Alhamisi, 3 Desemba 2015


CHANZO, DALILI NA MATIBABU YAKE

Mafua yanaweza kuwa moja ya sababu  inayofanya watu wengi kushindwa kwenda kazini, kuhudhuria shuleni  au kupunguza ufanisi wa utendaji kazi na kwenda kutafuta msaada wa kitabibu hospitalini. 


Ingawa dalili za mafua sio mbaya sana na hazidumu kwa zaidi ya wiki tatu, utafiti unaonyesha kuwa mafua huchangia kukwamisha maendeleo kwa kiasi fulani. Utafiti  uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Archival of Internal Medicine, umebaini mafua yanaweza kusababisha mgogoro wa uchumi wa mtu ikiwa ataugua kwa kpindi kirefu na kushindwa kufanya kazi zake za kila siku za kumwingizia kipato.


Utafiti huo uliohusisha kaya 4,051 huko Marekani, ulionyesha kuwa takribani dola bilioni 40 za Serikali ya Marekani hupotea kila mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua (respiratoy diseases) yatokanayo na virusi vya mafua. 




KISABABISHI CHA MAFUA.


Mafua yanasababishwa  na virusi vya aina mbalimbali. Kuna zaidi ya aina 200 ya virusi visababishavyo mafua. Kirusi aina ya ‘’rhinoviruses’’ ndicho kinachosababisha mafua kwa asilimia kubwa 30 hadi 80 ukilinganisha na virusi vya aina nyingine. Virusi vingine vya mafua ni human coronavirus, influenza viruses, adenoviruses, human parainfluenza viruses, human respiratory syncytial virus, enteroviruses, metapneumovirus n.k. Mara nyingi mtu anaweza kuambukizwa virusi vya mafua vya aina mbalimbali kwa maana ya kimoja au zaidi ya kimoja vyote katika kipindi kimoja.


VIPINDI AMBAVYO MAAMBUKIZI YA MAFUA YAPO JUU.


Kwa kawaida mlipuko wa mafua hutokea zaidi wakati wa mvua na baridi kali. Hii ni kutokana na uwezo wa virusi vya mafua kusambaa kwa kasi zaidi kipindi cha baridi kuliko vipindi vingine. Sababu nyingine ni kwamba wakati wa baridi ni rahisi kupata maambukizi ya virusi vya mafua kwa njia ya hewa kupitia mfumo wa kupumua.


SEHEMU AMBAZO NI RAHISI KUPATA MAAMBUKIZI YA MAFUA.


1. Utafiti umebaini  kuwa watu wanaosafiri kwa ndege kwa muda mrefu kuanzia saa moja na kuendelea, wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa mafua.
Sababu hii kwa mujibu wa utafiti ni kwamba, kinga ya miili ya abiria wa kwenye ndege dhidi ya mafua  huparaganyika kutokana na ukavu wa hewa ndani ya ndege. Unyevu wa hewa katika ndege inayosafiri zaidi ya saa moja hupungua kufikia kiasi cha asilimia 10 hadi 5.


Ukavu wa hewa au kupungua kwa unyevu katika hewa, husababisha vinywele (cilia) katika njia ya hewa kushindwa kukamata virusi vya mafua na kuvisafirisha hadi tumboni ambako kwa kawaida huunguzwa kwa tindikali (acid) ya tumboni na kufa. Mfumo wa upumuaji katika njia ya hewa huwa katika hali bora  pale unyevu wa hewa unapokuwa kati ya asilimia 20 na 60.


2. Mahali penye mkusanyiko wa watu wengi. Mfano: Ndani ya daladala au popote pale ambapo hakuna mzunguko mzuri wa hewa. 




SABABU ZINAZOCHANGIA KUWEPO KWA MAFUA.


1. Uchafu wa mazingira ambao hupelekea kuchafuka kwa hewa hasa vumbi la ndani ya nyumba.


2. Moshi mfano wa sigara, kuchoma kwa taka n.k


3. Hali ya baridi na matumizi ya pafyumu zenye harufu kali.


DALILI ZA MAFUA.
 

Ugonjwa wa mafua unaweza kusababisha hali zifuatazo:

  • Kupiga chafya mara kwa mara.
  • Kutokwa na makamasi mepesi au mazito puani.
  • Kikohozi
  • Homa kali na
  • Kuziba kwa pua.
Dalili zingine ni pamoja na kichwa kuuma, uchovu wa mwili, kupoteza hamu ya kula chakula na hali ya kuwasha kwa koo.
Dalili hizi huanza ndani ya saa 16 tokea wakati wa kugusana na virusi au visababishi vya mafua. Hali huwa mbaya katika kipindi cha saa 24 hadi 72 ambapo virusi huwa vingi katika majimaji yatokayo puani. Katika kipindi hiki mgonjwa wa mafua huwa na uwezo mkubwa wa kuambukiza watu wengine. Dalili za ugonjwa wa mafua hutegemea zaidi uwezo wa mwili kupambana na ugonjwa.


Mafua yanaweza kusababisha matatizo makubwa katika mfumo wa kupumua hasa pale yanapoambatana na mambukizi ya pili mfano maambukizi mengine yaliyosababishwa na bakteria. Matatizo yanaweza kuwa makubwa zaidi kwa watoto wachanga, wazee au kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini. 




Mafua pia yanaweza kusababisha mambukizi ya bakteria katika masikio na kooni. Katika hali hii mgonjwa hutoa makohozi au makamasi. Katika hatua hii, mgonjwa wa mafua anaweza kupata homa kali sawa na mtu mwenye homa ya Malaria.


Kabla ya kusoma njia za kukabiliana na mafua. Angalia video inayoeleza namna ya kutengeza juisi ya kutuliza mafua.


 NJIA ZA KUKABILIANA NA MAFUA.

Njia zinazosaidia kukabiliana na tatizo la mafua ni pamoja na


  •  Kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka kushika shika pua na macho.
  • Kufunika pua na mdomo kwa kitambaa wakati wa kupiga chafya.
  • Kupumzika muda wa kutosha.
  • Kunywa maji na juisi za matunda kwa wingi. Mfano juisi zilizotengenezwa na matunda yenye vitamin C kwa wingi kama mananasi, machungwa, malimao n.k
      
  • Kuondoa maumivu na homa ili kupata nafuu. Unaweza kuondoa maumivu kwa kumeza dawa za kutuliza maumivu. Mfano: Panadol, Paracetamol n.k
  • Kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.
  • Kula mboga mboga na matunda kwa wingi kwani ni njia bora ya kupunguza uwezekano wa kupata mafua mara kwa mara kwasababu vitamin C na madini ya zinc yanayopatikana katika vyakula hivi huongeza na kuimarisha kinga ya mwili.
  • kama una mafua sugu tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.
  • VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA, 


    kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.


     

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni