Jumamosi, 8 Oktoba 2016

                      Kutokwa na Uchafu Ukeni


Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’.
Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.
Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni:
• Kuwa na wapenzi wengi
• Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
• Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali
• Uchafu
• Uvutaji sigara
• Pombe
• Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni
Dalili:
• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
• Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza
• Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke
• Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu
• Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa
• Maumivu makali chini ya kitovu
• Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu
Matibabu
Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.

NB: lakini pia unaweza kutufikia lupimo sanitarium clinic tukakutibu tatizo hilo vizuri kabisa na lisijirudie nipigie simu sasa hivi nikuelekeze tulipo namba yangu ni 0759324414 karibu sana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni