MATATIZO YA KUKOSA USINGIZI {INSOMNIA}
Insomnia ni nini?
Huu ni ugonjwa ambao huambatana na tabia
zifuatazo..
- · Kushindwa kupata usingizi kabisa.
- · Kulala na usingizi kuisha usiku sana na kushindwa kulala tena.
- · Kubadilika kwa mfumo wa kulala I:e mtu wa aina hii husinzia mchana na kukosa usingizi usiku.
- · Kusinzia haraka baada ya kufika kitandani na usingizi kuisha haraka kisha kushindwa kupata usingizi tena.
Ugonjwa huu husababishwa na nini?
- · Utumiaji wa madawa kama cocaine, nicotine,cafaine na unywaji wa pombe uliopitiliza.
- · Magonjwa ya moyo ambayo humfanya mtu ashindwe kupumua vizuri wakati wa kulala.
- · Maumivu makali ya mwili kama kidonda, kuvunjika mfupa, misuli na kadhalika.
- · Matatizo ya mfumo wa chakula kama kiungulia na kupata choo ngumu.
- · Mazingira mabaya ya kulala kama kelele nyingi na harufu kali.
- · Msongo mzito wa mawazo
- · Magonjwa ya akili mfano schizophrenia na dementia.
- · Utumiaji wa ovyo wa dawa za kuleta usingizi mfano diazepam maarufu kama valiam.
- · Upungufu au ongezeko la homoni za uzazi hasa kipindi cha uzeeni kwa wanawake{menopause} .
MATIBABU
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyka katika sehemu kuu mbili
kama ifuatavyo.
Matibabu yasiyotumia dawa{non pharmacological treatment}:
kikubwa kinachofanyika hapa ni kuacha tabia zote ambazo ziko
ndani ya uwezo wako ambazo zinakufanya ukose usingizi kama nilivyozianisha hapo
juu. Aina hii ya matibabu ni nzuri na bora zaidi kuliko matumizi ya dawa za
kuleta usingizi ambazo mara nyingi zinasababisha kuzitegemea yaani bila hizo
haulali{dependence} na kuleta madhara mengine ya kiafya.
- · Usile chakula kingi wakati wa kwenda kulala.
- · Usinywe kahawa wakati wa kwenda kulala
- · Kitanda kitumike kama sehemu ya kulala sio kuangalizia video na kucheza game.
- · Usiangalie video za kutisha wakati wa kwenda kulala.
Matibabu ya dawa {Pharmacological treatment}
Magonjwa yanayosababisha{underlying causes} mtu kushindwa kulala
yanatakiwa yatibiwe kwanza. mfano maumivu
makali ya mwili kutokana na magonjwa
flani.
Baadhi ya dawa hutumika kwa mda mfupi kutibu ugonjwa huu kwa
kupunguza dalili kali za mwanzo kisha
matibabu ya bila dawa huendelea.
Dawa hizo ni kama zifuatazo.
- · Antidepressant mfano amitripyline.
- · Benzodiapines mfano diazepam
- · Opiods mfano morphine pale mgonjwa anapokua na maumivu makali sana.
Kuna dawa nyingi sana zinazotumika ila hizo ni baadhi tu na
ambazo zinapatikana kwenye nchi yetu kirahisi.
kama unatatizo hilo tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni