Jumanne, 2 Februari 2016

AJALI MBAYA.. BODABODA AGONGA GARI NA KUFARIKI PAPO HAPO.

habari hii inaletwa kwako kwa hisani kubwa mkubwa ya lupimo sanitarium clinic kwa huduma nzuri ya kiafya wasiliana nasi kupitia namba 0769368546 au 0719097574 karibu sana

DEREVA wa bodaboda, Colnery Mpande (18), mkazi wa Kiluvya Kwa Komba, amekufa baada ya pikipiki aliyokuwa akiiendesha kugonga gari kwa nyuma na yeye kuangukia barabarani na kukanyagwa kichwa na gari lingine.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi alisema pikipiki hiyo baada ya kuligonga gari hilo ilipoteza mwelekeo na kuanguka barabarani kisha kugongwa kwa kukanyagwa kichwa na kufa papo hapo.

Alisema tukio hilo ni la jana saa 10 alfajiri eneo la Mpakani, katika barabara ya Morogoro wilayani Kibaha.

Kamanda alisema gari aliloligonga kwa nyuma dereva huyo wa bodaboda lilisimama ghafla na halikuonesha ishara kwamba linakatisha kuingia kushoto.

Alisema Mpande alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili MC 332 AXL aina ya Sanlg akitokea Kibaha kuelekea Kiluvya na aligonga gari lenye namba za usajili T 616 DCB aina ya Mitsubishi Canter lililokuwa likiendeshwa na Shaaban Ally kutoka Kibaha kwenda Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda, Mpande alikanyangwa kichwa na lori la mizigo lenye tela na namba za usajili T 559 BFA/T 874 AQF likiendeshwa na Daniel Joseph aliyekuwa akitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni