Jumatatu, 17 Novemba 2014

YANAYOHUSU UGONJWA WA KIFAFA

Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.
Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.
Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.
Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.
Lakini Lupimo sanitarium clinic tunatibu ugonjwa wa kifafa kwa uhakika na unapona kabisaaaaa
Wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 nawww.twitter.com/lupimoclinic pamoja na www.hulkshare.com /lupimoclinic
MUNGU AWABARIKI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni