Aina saba za matatizo ya kusahau
1. KUSAHAU KWA MUDA MFUPI
(TRANSIENCE)
Hii ni hali ya kusahau habari au
matukio fulani yaliyopita. Tatizo hilo humfanya mtu asahau habari ambayo
ameipata muda mfupi. Hata hivyo, habari ambayo mtu atakuwa haihitaji kuitumia
mara kwa mara ni rahisi kuisahau.
Japokuwa hali ya kusahau mambo kwa
muda mfupi inaweza kuonekana kama ni dalili ya udhaifu wa kumbukumbu,
wanasayansi wa masuala ya akili huiona hali hiyo kuwa ni ya manufaa kwani
huisafisha akili kwa kuondoa kumbukumbu ambazo hazitumiki na kuingiza
kumbukumbu mpya na zenye manufaa.
2. USAHAULIFU WA KUTOTILIA MAANANI
MAMBO (ABSENTMINDEDNESS)
Aina hii ya usahaulifu hutokea iwapo
mtu hatilii maanani jambo fulani. Mfano, unaweza kusahau ulipoweka kalamu yako
kwa sababu hukuweka maanani mahali ulipoiweka. Inawezekana ulikuwa unafikiria
kitu kingine wakati unafanya hivyo, au huenda ulikuwa hufikirii chochote ila
akili yako haikuchukua kumbukumbu ya tendo ulilolifanya. Usahaulifu huu pia ni
pamoja na kusahau kufanya jambo fulani katika muda wake, kama vile kutumia dawa
au kwenda kutimiza ahadi.
3. KUTOKUMBUKA MARA MOJA (BLOCKING)
Mtu anaweza kukuuliza swali ambalo
unalifahamu kabisa, lakini ukashindwa kulijibu mara moja kwa kutolikumbuka. Huu
huenda ni aina kubwa zaidi ya usahaulifu ambapo akili hushindwa kuifikia
kumbukumbu mara moja.
Wanasayansi huamini kwamba
usahaulifu huu ni kawaida kulingana na umri wa mtu unavyozidi kuongezeka .
Pia, usahaulifu huu huchangia kwa
kiasi kikubwa kwa watu wenye umri mkubwa katika matatizo ya kukumbuka majina ya
watu na vitu vingine. Hata hivyo, utafiti umeonesha kwamba watu huweza kunasa
nusu ya kumbukumbu zao katika kipindi cha dakika moja.
4. KUMBUKUMBU POTOFU
(MISATTRIBUTION)
Kumbukumbu potofu hutokea wakati mtu
anapokumbuka sehemu ya jambo kwa usahihi, lakini akakosea maelezo kadhaa kama
vile wakati, mahali, au mtu husika. Usahaulifu mwingine wa aina hii ni pale
unapoamini kwamba dhana uliyokuwa nayo ni halisi wakati ukweli ni kwamba
ilitokana na kusoma mahali au kuisikia kwa watu wengine, lakini ukawa umesahau
ukweli huo.
Aina hii ya usahaulifu iko zaidi
katika wizi usiokusudiwa wa kazi za sanaa ambapo mwandishi, kwa mfano,
anaandika habari fulani akidhani ni ya kwake kumbe aliisoma mahali fulani.
Kuhusiana na matatizo mengine ya
kupoteza kumbukumbu, kumbukumbu potofu huendana na umri. Mtu anapozidi kuzeeka
anakuwa anaingiza habari chache zaidi kwenye akili yake, kwani akili yake
inakuwa haina uwezo wa kudaka habari kwa haraka.
5. KUDAKA HABARI POTOFU
(SUGGESTIBILITY)
Kudaka habari potofu pia kunaathiri
mfumo wa kumbukumbu, ambapo mtu huiweka habari hiyo katika akili yake akifahamu
kwamba ni jambo la kweli wakati siyo kama alivyoliona wakati likitokea.
Alidanganyika.
6. KUMBUKUMBU ILIYOJENGA DHANA
TAYARI (BIAS)
Kumbukumbu ya mtu ambayo tayari
imejenga dhana fulani inayotokana na mambo aliyoyaona, imani fulani, mambo
ambayo ameyapa mwenyewe kipaumbele, itamletea matatizo.
Dhana ambayo tayari unayo kichwani
ni dhahiri itaathiri mawazo yako, hivyo kila ukitaka kukumbuka jambo fulani
mawazo yako na dhana zako ni lazima yatatawaliwa na habari ambayo unaikumbuka.
Lakini, pamoja na hali hii,
wanasayansi hawajafanya utafiti mkubwa kuhusu dhana aliyo nayo mtu na jinsi
inavyoweza kuathiri kumbukumbu zake, pia hawajafahamu vyema iwapo hali hiyo
huenda sambamba na umri.
7. KUMBUKUMBU MBAYA (PERSISTENCE)
Watu wengi husumbuliwa na tatizo la
kusahau mambo kila wakati lakini katika matukio mengine, kuna watu ambao
huteseka kwa kuwa na kumbukumbu mbaya ambazo hutaka kuzisahau, lakini
wanashindwa.
Kuendelea kwa kumbukumbu mbaya na
zenye matukio yasiyopendeza au yenye kuleta hisia mbaya ni moja ya matatizo ya
kumbukumbu.
Baadhi ya kumbukumbu hizi huonesha
matukio ya kutisha na mengine ambayo huwa ni ya kufikirika na hivyo kuleta
hisia mbaya.kama unasumbuliwa na tatizo la kusahau tufikie lupimo sanitarium clinic katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni