Msomaji wetu wa blog
hii ya lupimo sanitarium clinic karibu katika mwendelezo wa makala mbalimbali
zinazohusu afya yako zinazoletwa kwako na tabibu john lupimo wa lupimo
sanitarium ambapo leo anakuletea makala inayohusu matatizo ya njia ya mkojo kwa wanawake, lakini
kama unaswali unaweza kuuliza kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic. au unaweza kutufikia katika vituo vyetu
vilivyopo mikoani VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA
IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU
NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA
MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA
C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI
MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU
KALFONIA, Msomaji wetu mara baada ya kukumbusha mali na mawasiliano yetu
tunapopatikana sasa moja kwa moja twende kwenye makala yetu juu ya tatizo la
ugumba kwa mwanamke
Matatizo Ya Njia Ya Mkojo kwa Wanawake
Matatizo Ya Njia Ya Mkojo kwa Wanawake
Magonjwa ya mfumo wa njia ya mkojo na figo ni kati ya maradhi
yanayowasumbua watu wengi duniani. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kukojoa
mkojo wenye harufu mbaya au mkojo wenye rangi ya maziwa au damu.
Mgonjwa pia hupata maumivu ya kiuno na tumbo chini ya kitovu,
kukojoa mkojo kidogo mara kwa mara na kupata hisia za maumivu wakati wa
kujisaidia haja ndogo.
Kukojoa damu ingawa ni mojawapo ya dalili za ugonjwa huu, lakini
mara nyingi husababishwa na ugonjwa wa kichocho au mawe katika kibofu au katika
figo. Ugonjwa wa kifua kikuu katika mfumo wa mkojo pia unaweza kusababisha
dalili hii. Dalili nyingine hasa kwa watoto ni mwili kuwa na homa kali kama ile
ya malaria.
Utambuzi wa tatizo hili kwa wasichana na wanawake wengi unaweza
kuwa mgumu hasa pale wanapojihusisha na ngono hatarishi.
Wanawake wengi wa rika mbalimbali kuanzia vichanga hadi watu
wazima na vikongwe wanaweza wakakabiliwa na tatizo hili. Baadhi ya takwimu
zinaonyesha kuwa asilimia 10 ya wanawake wote duniani hupata tatizo la maradhi
ya ngono kila mwaka.
Takwimu zingine za afya ya jamii zinaonyesha kuwa, tatizo la
ugonjwa wa uambukizo katika njia ya mkojo huwapata wanawake takribani mara kumi
zaidi ya wanaume.
Wachunguzi wa masuala ya afya ya wanawake wanaongeza kusema
kwamba wanawake wenye umri kati ya miaka 16 na 35 ndiyo wanaopata maradhi haya
mara kwa mara.
Wengi wao hushindwa kuwaeleza madaktari kuhusu hali zao
kuhusiana na tatizo hili kutokana na kuona aibu au kuwa na hofu ya kushukiwa
kuwa ni wazinifu.
Katika utafiti uliofanywa na Ahamed Al-Badr na Ghadeer Al-Shaikh
wa Saudi Arabia, ulibaini kuwa asilimia 60 ya wanawake hukabiliwa
na tatizo hili.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Chuo
Kikuu cha Sultan Qaboos toleo la mwaka 2013, ulibaini kuwa wanawake wanene na
wale wenye ugonjwa wa kisukari, wako katika hatari kubwa ya maradhi haya ya
njia ya mkojo.
Utafiti
huo unaongeza kusema kuwa tatizo huwa kubwa zaidi kadri umri wa mwanamke
unavyoongezeka
Madaktari wa Magonjwa ya Kuambukiza wanasema “Ugonjwa wa
uambukizo katika njia ya mkojo ni tatizo linalojitokeza mara kwa mara kwa
wanawake waliokoma kupata damu ya hedhi”
Katika utafiti mwingine uliofanywa hapa nchini Tanzania na
kuchapishwa mwaka 2009 na A. Masinde pamoja na wenzake kutoka katika Kitengo
cha Magonjwa ya Wanawake cha Hospitali ya Bugando Mwanza, ilibainika kuwa
wanawake wengi wajawazito wanakabiliwa na tatizo hili. Na miongoni mwao wengi
huwa hawaonyeshi dalili za moja kwa moja za maradhi haya.
Wanawake wengi wanaopata tatizo la uambukizo katika njia ya
mkojo, hawana habari za kutosha zilizo sahihi juu ya vyanzo na madhara ya
tatizo hili linalosumbua mamilioni ya wanawake duniani.
Hii huwafanya wengi wachelewe kupata huduma sahihi za matibabu,
jambo ambalo huambatana na athari nyingi za kiafya na kiuchumi kwa familia zao
na taifa kwa ujumla.
Magonjwa ya njia ya mkojo mara nyingi hutokana na uambukizo wa
bakteria katika njia ya mfumo wa mkojo. Bakteria hawa hushambulia figo,
mirija miwili inayotoa mkojo ndani ya figo kupeleka katika kibofu cha mkojo.
Mara nyingi uambukizo huo unaotokana na bakteria huanzia katika
uke na kuingia ndani ya njia ya mkojo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba njia ya
mkojo ya mwanamke kutoka ukeni hadi ndani ya kibofu ni fupi sana na
inakaribiana na njia ya haja kubwa.
Ufupi wa njia hii huwezesha bakteria kuingia kwa urahisi zaidi
katika kibofu cha mkojo na kusababisha uambukizo katika mfumo wa mkojo.
Baadhi ya bakteria wanaosababisha uambukizo katika njia hii kwa
kawaida huishi ndani ya matumbo yetu na hutoka nje pamoja na kinyesi wakati
tunapojisaidia haja kubwa.
Sababu zingine zinazochangia kutokea kwa ugonjwa huu ni pamoja
na wanawake wengi kutozingatia usafi wa sehemu za siri hasa wakati wa
kujisaidia.
Wasichana na wanawake wengi wanapomaliza kujisaidia haja
kubwa, hujisafisha katika njia ya haja kubwa kabla ya kusafisha ukeni. Jambo
hilo husababisha bakteria kuchukuliwa kwa mikono toka katika njia ya haja kubwa
na kuwaingiza ukeni.
Kufanya tendo la ngono kwa muda mrefu au kushikashika viungo vya
kike bila kunawa kwa maji safi na sabuni, kunaweza kuwa chanzo cha tatizo hili
pia. Kufanya hivyo husababisha bakteria waingie kwa urahisi ndani ya kibofu na
kuleta uambukizo.
Wataalamu wa masuala ya afya ya wanawake wanakadiria kuwa kati
ya asilimia 75 hadi 90 ya maambukizi katika njia ya mkojo kwa wasichana na
wanawake wanaoshiriki tendo la kujamiiana hutokana na kufanya ngono mara kwa
mara.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa L.E.Nicolle wa mwaka 2008
uliochapishwa katika jarida la The Urologic Clinics of North America. Nicolle
ni mtaalamu wa sayansi ya maikrobailojia katika Chuo Kikuu cha Manitoba, nchini
Canada.
Jambo lingine linalowaweka wanawake wengi katika hatari hii, ni
kunawa kwa maji yenye povu jingi la sabuni au kutumia sabuni yenye kemikali
kali kusafisha ukeni. Sabuni zenye kemikali husababisha uvimbe ndani ya njia ya
mkojo na husababisha athari katika njia ya mkojo.
Ukeketaji wa wanawake au wasichana, kuumia kwa uti wa mgongo,
ulemavu katika maumbile ya njia ya mkojo pamoja na kutokupata choo vizuri pia
ni baadhi ya sababu zinazochangia kutokea kwa tatizo hili.
Lingine linalosababisha ukubwa wa tatizo hili kwa wanawake ni
ile tabia ya kutokunywa maji ya kutosha.
Tabia nyingine hatarishi kwa wanawake na wasichana ni kukaa na
mkojo kwa muda mrefu bila kwenda kujisaidia hasa wawapo safarini.
Mkojo unapokaa katika kibofu kwa muda mrefu hutoa nafasi kwa
bakteria kuzaliana kwa wingi na kusababisha kibofu kishindwe kufanya kazi zake
vizuri.
Kukaa na mkojo kwa kipindi kirefu pia huwapa nafasi bakteria
kupanda juu katika mirija inayotoa mkojo ndani ya figo na kufanya mashambulizi.
Kukaa kwa muda mrefu na vitambaa vya kukinga damu ya hedhi bila
kubadilisha pia huchangia kwa kiwango kikubwa kutokea kwa tatizo hili.
Baadhi ya wanawake hutumia vitambaa ambavyo si salama kwa afya
kiasi kwamba huwawia vigumu kuepuka tatizo hili kila mara wawapo katika siku za
hedhi.
Magonjwa ya njia na mfumo wa mkojo kwa wasichana na wanawake kwa
ujumla ni chanzo kikubwa cha upotevu wa mapato ya familia kutokana na ununuzi
wa dawa na kulipia gharama za matibabu na pengine kulazwa hospitalini mara kwa
mara.
Mwanamke anayelazwa hospitalini kutokana na matatizo yatokanayo
na maradhi katika njia ya mkojo anatazamiwa kukaa hospitalini kati ya siku nne
hadi sita akiendelea kupata matibabu.
Hiki ni kipindi kirefu hasa katika nyakati hizi ambapo hali ya
maisha inazidi kuwa ngumu kiuchumi. Lakini pia magonjwa mengine yanayoshambulia
mfumo wa mkojo yanaweza kushambulia mfumo wa uzazi wa mwanamke na kusababisha
matatizo kama vile ugumba, kuharibika kwa figo au shinikizo la damu na
kiharusi.
Ni vema jambo hili likaeleweka vyema miongoni mwa wasichana na
wanawake kwa ujumla ili tahadhari zichukuliwe mapema.
Pale msichana au mwanamke anapogundua kuwa ana ugonjwa katika
njia ya mkojo, asichelewe kupata huduma za tiba.
Hospitali nyingi nchini zinao wataalamu wanaoweza kutibu tatizo
hili kwa ufanisi mkubwa endapo mgonjwa atawahi kupata tiba. Lakini tatizo hili
linaweza kuzuilika endapo wanawake watazingatia kanuni za afya na usafi wa
mwili kikamilifu.kwa msaada zaidi na matibabu tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni