Kukabiliana na Matatizo ya Kukoma kwa Hedhi
“Ghafula nilihisi nimelemewa na huzuni bila kujua sababu. Nililia na kuanza kujiuliza ikiwa ninarukwa na akili.”—Rondro, * mwenye umri wa miaka 50.
“Unaamka asubuhi na kupata nyumba yako ikiwa shaghalabaghala. Huwezi kupata kitu chochote unachotafuta. Mambo ambayo ulikuwa ukifanya kwa urahisi, sasa yanaonekana kuwa magumu sana, na hujui ni kwa nini hali iko hivyo.”—Hanta, mwenye umri wa miaka 55.
WANAWAKE
hao si wagonjwa. Wanapitia tu kipindi cha kukoma kwa hedhi, ambacho ni
badiliko la kiasili katika maisha ya mwanamke anapoacha kuwa na uwezo wa
kupata watoto. Ikiwa wewe ni mwanamke, je, unakaribia kipindi hicho? Au
je, unapitia kipindi hicho sasa hivi? Vyovyote vile, kadiri ambavyo
wewe na wapendwa wako mnajifunza kuhusu kipindi hiki cha mabadiliko,
ndivyo mtakavyoweza kukabiliana kwa njia inayofaa na matatizo
yanayohusiana nacho.
Kipindi cha Kukoma Hedhi
Wanawake
wengi huanza kipindi hicho wakiwa na umri wa miaka 40 na kitu, lakini
wengine huanza wakiwa wamechelewa wakiwa na miaka 60 na kitu. *
Kwa wanawake wengi, hedhi hukoma hatua kwa hatua. Kwa sababu ya
kubadilika-badilika kwa kiwango cha homoni kinachotokezwa, huenda
mwanamke akakosa kupata hedhi pindi kwa pindi, akapata hedhi wakati
ambao hakutarajia, au akavuja damu nyingi isivyo kawaida wakati wa
hedhi. Wanawake wachache hukoma kupata hedhi ghafula, yaani, wanakosa
hedhi mwezi mmoja na huo unakuwa mwisho wa kuipata.
Kitabu kuhusu kukoma kwa hedhi (Menopause Guidebook)
kinasema: “Kipindi hicho huwa tofauti kwa kila mwanamke.” Kitabu hicho
kinaendelea kusema hivi: “Matatizo ya kawaida yanayohusiana na kipindi
hicho ni kupata joto la ghafula mwilini,” ambalo huenda likafuatwa na
kuhisi baridi. Dalili hizo zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na
kuishiwa na nguvu. Matatizo hayo huendelea kwa muda gani? Kulingana na
kitabu hicho, “wanawake fulani
hupatwa na joto la ghafula mwilini kwa mwaka mmoja au miwili wakati wa
kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi. Wengine hupatwa na hali hiyo kwa
miaka mingi, na wachache sana husema kwamba wao hupatwa na joto la
ghafla mara kwa mara maisha yao yote.” *
Kwa
sababu ya kubadilika-badilika kwa kiwango cha homoni, huenda mwanamke
akashuka moyo, hisia zake zikabadilika-badilika na hilo linaweza
kumfanya alielie bila sababu, na pia asiwe makini sana na asahau mambo.
Licha ya hayo, kitabu The Menopause Book kinasema kwamba “kuna
uwezekano mkubwa kwamba mwanamke hatapatwa na mambo hayo yote.” Kwa
kweli, wanawake fulani hupata matatizo machache sana na wengine hawapati
matatizo yoyote wakati wa kipindi hicho.
Jinsi ya Kukabiliana na Kipindi Hicho
Kubadili
mtindo wa maisha kunaweza kupunguza baadhi ya matatizo hayo. Kwa mfano,
wanawake wanaovuta sigara wanaweza kupunguza mara ambazo wanapatwa na
joto la ghafula kwa kuacha kuvuta sigara. Wanawake wengi hunufaika kwa
kubadili mazoea yao ya kula kama vile kupunguza au hata kuacha kunywa
kileo, vinywaji vyenye kafeini, na vyakula vyenye sukari au vikolezo
ambavyo vinaweza kusababisha joto la ghafula mwilini. Bila shaka, ni
muhimu kula vyakula mbalimbali na vyenye lishe.
Kufanya
mazoezi husaidia sana kupunguza matatizo yanayohusianishwa na kukoma
kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kupunguza kukosa usingizi na
kusaidia kuboresha hali ya kihisia na pia kuimarisha mifupa na afya ya
mtu kwa ujumla. *
Eleza Mambo Waziwazi
Rondro
aliyenukuliwa mwanzoni mwa makala hii anasema hivi: “Usiteseke
kimyakimya. Ukiwaeleza wapendwa wako mambo waziwazi, hawatakuwa na
wasiwasi kuhusu hali yako.” Jambo hilo linaweza kuwafanya hata
wakuonyeshe subira na huruma zaidi. “Upendo ni wenye ustahimilivu na
wenye fadhili,” linasema andiko la 1 Wakorintho 13:4.
Wanawake
wengi hunufaika kwa kusali, kutia ndani wale ambao wanahuzunika kwa
sababu kipindi hicho kinawafanya wapoteze uwezo wao wa kupata watoto.
Biblia inatuhakikishia hivi: “[Mungu] hutufariji sisi katika taabu zetu
zote.” (2 Wakorintho 1:4, Biblia Habari Njema)
Pia inafariji kujua kwamba kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi ni cha
muda tu. Kipindi hicho kinapokwisha, wanawake ambao hutunza afya yao,
wanapata tena nguvu na kuendelea kufurahia maisha.
Inawezekana unasumbuliwa na tatizo holo na limekusumbua kwa muda mrefu bila kupata matibabu stahiki tunaomba utufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni