Jumanne, 23 Februari 2016



Mimea, matunda mengi ni tiba



MATUMIZI ya mimea ya asili katika kutibu maradhi mbalimbali, wakati mwingine huwa ni muhimu hasa pale jamii inaposhindwa kununua dawa za viwandani kutokana na bei.

Dawa za viwandani pia zinaelezwa na wataalamu kwamba zina madhara ya baadaye kwa binadamu hasa zinapotumika kwa muda mrefu. Mimea inapata pia umuhimu wa kutumika kama tiba kutokana na maelezo ya wataalamu kwamba ulaji wa vyakula vilivyosindikwa, vingi vikiwa vimechanganywa na kemikali kwa ajili ya utunzaji wake hutupa pia madhara yanayokuja baada ya muda mrefu.

Utumiaji wa mimea katika tiba umethibitishwa na unaendelea kuthibitishwa na wataalamu wengi duniani. Vinavyochukuliwa katika mimea kwa ajili ya tiba ni maua, majani, magome ya miti, mizizi na matunda. Kuna wakati, kutibu maradhi mbalimbali kwa kutumia mimea, ilichukuliwa na baadhi ya watu kama  upagani, lakini ukweli unabaki palepale kwamba hata dawa za viwandani ni matokeo ya mimea

Mimea na matunda kama vitunguu swaumu, mdalasini, vitunguu maji, parachichi, tangawizi, papai, mshubiri (aloe vera), matango, matikiti na kadhalika yamegundulika kwamba hutibu magonjwa mengi yanayomkabili mwanadamu kama atadumu katika kuyatumia katika kiwango kinachotakiwa. Mimea hiyo sasa inathibitishwa na wataalamu kwamba inatibu  magonjwa kama saratani, kisukari, kuhara, na  kupooza.

Kutokana na umuhimu wa kutumia mimea katika kutibu magonjwa mbalimbali, wataalamu wa tiba wamekuwa wakiwashauri wananchi kujaribu kupunguza tabia hatarishi katika kula vyakula vyenye mafuta mengi, vilivyokaangwa na vyakula vilivyosindikwa viwandani. Ushauri pia umekuwa ukitolewa kwa wananchi kuacha kunywa pombe na badala yake wajikite katika kujali afya zao kwa kula vyakula vya asili na kufanya mazoezi ili kuboresha afya zao.

kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni