AFYA NI KILE UNACHOKULA, HIZI NI FAIDA ZA NDIZI
Ndizi
ni tunda linalotumika sana kama mlo sehemu mbalimbali duniani. Ni tunda
ambalo ni tamu na lenye virutubisho mbalimbali na muhimu kwa mwili.
VIRUTUBISHO VILIVYOMO KWENYE NDIZI:
Ndizi
ya wastani ina uzito wa kama gramu 1260. Ina nishati kiasi cha kalori
110, gramu 30 za wanga na gramu 1 ya protini. Ndizi hazina fati, lehemu
(cholesterol) au madini ya Sodiamu.
FAIDA ZA NDIZI KIAFYA:
Kushusha Shinikizo la Damu
Ndizi
zina madini ya Potasiamu kwa wingi ambayo husaidia kulegeza mishipa ya
damu na hivyo kupunguza shinikizo la damu au presha (blood pressure).
Pia ulaji wa madini ya potasiamu kwa wingi hupunguza hatari ya kufa
kutokana na magonjwa mbalimbali.
Kupunguza Hatari ya Kupata Saratani
Ndizi
ni chanzo kizuri cha vitamini C ambayo husaidia kuondoa sumu kwenye
mwili ambazo husababisha saratani kutokea. Pia kambakamba (fibers)
zinazopatikana kwenye ndizi kwa wingi husaidia kuondoa sumu kwenye
utumbo zinazoweza kuchangia saratani ya utumbo.
Ufanyaji Kazi wa Moyo
Madini
ya Potasiamu, vitamini C na B ambayo hupatikana kwa wingi kwenye ndizi
huwezesha moyo kufanya kazi vizuri. Ulaji wa vyakula vyenye Potasiamu
kwa wingi na Sodiamu kidogo kama ndizi hupunguza hatari ya magonjwa kama
shambulio la moyo, kiharusi na shinikizo la damu la kupanda.
Kutibu Kuharisha
Kuharisha hupoteza madini mengi hasa ya Potasiamu. Ulaji wa ndizi utakusaidia kurudisha madini haya mwilini mwako.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana
nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni