Jumatatu, 16 Novemba 2015


UGONJWA WA HOMA YA INI.

Mgonjwa mwenye virusi vya Hepatitis B ngozi na macho yake vikiwa vya njano.

HEPATITIS B NI NINI?
Hepatitis B ni virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Homa ya Ini.
Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye KIFO.
Inakadiriwa watu milioni 350 duniani wameathirika na ugonjwa huu ambapo watu 620,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa huu.

Virusi vya Hepatitis baada ya kulishambulia ini.

HOMA YA INI INASABABISHWA NA NINI?
Ugonjwa huu husababishwa na virusi waitwao Hepatitis B (HBV) ambao hukaa katika ini, damu na baadhi ya majimaji mwilini.

UNAAMBUKIZWAJE?
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia zifuatazo:
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi 'denda'
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki

Mojawapo ya njia zinazoambukiza ugonjwa wa Homa ya Ini.

NB: Ugonjwa huu hauambukizwi kupitia chakula, maji au kushikana mikono na waathirika.
DALILI ZAKE
Dalili za ugonjwa huu huchukua muda mrefu kuonekana, zikionekana mgonjwa anakuwa tayari ameathirika sana na ni kama ifuatavyo:

-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili kuwa dhaifu
-Homa kali
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupungua uzito
-Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
-Macho na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo mweusi


TIBA
  

Mgonjwa akiwahi hospitali atapatiwa dawa za kupambana na virusi kuvipunguza nguvu za kushambulia ini.
-Kupandikiza ini ambapo ini lililoathirika huondolewa na kuwekwa ini lingine japo ni vigumu kupata ini salama.
-Mgonjwa anashauriwa kuacha kutumia pombe, madawa ya kulevya na vitu vingine vinavyochosha ini.


Inawezekana unasumbuliwa na tatizo hili la ugonjwa wa homa ya ini na umeenda katika hospitali mbalimbali imeshindikana, tufikie lupimo sanitarium clinic tukutibu kwani tunazo mashine za kisasa kabisa zinazoongozwa na komputer na kubaini jinsi ugonjwa huo ulivyokuathiri, tumewatibu wengi waliokuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo na wamepona.
 

HII NI MIKOA TUNAYOPATIKANA,

VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,  

kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni