Jumatano, 23 Machi 2016

TUNDA LA TUFAHA (APPLE) LINANAFASI YA KUONDOSHA TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO



Mawe kwenye figo siyo tatizo geni miongoni mwa watu hivi sasa, hasa wenye umri mkubwa.



Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaam linajulikana kama ‘Gallstones’.

Tunapozungumzia tatizo la mawe kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo vidogo hii hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.

Mara nyingi tatizo hili hutibika kwa njia ya upasuaji na kuvitoa, huku zoezi hilo likigharimu fedha nyingi na pia husababisha maumivu wakati wa kufanya oparesheni hiyo. Lakini kwa kutumia tiba mbadala ya vyakula, pia huweza kukusaidia kuondokana na tatizo hilo.

Juisi ya tufaa (pure apple juice) glasi kubwa nne kila siku kwa siku tano mfululizo. Au ulaji wa tufaha nzuri tano badala ya juisi. Tunda hili huweza kusaidia katika kufanya kazi ya kulainisha kwanza mawe tumboni.

Pia unaweza kutumia mchanganyiko wa nusu kikombe cha juisi halisi ya limau na nusu kikombe cha mafuta halisi ya mzaituni (pure olive Oil). Kinywaji hiki utapaswa kutumia usiku kabla ya kulala.

Pia weka utaratibu wa kukagua haja yako na utaona vitu rangi ya kijivu au kijani vinavyong’aa na hapo utakuwa umefanikiwa.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni