ZIFAHAMU SABABU KUU ZA WANAWAKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA NA MATIBABU YAKE…
kama unaswali juu ya makala hii tupigie simu sasa kwa namba 0742120577 au 0672666601.
Utafiti unaonyesha asilimia thelathini ya wanawake wenye
umri wa kufanya mapenzi yaani kuanzia miaka 18 mpaka 59 wana tatizo la kuishiwa hamu
ya kufanya tendo la ndoa na hili ndio tatizo lao kuu inapokuja wenye afya ya tendo la ndoa kitaalamu
kama sexual health, hii ni moja ya sababu inayowafanya wanaume wengi wakimblie
nje kulala na wanawake wengine kwani wawanawake zao kila siku hutafuta
sababu ya kutofanya tendo la ndoa.
Lakini tatizo hili ni tofauti kidogo kwa upande wa wanaume
kwani ni vigumu sana mwanaume kukataa kufanya tendo la ndoa na pia
wanaume wanaweza kupata hamu kwa kutumia
vidonge tu vya aina Fulani ambavyo pia vianaweza kumletea madhara makubwa, lakini wanawake inahitaji mchanganyiko wa njia
mbalimbali ili kuweza kutatua tatizo lao yaani njia za ushauri wa kitaalamu na
dawa pia wakati mwingine.
Zifautazo ni sababu
za kuishiwa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake…
Matatizo ya kisaikolojia;
linapokuja swala la tendo la ndoa amani ya moyo na uhuru wa kiakili
unachangia sana mtu kupata hamu hata kufika kileleni lakini hali huu huweza kua
na vikwazo kama historia ya kulazimishwa
kingono au kubakwa hapo kipindi cha nyuma, mawazo mengi hasa ya kazi, matatizo
ya kifedha,kutojiamini na kuhisi labda maumbile yake mwanamke hayavutii, magonjwa
ya akili na mgandamizo wa mawazo, mtizamo hasi kuhusu ngono kwamba anahisi ni
unyanyasaji wa kijinsia na kadhalika.
Matatizo ya kimahusiano; sio rahisi kwa mwanamke kufanya
mapenzi kwa mtu ambaye hana hisia naye hata kidogo japokua
wanaume wanaweza kufanya ngono na mtu yeyote hivyo shida yeyote ambayo inaharibu hisia za mwanamke kwa
mwanaume wake humfanya kose hamu kabisa ya kufanya ngono, mfano mawasiliano
mabovu kati ya wapenzi, ugomvi kati ya wapenzi ambao haujapata suluhisho, kutoaminiana
kati ya wapenzi na kuisha kabisa kwa hisia za mapenzi ambazo mwanzoni
zilikuepo, ndoa ya muda mrefu sana pia huchosha kabisa linapokuja swala la
tendo la ndoa.
Matatizo wakati wa tendo la ndoa; kama mwanamke anasikia maumivu
makali kipindi cha kufanya ngono tendo la ndoa hataweza kusikia hamu kabisa.
Magonjwa; magonjwa mengi huchangia kuishiwa hamu ya kufanya
tendo la ndoa mfano magonjwa yote yanayosababisha maumivu mfano maumivu makali
ya joint, maumivu makali ya kifua, maumivu ya tumbo pia magonjwa ya mishipa ya
fahamu, kisukari, ugonjwa wa presha na kadhalika
.
Uchovu: kufanya kazi nyingi na kurudi nyumbani usiku ukiwa
umechoka, kazi ya kuwahudumia watoto kama kufua, vyombo, kupika na kadhalika
huleta uchovu mwingi ambao hupoteza kabisa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Upasuaji; upasuaji wowote unaohusu matiti ya mwanamke au sehemu zake za siri unaweza kuathiri
kabisa uwezo wake wa kushiriki tendo la ndoa.
Tabia na maisha kwa ujumla; unywaji wa pombe uliopitiliza na
uvutaji wa sigara huathiri uwezo na hamu ya kushiriki tendo la ndoa japokua
unywaji wa wine kidogo kama glass moja huleta hamu ya kushiriki kingono.
mazoea ya kushiriki aina zingine za ngono; kuna aina zingine za ngono ambazo si za kawaida mwanamke
akishazoea inakua ngumu sana kuacha hata akiolewa inakua vigumu kushiriki ngono
za kawaida mfano mazoea ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, kufanya ngono
na wanawake wenzake, kufanya ngono na mtu zaidi ya mmoja mfano threesome au
foursome.
Ujauzito na kunyonyesha: hua kuna mabadiliko makubwa ya
viwango vya homoni pale mwanamke anapobeba mimba na wakati wa kunyonyesha hii
hupunguza hamu ya kufanya ngono kwa kiasi kikubwa sana.
Umri: kadri umri unavyozidi kwenda hamu ya kufanya ngono
inazidi kupungua kwa wanawake na mwanamke anapofika miaka hamsini kitaalamu
tunaita menopause homoni inayoitwa oestrogen hupungua sana na kumfanya awe na
uke mkavu ambao hua na maumivu kipindi cha kushiriki ngono.
MATIBABU
Ushauri;Kama nilivyosema mwanzoni kuishiwa hamu ya tendo la ndoa
kwa wanawake huletwa na sababu nyingi na matibabu yake hutegemea sana
chanzo cha tatizo
husika yaani chanzo kikitatuliwa mtu ataweza kurudi katika hali yake ya
kawaida. Mfano wanawake wenye matatizo ya kisaikolojia wanatakiwa
wamuone
mshauri aweze kuwasaidia kulingana na matatizo yao na kama kuna shida ya
mahusiano kutafuta ufumbuzi wake.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni