Ijumaa, 18 Desemba 2015

TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MWILINI




Harufu mbaya ni kitu kisichompendeza mtu yeyote. Unapotoa harufu mbaya toka mwilini mwako, haikupendezi wewe mwenyewe wala mtu wa jirani. Kama kitu hukipendi wewe na ukakiona hakifai basi usimlazimishe mwenzio akipende au akione cha kawaida.

Harufu mbaya mwilini inatoka maeneo yote ya mwili kuanzia kichwani hadi miguuni.

Zipo sababu nyingi zinazomfanya mtu atokwe na harufu mbaya, inaweza kuwa uchafu, maradhi au maumbile.


Hali ya uchafu ipo wazi endapo mtu haogi, hafui au hanawi. Uchafu wa kichwani inaweza kuwa nywele au wigi au

kitu chochote kinachowekwa kichwani.Uchafu unaweza kuwa maeneo mbalimbali ya mwili.

Maradhi ya ngozi, kansa au vidonda vyenye maambukizi vinaweza kusababisha kutoa harufu mbaya au vitambaa vilivyofungiwa vidonda.


Kwa hiyo kundi la maradhi ni pana kwa kuwa tatizo la ngozi pekee linaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa.

Sababu za kimaumbile linawahusu zaidi watu wanene ingawa hata wembamba pia wanaweza kupatwa na tatizo hili kutegemea na harufu inatoka eneo gani la mwili.


Watu wanene hupatwa na matatizo ya kutoa harufu mbaya kama hawatazidisha usafi na kuhakikisha miili yao sehemu za mikunjo inakuwa mikavu. Sehemu hizo ni chini ya kifua au matiti, nyama za tumboni, chini ya tumbo, mbavuni, sehemu za siri na mapajani.


Unene pamoja na matatizo mengi yanayoweza kujitokeza pia huweza kusababisha magonjwa ya ngozi na kutokwa na jasho lenye harufu kali.


MAENEO YANAYOTOA HARUFU MBAYA
Sehemu yoyote ya mwili inaweza kutoa harufu mbaya kama tulivyoona hapo mwanzoni kuanzia kichwani hadi miguuni. Lakini yapo maeneo kama masikioni na puani pia harufu mbaya hutoka. Harufu za maeneo hayo mara nyingi haziwi kali.

KUTOKWA HARUFU MBAYA KINYWANI

Tatizo la kutokwa na harufu mbaya mdomoni au kinywani hutokana na matatizo mbalimbali kama kuwa na meno mabovu, magonjwa ya fizi, ulimi, fangasi za kinywani na uchafu kutokana na kutosafisha kinywa vizuri.

Wapo watu ambao kwa asili hutoa harufu mbaya kinywani pasipo kuwa na magonjwa ya kinywa na huwa makini kusafisha kinywa, lakini harufu haiishi.

Tatizo hili hutibika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina katika tabaka linalotandika ndani ya kinywa.
Wakati mwingine harufu mbaya ya kinywa husababishwa na ulaji wa vyakula, unywaji pombe, uvutaji wa sigara, bangi na ugoro.


KUTOKWA NA HARUFU MBAYA KWAPANI

Kutokwa na harufu mbaya kwapani au kunuka kikwapa inatokana na mambo mbalimbali hata kama unajisafisha mara kwa mara na kutoa vinyweleo vya kwapani.


Harufu ya kikwapa husababishwa na njia ambazo ngozi ya kwapani hupumua zinaziba, hivyo kusababisha njia za kutolea jasho kuwa chache na jasho kutoka kidogo kidogo na kujaa kwapani.

Hivyo kujaa na kulowesha nguo sehemu hizo, hali hii ikiendelea kwa muda mrefu husababisha bakteria aina ya ‘staphylloccocus’ kuanza kuishi hapo na jasho linalojirundika kukauka na kuganda, hivyo kutoa harufu mbaya.


Tatizo la kikwapa likiendelea kwa muda mrefu baadhi ya njia za jasho huziba kabisa na bakteria kujipenyeza.

Hapo ndipo unaweza kusumbuliwa na majipu ya mara kwa mara kwapani, kutokwa na vipele vikubwa kwapani na muwasho mkali baada ya kunyoa kwapani na hata vidonda vidogovidogo.

Matumizi ya baadhi ya pafyumu husababisha mzio ambapo kwapa litawasha sana kila wakati au utatokwa na vipele vingi au ngozi ya kwapani inabadilika na kuwa nyeusi sana huku ikitoka harufu mbaya. Tatizo hili linaweza kutibika hospitali.


HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI
Harufu mbaya sehemu za siri inaweza kuwa kwa wanaume na wanawake. Zipo sababu mbalimbali kwa wanaume ambazo zinahitaji uchunguzi wa kina na tiba.


Kwa wanawake harufu inaweza kutoka ukeni ikiambatana na uchafu au la. Harufu ya ukeni huwa mbaya inayofanana na shombo la samaki hutokana na kutokuwa makini kiusafi.


Maambukizi ya fangasi na bakteria, magonjwa ya zinaa, kisonono na kaswende ni sababu mojawapo.
Wapo wanawake ambao hutokwa na harufu sehemu za siri kutokana na mikunjo ya kwenye mapaja yao, hasa kwa wale wanene. Harufu pia inaweza kutoka katika sehemu ya haja kubwa na hii ni ya kinyesi endapo hutanawa vizuri au kuwa na maradhi sehemu hiyo.


NINI CHA KUFANYA?

Endapo utakuwa na tatizo hili la kutoa harufu mbaya maeneo tofauti ya mwili au unahisi mwenzio ana tatizo hili na anakukwaza, inashauriwa uwaone madaktari katika hospitali za wilaya kwa uchunguzi wa kina au utufikie lupimo sanitarium clinic.

Tatizo hili linatibika na hupotea kabisa na kukuacha huru. Tatizo la kutokwa na majipu, vipele, kubadilika rangi ya ngozi kwapani, chini ya matiti na sehemu za siri, pia linatibika kabisa endapo utawaona wataalamu. Wahi mapema hospitali.

USHAURI :

Zifuatazo ni njia mbadala unazoweza kufanya kuweza kukabili tatizo.

Tumia sabuni zilizo na uwezo wa kupambana na bakteria (Anti bacteria soap). Baadhi ya sabuni hizo ni Dettol, Family, Protex au Dove.

Hakikisha unavaa nguo zilizotengenezwa kwa malighafi za pamba kipindi cha joto kwani zinasaidia kunyonya jasho linalotoka mwilini.

Badala ya kutumia kiondoa harufu (Deodorant), unaweza kufuta sehemu za mwili wako zinazotoa jasho kama kwapani kwa kutumia ‘white vinegar’ au ‘ apple cider vinegar’.

Kama tatizo linasababishwa na dawa unazotumia mwone daktari wako akupe njia mbadala ya kukabili tatizo au akubadilishie dawa.

Unaweza kuweka maji ya nyanya katika maji yako ya kuoga, kama unatumia sinki unaweza kukaa ndani ya maji yao kwa takribani dakika 15.

Paka poda ya watoto kwa ajili ya kukausha jasho kwenye shemu zenye mkonjo na kuondoa harufu mbaya mwilini.
Usirudia kuvaa nguo nguo za ndani wakati wa joto.

Nywele za kwapa zinapokuwa nyingi husababisha tatizo hilo, hivyo basi hakiksha unazinyoa mara kwa mara .
Ikumbukwe pia harufu hii huweza kusababishwa na soski chafu, wale wanaovaa soksi kwa muda mrefu na kuloa miguu, harufu hiyo ina uwezo mkubwa wa kusambaa mwili mzima . Ili Kuepuka tatizo ni vizuri kama utavaa soksi safi na usirudie kuzivaa na usafishe miguu yako vizuri. Ukiwa na Swali au Tatizo lako lolote la Siri usikose kuwasiliana nasi lupimo sanitariumu clinic au kutufikia katika vituo mbalimbali vilivyopo mikoani

 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni