Katika
mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za
mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya
pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu
hujulikana kwa jina la Peripheral
Neuropathy.
Mwili
wa binadamu hutawaliwa na mifumo ya neva au kwa kitaalamu Nervous
System, ambapo katika mifumo hii kuna mfumo mkuu, central nervous system
(ubongo na uti wa mgongo) na pia kuna mfumo wa pembezoni ambao ni kazi
za mwili mbali na ubongo na uti wa mgongo (peripheral nervous system),
mfumo huu wa pembezoni hujumuisha kazi za misuli, mapigo ya moyo,
mmeng’enyo wa chakula tumboni, uwezo wa kuhisi baridi/joto, kugusa vitu
na kujua ukali wa ncha ya kitu na kadhalika.
Matatizo
haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu)
husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili
(miguuni au mikononi) na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva
katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili
zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo: Mtu kuhisi ganzi,
maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi, kuhisi kama umevaa
soksi au gloves wakati hujavaa, kuhisi kama kuna kitu cha ncha kali
kinakuchoma miguuni au kwenye vidole, kushindwa kushika au kunyanyua
kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
Kupungua
kwa virutubisho mwilini, katika hili tunamaanisha mwili kutokuwa na
vitamini vya kutosha na hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B
Complex).
Matumizi
ya dawa, mtu kuwa katika matumizi ya baadhi ya dawa, mfano dawa za
kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi huweza
kumsababishia mtumiaji matatizo ya neva.
Uzito
mkubwa wa mwili, hii hupelekea maumbile ya viungo vya mwili mfano umbile
la uti wa mgongo lionekane tofauti na ilivyo kawaida, kubadilika huku
husababisha baadhi ya neva katika uti wa mgongo zikandamizwe zaidi na
misuli/uzito wa mwili na hivyo kusababisha neva hizo zishindwe kufanya
kazi vizuri, matokeo yake ni wewe kuanza kuhisi maumivi au kufa ganzi
kwa miguu.
Ugonjwa wa kisukari, mtu mwenye tatizo la kisukari huwa hatarini zaidi kuugua au kupata matatizo ya neva, (diabetic polyneuropathy).
Shinikizo
la damu, mtu kuwa na shinikizo kubwa la damu (High blood pressure) pia
ni kihatarishi kinachoweza kumfanya mtu apate ugonjwa huu wa neva.
Baadhi
ya vitu hatarishi vinavyoweza kumfanya mtu apate matatizo haya, vinaweza
kuepukika kwa mtu kuyabadili maisha yake mfano, kama ulikuwa hufanyi
mazoezi ya mwili, basi ujitahidi kuupa mwili mazoezi ili kupunguza uzito
wa mwili, kuepuka magonjwa ya kisukari na kuepuka kuwa na shinikizo
kubwa la damu, kula chakula chenye virutubisho vya kutosha na fuata
maelekezo ya wataalamu wa afya kuhusu matumizi sahihi ya dawa na kanuni
za kukufanya uishi huku ukiwa na afya bora.
kama una tatizo hilo tufikie haraka lupimo sanitarium clinic kwa matibabu zaidi katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini,
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA
IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU
NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA
MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA
C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI
MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU
KALFONIA,
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba
0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni