Umuhimu wa Maji mwilini
Pili, unywaji wa maji mengi hutupunguzia uwezekano wa kupata magonjwa kama ya moyo, hivyo inashauriwa kwa siku tunywe zaidi ya bilauri mbili za maji na kuendelea. Tatu, maji huongeza nguvu mwilini kwani unapokua na upungufu wa maji, unaanza na kusikia kiu ambayo huenda kupelekea kujisikia uchovu, misuli kuchoka, kizunguzungu na ishara nyingine za kunyongonyeza mwili.
Nne maji ni dawa ya maumivu ya kichwa. Mara kwa mara tuumwapo kichwa pengine ni upungufu wa maji ndio uliopelekea maumivu haya, lakini tunywapo maji basi maumivu huoondoka. Kuna sababu nyingine zinazopelekea vichwa vyetu kuuma lakini, ukosefu wa maji mwilini ni sababu inayojulikana zaidi.
Kama hatukuwahi kuwa na mazoea ya kunywa maji kwa kiwango hicho mwanzo huw ni mgumu, lakini waweza anza mdogo mdogo kwa bilauri mbili, kesho yake tatu, inayofuata nne mpaka tufikie hizo lita mbili.
Kuna wale wenzangu na mimi watakaosema maji hayana ladha, nakupa maarifa kidogo waweza changanya na kikorombwezo upendacho kuyapa ladha ili upate hamu yakuyanywa, maana mwisho wa siku ni lazima kunywa maji, Waweza tumbukiza kijipande cha ndimu, au chungwa au kitu kingine unachopenda ladha yake
Umuhimu
wa Tano wa maji mwilini ni kwamba, unywaji maji hupelekea kusafisha
ngozi yako, na mara kwa mara Rafiqs wengi wamejivunia kuwa na ngozi bora
baada ya unywaji wa maji wa kutosha. Haiwezi tokea mara moja ila baada
ya wiki moja utaanza kuona mabadiliko ya ngozi yako na itaanza kung'ara.
Sita, mfumo
wa kuchanganya chakula ndani ya miili yetu (digestive system) unahitaji
maji mengi ili kufanikisha kazi yake kifasaha, hivyo yatupasa
kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi yake vyema katika muda sahihi kwa
kunywa maji ya kutosha. Pia maji husaidia kuponesha maumivu ya vichomi
vya tumbo, na pia hutupa urahisi pale tuendapo haja kubwa, kwani tunakua
hatuna ukosefu wa maji mwilini. Maji husaidia pia kuondosha uchafu
ndani ya miili yetu na kuacha mwili ukiwa msafi.
Saba, Kwa
unywaji mwingi wakati wa mfumo wa kuchanganya chakula unaendelea,
imeonekana kuwa maji husaidia kupunguza uwezekani wa kupata saratani ya
colon kwa asilimia 45, asilimia 50 ya saratani ya kibofu cha mkojo na
pia hupunguza uwezakano wa kupata saratani ya matiti kwa kina mama.
Nane, Kuwa na
ukosefu wa maji mwilini husababisha kukurudisha nyuma katika swala zima
la mazoezi na kukufanya iwe ngumu kunyanyua vyuma vya mazoezi, pamoja
naa kufanya mazoezi mengine, hivyo basi inashauriwa kunywa maji kabla,
wakati na baada ya mazoezi ili uweze kuyafanya vyema na katika hali
salama.
kwa maelezo zaidi msomaji wetu wa blog hii ya lupimo sanitarium clinictufikie katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni