Ijumaa, 25 Novemba 2016

Faida ya Kula spinachi na viazi

Imebainika kuwa ulaji wa matunda na mbogamboga zenye kimeng’enyo cha carotenoid kwa wingi kama vile karoti, spinachi, tikitiki maji na hata viazi vitamu, unaweza kuondoka katika hatari ya kupata magonjwa kupitia viondoa sumu vinavyopatikana ndani yake.

Watafiti kadhaa wameitaja carotenoid kuwa ni chanzo kizuri cha vitamin A. miongoni mwa sifa kuu ya kimeng’enyo hicho ni kuukinga mwili dhidi ya maradhi makubwa yakiwemo shinikizo la damu pamoja na saratani ya matiti.
 
 tafiti nyingine zimeonyesha athari za matunda na mbogamboga pamoja na carotenoid iliyomo ndani yake kwa afya ya matiti.
Nyingi kati ya tafiti hizo zilionyesha matokeo mchanganyiko, lakini kwa ujumla zile zilishauri kuwa kimeng’enyo cha carotenoid inayopatikana kwenye mbogamboga na matunda yenye chembechembe za rangi ya njao, machungwa au nyekundu ina matokeo chanya kwa afya ya matiti.

Katika utafiti huo uliokuwa ukifanywa tangu mwaka 1996, kwa kupitia ripoti ya vyakula waliyokuwa wakitumia hadi mwaka 1998 na kisha kufanya tathimini mwaka 2005, 2007 na mwaka 2010 ilibainika kuwa wasichana wengi waliotumia mboga hizo hawakuwa nadalili zozote za kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na wale ambao walikuwa hawatumii.
 
NB: kwa ushauri malimbali wa kiafya naomba unipigie muda wowote kwa namba yangu ya 0759324414

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni