Jumatano, 16 Machi 2016

FAHAMU UMUHIMU WA KULA KOROSHO KWA AFYA YAKO

Habari za wakati huu mdau wangu wa www.lupimoclinic.blogspot.com sina shaka unaendelea vyema, karibu leo tuzifahamu zaidi  kuhusu faida za korosho.

Korosho ni moja ya zao la biashara ambalo hupatikana sana Kusini mwa Tanzania, Mtwara, licha ya kwamba zao hili linafahamika sana kama zao la biashara, lakini bado zao hili lina faida kwa afya zetu pia.

Napenda kuchukua muda wako kwa sasa ili niweze kukuelekeza baadhi ya faidi za matumizi ya korosho kama ifuatavyo:

Matumizi ya korosho yanasifika sana kwa kuwa na uwezo wa kulinda afya ya moyo kutokana na kwamba korosha ndani yake inakirutubisho kiitwacho 'antioxidants'
Aidha korosho pia inasifika kwa kuwa na madini ya 'magnesium' ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa na meno, lakini pia humsaidia mhusika anayependelea kutumia korosho kuwa na nafasi ndogo ya kupatwa na matatizo ya shinikizo la damu, hususani shinikizo la juu la damu.

Pia ulaji wa korosho husaidia sana kuimarisha afya ya usingizi na kumfanya mhusika kuacha kupata usingizi wa mang'amng'am na badala yake atajikuta akipata usingizi mzuri kabisa.

Mara nyingi kinamama wanaoingia kwenye kufungu hedhi 'menopause' wao huzongwa sana na tatizo la kukosa usingizi, hivyo wanashauriwa kutumia korosho ili kuepuka tatizo hilo.




kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni