Jumatano, 13 Mei 2015

FAHAMU NAMNA HOMA YA MANJANO INAVYOWEZA KUMPATA BINADAMU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEglCt73Sn7YvvqmBcX2ORRbY-RIRjvCpAfoj4WmVHdYNk2eDF6JwqVPCnJ1VVQRHJ-7yHsxd953hWiljkWdnH-Ly-_HTYUOTVRaPYoWK_fp0kHJnfp1473LmD6FxVHrhxQI_FyEjibgTaE/s1600/om831a.jpg
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitwavyo flavivirus. Ugonjwa huu huenezwa na mbu aina ya aedes aegypti na ni vigumu kuutofautisha na magonjwa mengine kama malaria kwenye dalili za mwanzo bila kutumia vipimo. Ugonjwa huu hushambulia seli za kinga mwilini (macrophages, monocytes).
Baada ya kuingia ndani ya seli, virusi vya homa ya manjano huzaliana na kuendelea kukua huku wakihama kutoka kwenye seli moja hadi nyingine kushambulia. Virusi huenda kwenye seli za ini na kuanza kuzishambulia na hivyo kusababisha sumu kwenye damu

DALILI ZA HOMA YA MANJANO
Baada ya kuambukizwa homa ya manjano, huchukua siku tatu hadi sita kabla ya dalili za mwanzo kuanza kujitokeza. Dalili za mwanzo za homa ya manjano ni pamoja na:

  • Homa 
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya mgongo
  • Kukosa hamu ya kula (anorexia)
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Uchovu na udhaifu wa mwili

 
Asilimia 15 ya watu wanaopata homa ya manjano huingia kwenye hatua ya pili ya ugonjwa huu, isababishwayo na kuharibika kwa ini. Hatua ya pili  inaambatana na dalili mbaya zaidi zikiwemo:



  • Jaundice (macho, ulimi na viganja kubadilika kuwa rangi ya njano)
  • Maumivu makali ya tumbo
  • Kutapika damu
  • Kutokwa na damu machoni na mdomoni (hemorrhage)
Mgonjwa akifanikiwa kupona ugonjwa huu, atakua amejijengea kinga hivyo hataweza kupata homa ya manjano maisha yake yote
NJIA ZA KUJIKINGA NA HOMA YA MANJANO
Mbinu za kujikinga na homa ya manjano zinahusisha kujikinga kuumwa na mbu, na nyingi zinafanana na zile za kujikinga na malaria pamoja na dengue fever. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kujikinga na homa ya manjano
:

  • Vaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri
  •  Pulizia dawa ya mbu kwenye nyumba ili kuua mbu
  •  Tokomeza mazalia ya mbu kwa kufukia maji yaliyotuama, ikiwa na pamoja na makopo, vifuu pamoja na vitu vingine vinavyoweza kukinga maji.
  • Mtu akigundulika kwamba ana homa ya manjano atibiwe haraka ili kuzuia ugonjwa kusambaa
  • Usichangie sindano pamoja na watu wengine, kwani kuna hatari ya kuambukizwa magonjwa mengi ikiwemo homa ya manjano.

Kama una swali,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu 

namba 0769368546,0719097574 na 0754301115

pia 
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni