ZIJUE SABABU, DALILI NA MADHARA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA MWANAWAKE.
Saratani ya shingo ya
kizazi ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi duniani.
Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea.
Kwa Tanzania, wastani wa wanawake 6,241 huugua saratani hii kila mwaka, ambapo
4,355 kati yao hufa, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani
(W.H.O) ya mwaka 2010.
Saratani ya shingo ya
kizazi ndio saratani ya kwanza kwa wanawake nchini Tanzania, na Saratani namba
moja kwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 44. Tanzania ina wanawake
milioni 10.97 walio na umri wa miaka 15 na kuendelea, ambao wako kwenye hatari
kubwa ya kupata saratani hii. Kwa afrika mashariki, asilimia 33.6 ya wanawake
wote, wanasadikiwa kuwa na virusi aina ya human papilloma virus ambavyo ndio
visababishi vya ugonjwa huu.
Je nini kinasababisha saratani
ya shingo ya kizazi?
Maambukizi ya human papilloma virus ndio yanayosababisha saratani ya shingo ya kizazi. Kuna zaidi ya aina 150 ya virusi hivi vya human papilloma virus, ambapo aina tatu (yaani aina ya 26,53,66) ndio venye hatari sana ya kusababisha ugonjwa huu, aina ya 16 na 18 ndivyo vinavyojulikana kusababisha zaidi ya asilimia 70 ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi. Virusi hivi huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kugusana kwa ngozi ya mtu mmoja na mwengine, na huambukiza wanaume na wanawake.
Maambukizi ya human papilloma virus ndio yanayosababisha saratani ya shingo ya kizazi. Kuna zaidi ya aina 150 ya virusi hivi vya human papilloma virus, ambapo aina tatu (yaani aina ya 26,53,66) ndio venye hatari sana ya kusababisha ugonjwa huu, aina ya 16 na 18 ndivyo vinavyojulikana kusababisha zaidi ya asilimia 70 ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi. Virusi hivi huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kugusana kwa ngozi ya mtu mmoja na mwengine, na huambukiza wanaume na wanawake.
Visababishi vya saratani ya
shingo ya kizazi.
1.
Kuanza
kufanya ngono mapema - Wanawake wanaoanza kujamiana wakiwa na umri wa miaka 16 wako
kwenye hatari baadae kupata saratani ya shingo ya kizazi.
2.
Kuwa
na wapenzi wengi – Mwanamke
mwenye wapenzi wengi au mwenye mwanamume mwenye wapenzi wengi yupo kwenye
hatari ya kupata ugonjwa huu. Utumiaji wa kondomu hupunguza hatari ya kupata
saratani hii, lakini ikumbukwe ya kwamba kondomu sio kinga ya ugonjwa huu.
3.
Maambukizi ya human
papilloma virus.
4.
Uvutaji
sigara – Kemikali
zilizopo kwenye sigara huchanganyikana na seli au chembechembe za shingo ya
kizazi hivyo kuleta mabadiliko katika shingo ya kizazi hatimaye kusababisha
saratani.
5.
Utumiaji wa vidonge
vya kupanga uzazi kwa muda mrefu hasa wale wanaotumia kwa zaidi ya miaka
mitano.
6.
Ugonjwa wa
masundosundo (dalili ni matezi na muda mwingine vidonda katika sehemu ya siri
ya mwanamke). Hii husababishwa na virusi vya human papilloma virus.
7.
Lishe duni au utapia
mlo.
8.
Kuzaa
watoto wengi – Wanawake ambao
wamepata watoto zaidi ya watano wako kwenye hatari kubwa sana ya kupata
saratani ya shingo ya kizazi. Ndio maana mama akishafikisha watoto watano
anashauriwa kufunga kizazi.
9.
Umri
mkubwa – Baada ya
kufikisha umri wa miaka 25, hatari ya kupata saratani hii huongezeka. Wanawake
wenye zaidi ya miaka 45 wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya shingo
ya kizazi.
10.
Uasili
wa mtu – Saratani ya
shingo ya kizazi huonekana sana kwa watu weusi kuliko watu weupe.
11.
Upungufu
wa kinga mwilini – Magonjwa
yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini kama ukimwi huchangia kupata saratani
ya shingo ya kizazi. Hata baadhi ya dawa pia husababisha upungufu wa kinga
mwilini, mfano, dawa zinazotolewa baada ya mgonjwa kupewa kiungo cha mtu
mwengine kama figo,moyo nk.
12.
Historia
ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia – Saratani hii pia inahusishwa na
kiashiria cha aina ya HLA-B7 ambacho kinaweza kurithishwa kwenye familia ya
mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
13.
Matumizi ya dawa aina
ya diethystilbestrol (DES).
14.
Kujamiana
na mwanaume ambaye hajatahiriwa - Tafiti zimeonyesha ya kwamba wanaume ambao hawajatahiriwa wako
katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya human papilloma virus. Hii ni
kutokana na uchafu ndani ya gozi linalofunika kichwa cha uume hivyo kuweka
mazingira mazuri kwa virusi vya human papilloma virus kustawi na hatimaye
kuambukiza mwanamke wakati wa kujamiana.
Dalili na viashiria vya
saratani ya shingo ya kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.
Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.
Dalili au viashiria
vya saratani ya shingo ya kizazi ni;
1.
Kutokwa na damu katika
tupu ya mwanamke (uke) ambayo sio ya kawaida. Damu hii inaweza kuwa matone, au
damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya
hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.
2.
Kutokwa na damu baada
ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.
3.
Maumivu wakati wa
kujamiana.
Dalili za saratani
iliyosambaa ni kama zifuatavyo;
1.
Kupungua kwa hamu ya
kula.
2.
Kupungua uzito.
3.
Kuhisi uchovu.
4.
Maumivu ya nyonga.
5.
Maumivu kwenye mgongo.
6.
Maumivu ya mguu.
7.
Mguu mmoja kuvimba.
8.
Kutokwa na damu nyingi
kwenye tupu ya mwanamke.
9.
Kuvunjika mifupa.
10.
Kutokwa na mkojo au
kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.
Vipimo vya saratani ya shingo
ya kizazi
·
Pap
smear – Chembechembe
au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kutumia hadubini. Kipimo
hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake ili kujua kama wamepata saratani
ya shingo ya kizazi au la. Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu
wa kinga mwilini wanashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara moja kwa mwaka
ili wajue afya yao.
·
Cervical
Biopsy – Kipimo hiki
huhusisha uchukuaji wa nyama kutoka kwenye uvimbe katika shingo ya kizazi na
hupelekwa maabara kuchunguzwa kama kuna saratani au la. Kipimo hiki
kinathibitisha uwepo wa saratani.
·
Colposcopy – Hii ni aina ya darubini inayotumiwa
kuchunguza shingo ya kizazi ili kuangalia kama kuna tishu ambayo si ya kawaida.
Kipimo hiki kinaweza kufanywa na daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama.
·
Cone
Biopsy – Kipimo hiki
hufanywa kwa kuchukua nyama kutoka katika shingo ya kizazi mfano wa koni kwa
uchunguzi zaidi na hufanywa katika chumba cha upasuaji mgonjwa akiwa amepewa
dawa ya nusu kaputi. Hiki kipimo kinaweza kutumiwa kama njia moja ya kutibu
saratani ambayo haijaenea na ambayo ni ndogo sana kuondolewa kwa njia hii. Kuna
aina mbili ya kufanya kipimo hiki;
(a) Kukata nyama
kutoka katika shingo ya kizazi kwa kutumia nyaya ya umeme inayojulikana
kitaalamu kama loop electrosurgical excision procedure (LEEP).
(b) Kukata nyama ya
shingo ya kizazi kwa kutumia visu maalum vya upasuaji au laser.
·
PET
Scan – Kipimo hiki
pia huweza kuthibitisha uwepo wa saratani na kuangalia maendeleo ya mgonjwa
baada ya kupata tiba.
·
Blood
test – Vipimo vya
damu, kuangalia wingi wa damu, kwa sababu wagonjwa wengi wanakuwa na upungufu
wa damu kutokana na kuvuja damu mara kwa mara.
·
Picha
ya kifua ya X-ray – Kuangalia kama
saratani imesambaa kwenye mapafu au la.
·
CT
Scan – Kuangalia
kibofu cha mkojo kama kimeathirika au la, na pia kuangalia kama saratani
imesambaa kwenye mifupa, ini, figo na sehemu nyingine za mwili.
Makundi ya saratani ya shingo
ya kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi imegawanywa katika makundi mbali mbali kulingana na TNM ama FGO (Classification) kama ifuatavyo;
Saratani ya shingo ya kizazi imegawanywa katika makundi mbali mbali kulingana na TNM ama FGO (Classification) kama ifuatavyo;
·
Stage
0 – Saratani iliyo
kwenye chembechembe au seli za aina ya epithelium lakini haifiki kwenye nyama
za ndani za shingo ya kizazi.
·
Stage
I – Saratani
iliyopo kwenye shingo ya kizazi.
·
Stage
II – Saratani
iliyosambaa hadi kwenye tupu ya mwanamke sehemu ya juu kwa 2/3.
·
Stage
III – Saratani
iliyosambaa hadi kwenye ukuta wa nyonga na sehemu ya chini ya uke kwa 1/3. Hii
inaleta madhara katika figo.
·
Stage
IV – Saratani
iliyosambaa hadi nje ya tupu ya mwanamke na pia husambaa hadi kwenye sehemu
nyingine za mwili kama mapafu, figo, mifupa nk.
Tiba ya saratani ya shingo ya
kizazi
Tiba ya saratani hii inategemea na kundi na aina ya saratani mgonjwa aliyonayo. Tiba ni kama ifuatavyo;
Tiba ya saratani hii inategemea na kundi na aina ya saratani mgonjwa aliyonayo. Tiba ni kama ifuatavyo;
·
Tiba
ya kuchoma (cauterization) –
Tiba hii hutolewa kwa wagonjwa wenye matatizo ya shingo ya kizazi kabla
hayajakuwa saratani na hutumia joto kali , umeme, na kemikali kuchoma sehemu
iliyoathirika.
·
Tiba
ya dawa (Chemotherapy) –
Tiba kwa kutumia dawa za saratani ambazo huuwa chembechembe au seli za saratani
ya shingo ya kizazi. Dawa hizi hutolewa kwa mgonjwa ambae saratani imeshasambaa
mwilini na inahusisha dawa moja pekee au mchanganyiko wa dawa zaidi ya moja
ambazo mgonjwa hupewa kwa njia ya dripu au humeza kupitia mdomoni. Dawa hizi
hutumiwa zaidi ya mzunguko mmoja na ni za gharama. Dawa hizi zinaweza kutumiwa
ili;
(i) Kutibu saratani
(ii) Kuzuia saratani isisambae sehemu nyingine mwilini
(iii) Kupunguza kasi ya ukuaji wa saratani
(iv) Kupunguza madhara ya saratani
(ii) Kuzuia saratani isisambae sehemu nyingine mwilini
(iii) Kupunguza kasi ya ukuaji wa saratani
(iv) Kupunguza madhara ya saratani
Madhara ya dawa hizi
yanatofautiana kulingana na aina ya dawa, muda wa utumiaji, na kiwango cha dawa
yenyewe. Madhara yake ni kichefuchefu, uchovu, nywele kunyofyoka (hair loss)
nk.
·
Tiba
ya mionzi (radiation therapy) – Tiba ya mionzi kwa kutumia mionzi ya X-ray, gamma na
neutrons ambayo huua seli za saratani hii. Mionzi hii haina maumivu na madhara
yake ni uchovu, tupu kuwa nyembamba sana (narrowing of vagina) na mgonjwa
kupungukiwa na damu.
·
Tiba
ya upasuaji (surgical treatment) – Aina za upasuaji kwa mgonjwa wa saratani ya shingo ya
kizazi ni kama zifuatazo;
·
Cryosurgery – Mpira maalum (probe) huingiziwa
kupitia kwenye tupu hadi kwenye shingo ya kizazi na majimaji ya nitrogen
hupitishwa yaliyo na baridi ya -160 0 celsius yenye uwezo wa kugandisha na
kuharibu seli za shingo ya kizazi hivyo kuzuia saratani.
·
Laser
surgery – Aina hii ya
upasuaji inatumia mionzi ya laser ambayo huchoma seli za shingo ya kizazi
ambazo haziko kwenye hali ya kawaida, mionzi hii haiharibu tishu za pembeni na
hutumiwa kwa matatizo ya shingo ya kizazi kabla hayajakuwa saratani.
·
Cone
biopsy – Kama
nilivyoeleza kwenye vipimo hapo juu.
·
Simple
hysterectomy – Hii inahusisha
kuondoa mfuko wa kizazi (uterus) kupitia sehemu ya tumboni au kupitia kwenye
tupu ya mwanamke kwa wagonjwa wa kundi I (Stage I). Madhara yake ni ugumba,
kuvuja damu, kupata madhara sehemu ya haja ndogo au utumbo na maambukizi kwenye
kidonda.
·
Radical
hysterectomy – Hii inahusiha
kuondoa mfuko wa uzazi kupitia kwenye tumbo pamoja na tishu za mfuko wa uzazi,
sehemu ya juu ya tupu ya mwanamke, na tezi za kwenye nyonga. Mayai (ovaries) na
mirija ya uzazi yanabakizwa. Madhara yake ni kama ya hapo juu pamoja na kuleta karaha
na maumivu wakati wa kujamiana.
·
Pelvic
exenteration – Huhusisha
uondoaji wa kibofu cha mkojo, uke, puru (rectum) na sehemu ya utumbo mpana
(colon). Upasuaji huu hutumiwa kwa wagonjwa wenye na saratani iliyojirudia.
kwa upande wa clinic ya lupimo ni tofauti kutokana na kwamba sisi ukitufikia hatutakupa dawa ya vidonge, bali tutakupima kwanza katika vipimo vyetu vinavyotembea mwili mzima na kubaini tatizo lako limekuathiri kwa kiasi gani na tutakupa dawa ya kumaliza tatizo hilo ambapo sisi tunatibu kwa kutumia mimea na matunda, tufikie katika vituo vyetu vifuatavyo
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA
IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU
NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA
MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA
C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI
MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU
KALFONIA,
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba
0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni