Tatizo La Kutokwa na Kinyama Sehemu Ya Haja Kubwa : Chanzo, Athari Zake na Tiba Yake .
Lupimo sanitarium clinic ni
kituo cha tiba asili wanatibu magonjwa kama
kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na magonjwa mengine mengi, kutana tabibu
bingwa ambae ni mkurugenzi wa lupimo sanitarium clinic John lupimo mpigie simu
sasa hivi umweleze tatizo lako kupitia 0742120577,0769368546 au 0672666601.
Tatizo la kutoka na kinyama ama uvimbe katika sehemu ya haja kubwa hujulikana kama Bawasiri.
Katika lugha ya kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kama haemorrhoids ilihali katika lugha ya kiingereza, hujulikana kama Piles.
Tatizo hili husababishwa na kuvimba, kuharibika na kuondoshwa katika eneo lake kwa mishipa ya damu katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Tatizo hili huwaathiri zaidi watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu asilimia 50 ya idadi ya watu wote wako hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 50.
Aina Za Bawasiri :
Kuna aina mbili za bawasiri
Bawasiri ya nje:
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo.
Mara nyingine, mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina ya bawasiri ambayo kitaalam inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
Bawasiri ya ndani:
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Hutokana na kuvimba na kuharibika kwa vimishipa vya aina ya artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
-Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
-Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
-Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
-Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je, bawasiri husababishwa na nini?
Chanzo chake kikuu kitaalam hakijulikani, ingawa mambo yafuatayo yanaweza kusababisha au kukuweka katika hatari ya kupata bawasiri:
i.
Tatizo
sugu la kuharisha
ii.
Kupata kinyesi kigumu
iii.
Ujauzito
iv.
uzito
kupita kiasi (obesity)
v.
Mazoezi
ya kunyanyua vitu vizito
vi.
Kuingiliwa kinyume
na maumbile
vii.
Umri
mkubwa
viii.
Mambo
yanayoongeza shinikizo katika utumbo mpana
kama kukaa muda mrefu mahali pamoja
ix.
Matumizi
ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu kuliko vya kuchuchumaa na kujisaidia kwa mda
mrefu wakati wa haja.
Dalili za bawasiri
i.
Damu
kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
ii.
Maumivu
au usumbufu wakati wa kujisaidia
iii.
Kinyesi kuvuja
iv.
kijiuvimbe
katika eneo la tundu la haja kubwa
v.
Ngozi kuwasha
katika eneo la tundu la haja kubwa
vi.
Na
kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa.
Matatizo
yanayoweza kutokana na bawasiri:Upungufu wa damu mwilini (Anaemia) na bawasiri iliyojikaba (Strangulated haemorrhoids)
Kipimo cha kidole cha shahada kwa njia ya puru (Digital Rectal Examination), Kipimo cha njia ya haja kubwa cha kutazama moja kwa moja (Proctoscope) na Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
usiendelee kuteseka na ugonjwa huo kwani lupimo sanitarium clinic tunalitibu vizuri, tufikie katika vituo vyetu vilivyopo mikoani
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni