Jumanne, 1 Machi 2016

Maboga yanaweza kuzuia magonjwa yanayotokana na  Fungus


Kwa muda mrefu maboga yamekuwa yanajulikana kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutumika kama dawa, vilevile chakula hicho kina protini yenye nguvu ambayo inaweza kupambana na magonjwa mbalimbali yanayotokana na fungus.
 

Maboga yamekuwa yakitumika sana katika tiba za kiasili katika kutibu magonjwa tofauti kama vile kisukari, shinikizo la damu, kiasi kikubwa cha mafuta mwilini pamoja na saratani 

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Vyakula, imeonyeshwa kuwa protini inayotokana na boga iitwayo Pr-2, inapambana vilivyo na ugonjwa unaosababishwa kuvu au fungus wa sehemu za uke (Vaginal yeast infection). 

Vilevile michubuko inavyotokana na mkojo au nepi (diaper rashes) pamoja na matatizo mengine ya kiafya. Protini hiyo ya Pr-2 iliyoko kwenye maboga halikadhalika inazuia aina 10 za fungus au kuvu ikiwemo aina hatari ya fungus wajulikanao kama Candida Albicans. Fungus hao ni maarufu kwa kusababisha matatizo kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari na kupelekea kupata fungus midomoni, katika ngozi, chini ya kucha pamoja na katika mfumo mzima wa mwili.
 

Waaalamu wana matumaini kuwa, protini hiyo inayopatikana kwenye maboga inaweza kupelekea mafanikio ya kutengezezwa tiba asilia ya kupambana na magonjwa ya  fungus.
… Haya kama ulikuwa unadharau kula maboga, nafikiri inakubidi ufikirie tena! 


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni