Jumanne, 14 Aprili 2015

HOMA YA INI NI HATARI TAMBUA DALILI ZAKE

HEPATITIS B NI NINI?
Hepatitis B ni virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Homa ya Ini.
Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye KIFO.
Inakadiriwa watu milioni 350 duniani wameathirika na ugonjwa huu ambapo watu 620,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa huu.

Virusi vya Hepatitis baada ya kulishambulia ini.

HOMA YA INI INASABABISHWA NA NINI?
Ugonjwa huu husababishwa na virusi waitwao Hepatitis B (HBV) ambao hukaa katika ini, damu na baadhi ya majimaji mwilini.

UNAAMBUKIZWAJE?
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia zifuatazo:
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi 'denda'
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki


NB: Ugonjwa huu hauambukizwi kupitia chakula, maji au kushikana mikono na waathirika.

DALILI ZAKE
Dalili za ugonjwa huu huchukua muda mrefu kuonekana, zikionekana mgonjwa anakuwa tayari ameathirika sana na ni kama ifuatavyo:

-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili kuwa dhaifu
-Homa kali
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupungua uzito
-Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
-Macho na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo mweusi

KINGA
-Chanjo
-Kutumia kinga wakati wa kujamiana
-Kuacha kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kutochangia miswaki
-Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
-Kutochangia damu isiyo salama


Kama una swali,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu 

namba 0769368546,0719097574 na 0754301115

pia 
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni