IJUE KAROTI NA FAIDA ZAKE
Habari
za maisha wadau wenzangu! Naomba leo niwape japo kidogo kuhusu matumizi
ya zao la karoti pamoja na faida zinazopatikana kutokana na utumiaji wa
zao hilo, ambalo kimsingi mizizi yake ndiyo hasa zao lenyewe. kumbuka kuwa karoti inalimwa karibu kila pembe ya
dunia hii. Zao hili linatofautiana katika rangi, kwani kuna karoti
nyeusi, zenye rangi ya pinki, nyekundu na njano. Karoti yenye rangi
nyekundu na njano ndiyo hasa tunayolima hapa TZ. Karoti za rangi
nyekundu na njano ndizo zinasemekana kuwa na virutubisho vingi sana
kuliko karoti nyingine.
Karoti
ina protini kidogo na haina mafuta, Pia ina asili ya wanga, na ni chanzo kizuri cha vitamini B, C
na E. Aidha ina madini mengi ikiwemo madini ya chuma. Kuna kitu kinaitwa
beta-carotene ambayo imo ndani ya
karoti na hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamini A. Vile
vile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa
kukinga kuta za utumbo.
Karoti
ikitumiwa vizuri na tena mara kwa mara inasaidia kukinga na kuponya
magonjwa yafuatayo: macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu,
ngozi, kupunguza tindikali inayodhuru tumboni na kukinga magonjwa yenye
asili ya kansa.
Karoti
inaweza kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile, ikiwa mbichi kwa
kutafuna, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga zingine, inaweza
kusagwa na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi
zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye salad ya matunda au
mbogamboga. Machicha ya karoti iliyosagwa yanaweza kutumika kama dawa
kukinga ama kuponya maradhi ya nje ya mwili.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana
nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni