UTI: NI UGONJWA WA MAAMBUKIZA YA NJIA YA MKOJO YANAYOATHIRI MAMIA YA WANAWAKE NCHINI
Wanawake wanapata UTI kwa urahisi sana kuliko wanaume kwa sababu mirija
ya mkojoya mwanamke ni mifupi ambayo huruhusu bacteria kuingia kwa
urahisi tofauti na ya mwanaume.Katika magonjwa yanayosumbua wanawake wengi na watoto nchini
hivi sasa ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo U.T.I (Urinary Tract
Infection).
Wakati wanawake wengi wanaougua ugonjwa huu
wakihangaika kila siku kupata tiba yenye usahihi, wataalamu wa afya
wanasema unapojiimarisha mwilini kwa muda mrefu huathiri figo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Afya ya
Uzazi kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk Cyriel Massawe anasema,
tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo
unaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema,
huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya.
“Bakteria hawa hupatikana ndani ya sehemu za siri
za mwanamke, bakteria hao wakiwa ndani ya uke hawana madhara kabisa,
lakini pindi uke unapopata mchubuko bakteria hawa huanza kuathiri kibofu
cha mkojo na mtu kuanza kupata madhara,” anasema na kuongeza:
Wanawake wanapata UTI kwa urahisi sana kuliko
wanaume kwa sababu mirija ya mkojoya mwanamke ni mifupi ambayo huruhusu
bacteria kuingia kwa urahisi tofauti na ya mwanaume.
Vyanzo vya UTI
Dk Masawe anasema kuna vyanzo vingi
vinavyosababisha ugonjwa huu, ikiwamo matumizi ya maji machafu wakati
wa kujisafisha au kuoga huweza kuweka bakteria kwa urahisi na mwanamke
kupata UTI.
Uchafu wa vyoo umetajwa kuwa sababu nyingine,
kwani matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu huweza kusababisha mwanamke
kupata UTI kwa sababu ndani ya choo kuna bakteria wengi ambao wanaweza
kusababisha UTI.
Anasema kufanya ngono mara kwa mara ni tatizo
kubwa ambalo ndilo linafanya wanawake (kwa habari nyingi zaidi usisahau kulike page yetu ya mdadisi mambo kwa kuclick hapa)wengi kupata UTI siku hizi, kwani
wakati wa ngono msuguano huwa mkubwa ambao hufanya bakteria kutoka
kupitia majimaji ya ukeni na kuingia katika njia ya mkojo.
“Mwanamke ambaye anafanya ngono mara kwa mara yuko
kwenye hatari ya kupata UTI kuliko yule ambaye hafanyi ngono mara kwa
mara. Pia matumizi ya nguo za ndani za mitumba bila kufua husababisha
kwa urahisi mwanamke kupata UTI,” anasema.
Hata hivyo anasema tatizo kubwa limetajwa kuwa
kemikali, “kemikali zinawaathiri wanawake wengi siku hizi, kutumia sana
kemikali hasa kwenye vipodozi ambavyo kemikali hizi kwa kuwa ni sumu
huenda hadi kwenye kibofu na kuchubua kibofu na hapo ndipo tatizo hilo
huanza.”
Wataalamu wamesisitiza kwamba wengi wamekuwa na tabia ya kubana mkojo kwa muda mrefu, lakini matokeo ya tabia hii ni kupata UTI.
Dalili za UTI
Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mtu kusikia
haja ya kukojoa kila wakati na kusisimka wakati wa kujisaidia, kusikia
maumivu, kutoa mkojo mchafu na hata kutoa haja ndogo iliyochanganyika na
damu.
Mwili kuchoka mara kwa mara, homa za mara kwa
mara, kichwa kuuma mara kwa mara, kubanwa na mkojo halafu ukienda
kukojoa unakuta mkojo kidogo, maumivu wakati wa kukojoa na kiuno kuuma.
Unaweza kuikinga UTI kwa njia mbadala
Mkurugenzi wa Kituo cha huduma ya ushauri nasaha,
lishe na afya COUNSENUTH, Mary Materu anasema, kwa kawaida kila ugonjwa
una tiba mbadala, siyo lazima kwenda hospitali.
“Unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa
kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo
utawahi kabla tatizo halijawa sugu. Kwa maana nyingine, unaweza
kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha
kila siku. Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila
mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha
kabisa,” anasema Materu.
Aidha, anasema njia nyingine ya kuudhibiti ugonjwa
huu ni kunywa maji mengi au kwenda haja ndogo mara baada ya kufanya
tendo la ndoa, kitendo hiki husaidia kuwaondoa mapema bakteria wote
ulioambukizwa wakati wa kujamiiana na mwenzio.
“Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka
ndani ya siku tatu mara baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa
maji mengi na juisi ya matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo
baada ya siku hizo, hiyo itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na
hivyo hauwezi kutibika kwa tiba hii ya nyumbani,” anasema na kuongeza:
“Katika hali kama hii, utakuwa huna njia nyingine
isipokuwa kwenda hospitalini na kuonana na daktari ambaye atakufanyia
uchunguzi na kukupatia dozi sahihi ambayo utatakiwa kuizingatia bila
kukosa. Uamuzi huu ni muhimu hasa kama unasikia maumivu makali ambayo
yanaweza kuwa yanasababishwa na kuathirika kwa figo,” anasema Materu.
Dk Massawe anasema kwa kawaida tiba ya kidaktari
kwa ugonjwa huu huhusisha matumizi ya dawa kali za ‘antibiotics’, ambazo
watu wengi wanazikimbia kutokana na athari zake za baadaye (side
effects).
Lakini ni muhimu kufuata ushauri wa daktari na kumaliza dozi ili kuepuka uwezekano wa kurejea kwa ugonjwa, tena kwa kasi kubwa.
Unaweza kujikinga na UTI
Mkurugenzi kutoka Kituo cha Afya Tiba cha lupimo sanitarium clinic dr john lupimo anasema, ili kujiepusha
na ugonjwa huu, suala la usafi na kuwa na tabia ya kunywa maji ya
kutosha ni jambo muhimu sana.
“Hakikisha unajisafisha vizuri mara baada ya
kwenda haja na kubadilisha mara kwa mara nguo yako ya ndani, hasa kwa
akina mama,” anasema na kuongeza: “Vile vile usikae na haja ndogo kwa
muda mrefu, nenda kajisaidie mara nyingi kadri unavyosikia kufanya
hivyo. Kitu cha mwisho cha kuzingatia kwa mgonjwa wa UTI ni kupunguza
unywaji wa pombe na vinywaji vingine vyenye sukari, kwa sababu sukari ni
chakula cha bakteria hivyo kwa kuendelea kunywa kinywaji chenye sukari
kutaifanya hali kuendelea kuwa mbaya, “ anasema Dk lupimo
Anasema ugonjwa huu ni rahisi kuuepuka kwa mtu anayependa kunywa maji ya kutosha na kunywa juisi halisi kila siku.
Vyakula vinavyokukinga na UTI
Dk lupimo anasema, katika kuudhibiti ugonjwa
huu, pendelea kula vyakula au vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha
vitamini C, ambayo utaipata kwenye matunda ya aina mbalimbali yakiwemo
machungwa, mboga za majani n.k.
“Jiepushe na ulaji wa vyakula vya ‘kupaki’ kama
vile ‘chizi’, chokoleti na bidhaa nyingine zilizotengenezwa kutokana na
maziwa. Pia jiepushe na ulaji wa vyakula vyenye viungo vingi kama pilau,
epuka vinywaji vyenye ‘caffeine’, kilevi na sigara na mwisho achana na
vinywaji kama soda na vinavyofanana na soda,” anasema dr lupimo.
kama tatizo hili unalo na limekuwa sugu halisikii dawa tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM
CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO
SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA
MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA
MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA,
GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA
KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni