Haya Siyo Maneno Mazuri Kwa Mjazito
Licha ya kuwa na
changamoto nyingi, ujauzito ni hatua yenye faraja kubwa sana wanawake wengi.
Kwani kila mmoja huwa na matumaini makubwa kwa kile alichokibeba tumboni.
Hakuna ubishi kuwa mama
anapokuwa katika hali hii hupenda kuishi maisha yasiyo na bughudha ama rabsha.
Pamoja na kuwa watu wengi hukubaliana na changamoto zinazowapata wanawake
katika kipindi hiki, kumekuwapo na makosa kadhaa wanayofanya wakati mwingine
bila kujua athari zake.
Makosa haya husababisha
wanawake hawa kujisikia vibaya au wakati mwingine kujenga chuki kwa mtu husika.
Najua hata wewe inawezekana umekuwa ukifanya makosa haya bila kujua kama ni
kero kwa mjamzito husika. Hivyo kama jibu ni ndiyo, si vibaya ukasoma hapa
chini kuona je ni mambo gani hutakiwi kumwambia mwanamke anapokuwa kwenye hali
hii ya ujauzito.
Wataalamu kutoka mtandao
wa parenting.com wameainisha baadhi ya mambo hayo kuwa ni:
1.
Hivi ulijipanga kupata mimba au imekuja tu?
Unategemea kupata jibu
gani kutokana na swali hili. Mara nyingi unapomuuliza mwanamke mwenye hali hii
humaanisha vitu vingi. Hivyo kwa mujibu wa wataalamu unachotakiwa kumwambia ni
‘hongera’.
2.
Hivi una hakika huna mapacha kweli?
Eeeh akiwa na mapacha we
unataka nini? Au we nani hadi uulize swali kama hilo. Kwa kulitazama tu
unadhani swali hilo linafurahisha?
Hata kama unamuona ana tumbo kubwa pengine
isivyo kawaida hutakikiwi kumwambia kitu kama hicho, hasa ikizingatiwa kila mtu
huwa na mapokeo yake.
3.
Utakuwa umebeba mtoto wa...
Hili ni kosa jingine
linalofanywa na watu wengi, bila kujua kama linamkera mwanamke mjamzito.
Inawezekana mtoto unayemtabiria siyo aliyekuwa kichwani kwake. Au wakati
mwingine anaweza akaona kama unamfanyia uchuro. Kama unahisi huna jambo la
kuongea naye, siyo vibaya ukampa nafasi ya kupumzika.
4.
Hivi huyo mtoto anacheza kweli?
Swali kama hili linaweza
kusababisha ugomvi mkubwa baina ya muulizaji na muuliza hasa inapotokea, mama
mjamzito akawa na mimba kubwa.
Kwani wengi huhisi kuwa,
mtoto wake aliyetumboni atakuwa anatabiriwa kifo, jambo ambalo siyo zuri
kulisikia hata masikioni.
Unataka kujua kama
anacheza ama hachezi kwani we ni daktari? Wakati mwingine ni vyema kupima
maneno yako kabla hayajatoka nje ya kinywa chako.
5.
Naweza kulishika tumbo lako?
Watu wengi hupenda kufanya
mambo kwa kuiga. Inawezekana umeona kwenye video watu wakifanya hivi. Lakini
unafahamu kuwa katika tamaduni nyingi mambo ya kushika tumbo la mjamzito
hukatazwa.
Kwani wakati mwingine kwa kulishika tu, inaaminika unaweza
kusababisha madhara katika afya yake. Hivyo inatosha kumsalimia na kumjulia
hali. Kama yeye hajambo basi ni wazi kuwa hata mtoto wake atakuwa anaendelea
vizuri.
6.
Hivi na wewe utaweza kunyonyesha kweli?
Swali kama hili linavunja
moyo. Unapobeba mimba, kimsingi unakuwa umejipanga. Kwani ni wazi kuwa unaelewa
fika kila hatua utakayopitia. Hata kama siyo kwa kuipitia basi hata kwa
kuisikia kutoka kwa watu wengine.
Hivyo siyo sawa kumuuliza
swali kama hili, kwani mwingine anaweza kukuuliza umenionaje hasa? Na unaweza
ukawa umemkera bila ya wewe kufahamu.
7.
Kwa hiyo unatarajia wa kike au wa kiume
Hii ni tabia ya watu wengi
kutaka kujua maoni binafsi ya mtu mwenye ujauzito. Licha ya ukweli kuwa kwa
mama mtoto ni mtoto, huna haja ya kutaka kujua maoni yake kwani kwa kawaida ni
Mungu pekee ndiye mwenye hiyo.
Kwa kutaka kujua maoni
yake, unaweza kuwa umemkera. Hivyo ili hilo lisitokee ni bora ukaa kimya kama
huna cha kuongea naye.
Si vibaya tukiwaacha
wapendwa wetu hawa wabebe mimba kwa raha zao, kwani maswali mengine hukatisha
tamaa.kwa upande mwingine lupimo sanitarium clinic huwa tunakawaida ya kutoa semina mbalimbali ikiwemo ya uzazi na magonjwa mbalimbali, tufikie katika vituo vyetu ufaidike zaidi na semina zetu ambazo tunazitoa kila jumamosi asubuhi bure kabisa,
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni