Jumapili, 20 Desemba 2015

LISHE BORA KWA MTOTO WA MWA KA 1-4


Lishe mbaya kwa watoto husababiswa na ukosefu wa Elim na ufaham mzuri wa  vyakula  na lishe bora  wa wazazi,lakini kwa upande mwingine hali ya wazazi kutokujali watoto wao kwa sababu moja au nyingine pia huchangia tatizo hili.Mtoto kukosa  usingizi wakutosha au kushindwa kulala vizuri pia huchangiwa sana na njaa,mtoto asiposhiba vizuri hawezi kulala vizuri.Kelele,kumchelewesha mtoto kulala na kukosa ratiba ya mtoto kulala pia huchangia mtoto kukosa usingizi wakutosha.

Watoto wa mwaka mmoja adi mine(1-4)wanaitaji masaa 14 ya usingizi kila siku.wanatakiwa kupata usingizi wa mchana wa kati ya saa moja adi masaa matatu na nusu(1-3.5),usiku wanatakiwa kulala kati ya saa moja na saa tatu(1-3) na asubui  waamke kati ya saa kumi na mbili na saa mbili (12-2) Ni kosa kabisa mtoto kua macho baada ya saa tatu,endapo mtoto wako huwa macho baada ya saa tatu ni kiashirio kwamba anashida au tatizo Fulani.


Asilimia kubwa sana ya watoto hawapati mboga na matunda yakutosha katika lishe zao.Watoto wenye ukosefu wa  vitamin muhim,madini mwili,na aside mafuta za muhim (essential fatty acids) huwa na akili zilizozubaa na hawafanyi vizuri darasani na wana asili ya ukali,watoto wengine huwa na unene wa ziada ambao pia husababishwa na lishe mbaya,Lakini kubwa kabisa mtoto huyo hawezi kukua katika uwiano ulio sahihi.


Watoto wanapofikia umri wa kuanza kwenda madarasa ya awali ndio ule wakati ambao mtoto hurefuka na mwili wake huwa na nguvu nyingi,huu ndio wakati ambao wanaanza kujifunza kujitegemea na kutengeneza wasifu binafsi(personalities).Mtoto huanza kubagua chakula,na kuamua anapenda au apendi chakula kipi.


Watoto wanaobagua chakula huwa kwenye hatari kubwa ya kukosa virutubisho maalum vinavyoitajika kuwezesha ukuaji wao,kwani virutubisho hivyo huchangia ukuaji bora wa akili,mwili,na hata hisia.

Ukuaji sahihi wa mifupa na meno kwa watoto umekua ni changamoto kubwa  sana,kwani asilimia kubwa ya watoto hawapati vitamini muhim,madini mwili na asidi mafuta ya kutosha kuwezesha ukuaji wao.


Nini maana ya  Lishe Bora(balanced diet)?ni lishe yenye virutubisho vyote kwa kiasi sahihi na uwiano sahihi ili kuwezesha afya bora.Virutubisho vyote sita lazima viwepo: wanga,protini, mafuta ,vitamin, madini mwili na
maji.kwa ujumla hii ndio maana ya lishe bora,lakini kitaalam zaidi,wataalam wa afya husema lishe bora hutofautiana kati ya makundi mbalimbali ya binadam kutoka na uhitaji wa miili yao katika kipindi

Fulani,wakimaanisha inayoweza kua lishe bora kwa mtoto mchanga haiwezi kua lishe bora kwa mtoto wa miaka kumi na mbili kwani miili yao inauhitaji tofauti,au kilicho lishe bora kwa mama mjamzito hakiwezi kua lishe bora kwa mgonjwa wa Moyo kwani wao pia miili yao inauhitaji wa tofauti.

Kwa mantiki hiyo basi ili lishe ya mtoto wa mwaka mmoja adi miaka  minne iitwe lishe bora,ni lazima iwe na virutubisho vifuatavyo

  • Wanga:ugali,wali,viazi,mkate
  • Mboga za majani na matunda kwa wingi-lenga kumpa mara tano kwa siku
  • Protini:nyama,samaki,mayai,maharagenjegere(angalao  ale samaki mara mbili kwa wiki)
  • Vyakula vyenye asili ya maziwa:maziwa,yoghurt,cheese (lazima ale kila siku)
  • Mafuta.sio mafuta ya wanyama  bali mafuta yatokanayo na mimea(saturated fats)
Baada ya kujua lishe bora ya mtoto,tuangalie umuhim na kazi za Virutubisho tulivyoainisha hapo juu.

Vitamini C

Mwili wa binadm hauwezi kujitengenezea vitamin C,hivyo ni lazima ipatikane katika lishe.Vitamini C huwezesha utendaji bora wa akili,huusika katika kuendesha hisia,pia huuwezesha mwili  kunyonya madini joto.kila siku mpe mtoto juisi ya machungwa au apple(isiwe kali)na apate Nyama au samaki.Vitamini C hupatikana kwenye machungwa,mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo na Apples.

Vitamini A

Vitamin A hutengeneza Meno na Ngozi yenye afya nzuri na kufanya mtoto aone vizuri.inapatikana kwenye mayai,nyama,maziwa,cheese,karoti na mboga  za majani zenye rangi ya kijani mkoozo.


Vitamin D

Vitamini D huwezesha mwili kunyonya calcium,bila calcium mifupa haiwezi kukua katika uwiano sahihi wala kuwa na nguvu hivyo mtoto anaweza kupata matege na kua na mifupa dhaifu.Vitamini D nyingi hutoka kwenye mwanga wa jua,si lazima liwe jua kali.Ingawa vitamin D inapatikana pia kwenye Mayai na samaki wenye mafuta  ni vyema kuhakikisha mtoto anatoka nje kucheza kila siku ilia pate vitamin D ya kutosha.

Madini  Chuma(iron)

Madini chuma hutengeneza seli za damu,hasa seli nyekundu ambazo hutumika kusafirisha oxygen katika mwili wa mtoto:bila oxygen yakutosha mtoto hawezi kucheza,kama mtoto wako anachoka wakati wote kuna uwezekano mkubwa wa kua na upungufu wa madini joto.Madini joto hupatikana kwenye nyama,samaki,mbegu za maboga,brown bread,maharage na mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo.


Folate (asili yake familia ya vitamin B)

Huusika sana katika utengenezaji wa seli mpya,hutengeneza DNA,ni ya muhim sana katika ukuaji wa vichanga na watoto wadogo.Folate inapatikana katika mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo,maharage,karanga ,korosho,hata ivyo spinachi ndio chanzo kikubwa kabisa cha folate.

Asidi mafuta Muhim(Essential Fatty Acids-EFA’s)

Mwili hauwezi jitengenezea kirutubisho hiki,ni lazima kipatikane kwenye lishe,kuna familia mbili za EFA’s-Omega 3 na omega 6_ambazo zinaitajika kuwezesha utendaji mzuri wa ubongo,utendaji bora wa kinga za mwili,na kuwezesha  afya akili kwa ujumla.hupatikana kwenye oily fish,na flax oil.Kama mtoto wako anashindwa kutulia darasani,anashindwa kukumbuka vitu,analala kwa shida au hapati usingizi vizuri  basi kuna uwezekano mkubwa wa mtoto huyo kua na upungufu wa Omegas.Nashauri matumizi ya Suppliments(dawa zinazobeba virutubisho) kwani  vyanzo vya omegas ni vichache.

Calcium

Madini ya calcium ni kwa ajili ya utengenezaji wa mifupa na meno na pia inaendesha mfumo wa mapigo ya moyo na inasaidia damu kuganda kwa haraka.Bila vitamin D,mwili hauwezi nyonya calcium.calcium inapatikana kwenye mboga za majani zenye rangi ya kijani venye asili ya mbegu na katika maji(hard water)

Fibre(Nyuzi nyuzi)

Fibre ni muhim sana katika usagaji wa chakula mwilini.watoto wengi hupata shida kupata aja kubwa (constipation )kwa ajili ya ukosefu wa fibre katika lishe zao.ili kuepuka tatizo hili,hakikisha mtoto anapata fibre ya kutosha katika lishe yake.Matunda,mboga za majani,unga usiokobolewa na karanga ni vyanzo vizuri vya Fiber
.

Maji

Mtoto anatakiwa kunywa maji mengi,ili kuzuia constipation na kuepuka kuishiwa maji mwilini,apate kati ya glasi 6 adi 8 kwa siku.

Kwa ujumla matunda na mboga za majani na matunda ni vyakula muhim sana kwa afya na ukuaji bora wa
mtoto.Fanya matunda na mboga za majani sehem kubwa ya mlo wake.badala ya kumpa mtoto biskuti na soda anapotaka kitu cha kula kula,mpe matunda,au juice au smoothie au supu ya mboga.kwa kufanya hivyo unamuweka mtoto wako salama.

Kwa kumalizia niwaseme wale wakinadada na kinamama wanajiita wa dot com, wanaodhani kumlisha mtoto chipsi na kuku,soseji,tambi,na vyakula vya makopo ndio
uzungu.laaa!mnatia aibu.pika chakula kizuri na fresh nyumbani umpe mtoto,zingatia virutubisho ambavyo mtoto anaitaji.Pia niseme na wale kinadada na kinamama ambao wamekariri kua chakula cha mtoto ni uji,mtori,wali wa maziwa na maziwa.mtoto anapofikisha mwaka mmoja anakua katika uwezo wa kuanza kuonjeshwa vyakula vingine.Inashangaza pale unapomkuta mama bado anamsagia mtoto wa miaka mitatu chakula kama ndizi na viazi.Mpe mtoto chakula cha kawaida kabisa kama nyama,maharage,mayai,karanga,ugali,mboga za majani,ili mradi tu kiwe na virutubisho vyote mtoto anavyoitaji.

Ni hayo tu kwa leo,chukua atua mpe mtoto wako lishe bora. 


kwa maelezo zaidi kuhusu mtoto wako basi unaweza kutufikia lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini, huwa tunatoa semina ya magonjwa mbalimbali pamoja na jinsi gani ya kuwahudumia watoto wadogo,
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni