HIZI NDIZO FAIDA ZA MACHUNGWA KATIKA MWILI WAKO
Chungwa ni tunda linalostawi ulimwenguni kote , lakini haswa tunda hili lilianza
kusini mwa bara la Asia, huku likilimwa sana huko nchini China.
Mtaalam wa tiba asili kutoka lupimo sanitarium clinic tabibu john lupimo anasema kuwa kwa wale wanaosumbuliwa na mafua
wanaweza kuongeza maji ya moto katika juisi ya chungwa kisha mhusika anywe.
Mtaalam huyo, anaeleza kuwa majani ya mchungwa
yakipondwa na kisha kuchanganywa na maji ya moto pamoja na asali kidogo, kwa
ujumla mchanganyiko huo hutumika kama dawa ya kikohozi.
Endapo maua makavu yakisagwa nakuchanganywa katika maji ya moto ni dawa ya shinikizo la mishipa ya fahamu. Huku maganda yake yakisuguliwa usoni huwa ni dawa ya chunusi.
Pamoja na hayo,tabibu john lupimo anabainisha kuwa kwa
ujumla juisi ya machungwa husaidia ugonjwa wa pumu, matatizo ya kifua,
kusafisha damu, kupooza, kuungua, matatizo ya meno pamoja na beriberi.
Mbali na magonjwa hayo, pia husaidia matatizo ya
kizazi, mishipa ya damu, magonjwa ya ngozi, matatizo ya mirija ya uzazi,
husaidia usagaji wa chakula mwilini pamoja na kutuliza kichefuchefu kwa
wajawazito.
Hizo ndizo baadhi ya dondoo muhumu za faida za machungwa kwa afya ya mwili wako.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana
nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania, www.lupimoclinic.blogspot.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni