Jumatatu, 21 Desemba 2015

              Kuumwa na Macho - Conjuctivitis

TABIBU JOHN LUPIMO WA LUPIMO SANITARIUM CLINIC
 Tuungane na tabibu john lupimo katika makala hii ya ugonjwa wa macho, Ugonjwa wa macho hutokea wakati ambapo utando ufunikao macho hubadilika na kuwa na rangi nyekundu na kuwasha. Hali hii huenda ikaathiri jicho au macho. Chanzo chake huwa ni mzio (allergy) unaosababishwa na kemi kali. Tatizo hili pia husababishwa na maambukizo. Haya yanaweza kutokea mtu anaposhika macho yake kisha akashika taulo, kitambaa cha meza 
Dalili za ugonjwa huu:
  • Macho mekundu au waridi
  • Macho kuwasha kana kwamba kuna uchafu
  • Uchungu wa macho 
Ni vyema kumuona daktari ikiwa mtoto wako ana ishara hizi. Daktari atatibu maambukizo ya bakteria kwa kutumia kiua bacteria. Ikiwa tatizo hili linatokana na athari nyingine, daktari atakupa dawa ya kumeza au kuweka machoni. Pia unaweza kutumia kitambaa vuguvugu kwa kuweka kwa macho ya mtoto wako ili kupoesha uchungu.
 
Mwite daktari ikiwa mtoto wako:
  • Ana macho mekundu hali isiyo ya kawaida
  • Macho yaliyofura
  • Usaha kutoka machoni
  • Kuwa na ugumu wa kufungua macho wakati anapoamka.
  • Analalamika kuwa haoni
Kumbuka kumwita daktari wa mtoto wako ikiwa sehemu ya chini ya jicho imefura, au hamna tofauti yoyote siku 2-3 baada ya matibabu ama baada ya juma.
 
pia sisi lupimo sanitarium clinic tunatibu tatizo hili la macho kwa hiyo kama unasumbuliwa na macho au mtoto wako ana tatizo hilo tufikie haraka sana lupimo katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni