dawa za asili kwa kutumia mimea, matunda pamoja na  mbogamboga, kiwanda hiki kipo jijini dar es salaam ambapo dawa zote zitakuwa zinazaliwa hapa dar es salaam na kusambazwa katika vituo vyote vya lupimo clinic.

Kiwanda hiki kitarahisisha utengenezwaji wa dawa kwa haraka tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo dawa zilikuwa zikichukua mda mrefu kukamilika.

hii imekuja kufuataia agizo la serikali kupitia wizara ya afya kuwataka matabibu wote katika vituo vyao.

Lupimo sanitarium clinic wanakuhakikishia huduma bora na yenye uhakika

MAWASILIANO 0759324414 AU 0672666601



Tabibu john lupimo akielekeza jambo juu ya kiwanda hiki cha kutengeneza dawa










Jumatano, 26 Aprili 2017

TATIZO LA KUTOPATA RAHA WAKATI WA TENDO LA NDOA



https://encrypted-tbn0.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcTPxu_qqnuERMXGjQ1VbK2vEK0nWyQ55xmuELcCdgziGoJs2h2x


Wapo ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata raha, husikia maumivu, mwanaume katika uume lakini ni mara chache sana kulinganisha na wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili.
Mwanamke anaweza kukosa raha kabisa na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni ukeni au kwa ndani zaidi. Maumivu haya pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni maumivu wakati wa tendo ambayo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya tendo.


Kuumia wakati wa tendo
Maumivu haya hutokea pale uume unapoanza kuingia ukeni na hutokana na uke kuwa mkavu.
Hili linaweza kusababishwa na maandalizi duni kabla ya tendo, matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko na hamu ya tendo.

Kubana kwa misuli ya uke pia huchangia ingawa tatizo hili zaidi ni la kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo.

Kuwa na makovu ukeni kutokana na athari za kukeketwa, uwepo wa michubuko na vidonda au maambukizi ukeni mfano fangasi ya muda mrefu na maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono.
Uvimbe ukeni au uwepo wa jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia ya kawaida endapo hukupona vizuri.

Kuhisi maumivu baada ya tendo
Maumivu haya hutokea muda mfupi baada ya tendo la ndoa. Mwanamke huhisi maumivu kwa ndani zaidi ukeni au chini ya tumbo. Maumivu huwa makali na huchukua muda mrefu.
Maumivu ya chini na ndani zaidi ukeni huleta hisia kama muwasho mkali wa pilipili au kama unakatwakatwa na viwembe na ukinawa unazidi kupata maumivu.

Maumivu ya ndani zaidi ukeni wakati mwingine huambatana na hali ya kuhisi kama kuna kitu kinasukumwa wakati wa tendo na unapomaliza tendo ukinawa unahisi kitu kimevimba ndani ukeni kama kigololi. Maumivu huwa chini ya tumbo na wakati mwingine husambaa kulia na kushoto ya mirija. Wengine huumwa na kiuno hata kutembea inakuwa shida mara tu baada ya kumaliza tendo.

Hali ikiwa mbaya mwanamke hutokwa na damu baada ya tendo, hali ambayo siyo dalili nzuri kwani hata saratani ya shingo ya uzazi nayo huonyesha dalili hii ya damu.

Hali ya maumivu pia huambatana na kutokwa na majimaji ukeni wakati mwingine yakiambatana na muwasho mkali na harufu. Hata wanaume wanaweza kutokwa na damu baada ya tendo badala ya manii.

Nini cha kufanya?
Tatizo hili ni kubwa na lina vyanzo vingi kama tulivyoona, hivyo ni vema kufanya uchunguzi kujua chanzo halisi ndiyo tiba ifuate.

Epuka kutumia dawa bila ya kujua chanzo halisi.
Uchunguzi hufanyika katika hospitali za mikoa, wilaya kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama.
Ni vema uwahi hospitali. 
lakini kama ikikupendeza unaweza kutufikia lupimo sanitarium clinic ukapata matibabu, na hapo utakutana na tabibu mkuu john lupimo kwa ushauri na matibabu zaidi karibuni sana

Jumanne, 25 Aprili 2017

                           FAHAMU JUU YA HEDHI YA KAWAIDA NI IPI?



Hedhi ya kawaida ni ile ambayo;
 Hutoka mara moja kwa mwezi .
 Hutoka kwa muda wa siku 3,4 au 5 tu.
 Hutoka bila maumivu makali
 Hutoka kwa kiasi cha kati cha damu yaani kubadili pedi mara moja tu kwa siku.
AINA TATU (3) ZA MZUNGUKO WA HEDHI
• Mzunguko wa siku 24 (mfupi)
• Mzunguko wa siku 28 (wa kati)
• Mzunguko wa siku 30 au 32 (mrefu)
SIKU ZA KUBEBA MIMBA (OVULATION DAY)
 SIKU 24 (MFUPI)
Huu ni mzunguko mfupi ,Hivyo hesabu kuanzia siku unapoanza hedhi siku ya kwanza hadi ya 9 hizi ni siku salama, kuanzia siku (10,11,12,13,14) Hizi ni siku za kubeba mimba.
 SIKU 28 (KATI)
Huu ni mzunguko wa kati, hivyo hesabu kuanzia siku ya kwanza unapoanza hedhi hadi siku ya 11 ni siku salama, siku ya (12,13,14,15,16,17). Hizi ni siku za kubeba mimba.
 SIKU 30 (MREFU)
Hesabu kuanzia siku ya kwanza unapoanza hedhi hadi siku ya 12.Hizi ni siku salama. Kuanzia siku ya (13,14,15,16,17,18). Hizi ni siku za kubeba mimba.
DALILI ZA KUPEVUKA KWA MAYAI
1. Joto la mwili kuongezeka 0.2 – 0.58C
2. Ute kuvutika.
3. Siku za mzunguko wa hedhi
4. Mlango wa mji wa mimba (cervix) kulainika kuwa mwekundu zaidi
5. Maumivu kidogo ya tumbo kulia au kushoto
6. Chuchu kuuma na kutoa majimaji au maziwa.
NB: Kwa maelezo zaidi juu ya mada hii naomba unipigie kwa namba yangu ya mknoni ya 0759324414 au 0719097574 karibu kwa swali lolote juu ya mada hii.







Jumamosi, 28 Januari 2017

                         OFA OFA OFA OFA OFA OFA OFA OFA OFAAAAAAA




Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef


Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef


KWA MARA NYINGINE TENA MKURUGENZI WA LUPIMO SANITARIUM CLINIC TABIBU JOHN LUPIMO ANAKUTANGAZIA OFA YA VIPIMO BUUUREEEE KABISA KATIKA VITUO VYA MBEYA NA MWANZA AMBAPO OFA HII ITAANZA TAREHE 01,02,2017 HADI TAREHE 01,03,2017,

OFA HII ITAKUWA INAANZA MAJIRA YA SAA MBILI KAMILI ASUBUHI HADI SAA KUMI NA MOJA NA NUSU ZA JIONI.

UNACHOTAKIWA KUKIFANYA NI KUCHUKUA SHILLINGI 5000 TU KWA AJILI YA GHARAMA ZA KUMWONA TABIBU NA KUFUNGUA FILE LAKO NA BAADA YA KUPATA VIPIMO AMBAVYO UTAPIMWABURE NA KUSOMEWA MAJIBU YAKO JUU YA MATATIZO YANAYOKUSUMBUA, UNARUHUSIWA PIA KUANZA MATIBABU KWA HELA YOYOTE UTAKAYOKUWA NAYO KWANI LUPIMO SANITARIUM CLINI PIA TUNAKURUHUSU KULIPIA KIDOKIDOGO HUKU UKIENDELEA NA MATIBABU.

KUMBUKA OFA HII YA VIPIMO BURE, VITUO VINAVYOHUSIKA NI MBEYA NA MWANZA TU, VINGINE VITAFUATA, NA ITAANZA 01,02,2017 HADI 01,03,2017 KUANZIA SAA MBILI KAMILI ASUBUHI HADI SAA KUMI NA MOJA NA NUSU ZA JIONI KILA SIKU.
LUPIMO SANITARIUM CLINIC TUNATIBU MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA MIMEA MATUNDA NA MBOGAMBOGA.

TUNATIBU : MATATIZO YA UZAZI KWA PANDE ZOTE YAANI MAMA NA BABA , KUTOKUSHIKA MIMBA, MIRIJA YA UZAZI KUZIBA, UVIMBE KWENYE KIZAZI, HEDHI KUBADILIKABADILIKA, MUWASHO SEHEMU ZA SIRI, UTI, UPUNGUFU WA WA NGUVU ZA KIUME, VIDONDA VYA TUMBO, KISUKARI, KIFAFA, PUMU, MOYO, KUTOKWA NA KINYAMA SEHEMU ZA HAJA KUBWA YAANI BAWASILI, TUNAYO PIA DAWA YA KUONGEZA CD4 KWA HARAKA NA NA MAGONJWA MENGINE MENGI,.

KWA MAELEZO ZAIDI BASI UNAWEZA KUNIPIGIA SIMU SASA HIVI KWA NAMBA 0759324414 AU 0742120577, PIA UNAWEZA KUTEMBELEA UKURASA WETU WA FACEBOOK WA WWW.FACEBOOK.COM/LUPIMO CLINI AU INSTAGRAM, ANDIKA LUPIMO CLINIC, TWITTER, ANDIKA LUPIMO CLINIC, KARIBUNI SANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC UFURAHIE HUDUMA ZETU.