MTINDI (YOGURT) |
PAPAI (PAPAYA) |
KWA njia moja au nyingine, unajikuta tumbo limechafuka kwa kujaa gesi, kuuma na hata kuunguruma, unahisi unahitaji kunywa dawa ili litulie. Katika makala ya leo utajifunza njia bora ya kutuliza mchafuko wa tumbo kwa kutumia vyakula badala ya dawa za kisasa ambazo hutuliza dalili na haziondoi tatizo.
CHANZO
Kabla ya kukimbilia kwenye tiba, ni vizuri kwanza kujua chanzo cha tatizo na katika hili unahitaji kujua ni vyakula gani ukila vinasababisha matatizo ya tumbo. Aina ya vyakula inaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu lakini kuna aina ya vyakula vinajulikana zaidi kusababisha matatizo ya tumbo.
tumbo lako kuwa safi wakati wote:
PAPAI (PAPAYA)
Baadhi ya utafiti uliyopo, unaonesha kwamba ‘enzyme’ waliyomo kwenye papai husaidia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kulifanya tunda hili kuitwa na mtafiti wa zama za kale Christopher Columbus kama ‘tunda la malaika’.
Watafiti wamebaini kuwa tunda hili, lenye ladha tamu na harufu nzuri, huboresha mfumo wa usagaji chakula, husafisha utumbo, huzuia magonjwa ya uvimbe tumboni na huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
“Vitamini na virutubisho vya papai vina faida nyingi, lakini faida kubwa ya papai ipo kwenye kirutubisho (Enzyme) aina ya ‘Papain’ ambacho hujulikana kwa uwezo mkubwa ilionao wa usagaji mzuri wa chakula tumboni.
Mwandishi huyo anaongeza kwa kusema kuwa papai limekuwa likitumika kama tiba tangu karne ya 18, lakini utafiti wa kisayansi haukugundua faida za papai hadi mwaka 1870 wanasayansi walipogundua kirutubisho cha ‘papain kilichomo kwenye papai na tangu wakati huo tafiti nyingi zimekuwa zikifanywa kuhusu faida za tunda hili na uwezo wa tiba iliyonalo.
MTINDI (YOGURT)
Hata kama wewe si mpenzi wa mtindi, jaribu kunywa na utaupenda, hasa uwezo wake wa kuondoa matatizo ya kujaa gesi tumboni pamoja na matatizo mengine. Mtindi mzuri ni ule ‘plain’ ambao haujachanganywa na ladha au vitu vingine kwa lengo la kuongeza
ladha. Bakteria asilia waliyomo kwenye maziwa mtindi ndiyo hufanya usagaji wa chakula kuwa mwepesi.
Mwisho, ili kupata faida ya papai na mtindi kama ilivyoelezwa hapo juu, ni vizuri ukala mara kwa mara kama siyo kila siku, kabla au mara baada ya kula vyakula ambavyo vinaweza kukuletea shida tumboni, au ukaweka mazoea ya kula kila siku ili kuliweka tumbo lako katika hali salama.
Kunywa Maji Mengi Ya Uvuguvugu.
Kwa Mtu Mgonjwa wa Maradhi yoyote inatakikana awe anakunywa maji Uvuguvugu unapo amka
Asubuhi kabla ya kupiga mswaki unywe Glasi 2 za Maji ya Uvugvugu na baada ya kupiga Mswaki
anywe glasi 1 na kabla ya kunywa chai unywe Glasi moja ya maji moto kila siku afanye hivyo
kwa wakati wa asubuhi.
Na Wakati wa mchana Dakika 15 au dakika 30 kabla ya kula chakula cha mchana unywe maji ya moto au Maji ya Uvuguvugu Glasi 1.
Na Wakati wa chakula cha Usiku unatakiwa unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 2 kabla ya kula chakula cha usiku.
na unywe Maji Ya Uvuguvugu Glasi 1 kabla ya kwenda kulala usiku.
Endapo utafanya hivyo vyote tumbo bado likaendelea kuunguruma tufikie haraka sana lupimo sanitarium clinic,kwa matibabu zaidi, tupo mikoa mbalimbali hapa nchini kama ifuatavyo:
IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU
NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA
MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA
C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI
MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU
KALFONIA,
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba
0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni