Jumanne, 2 Februari 2016

Wednesday, February 3, 2016

Spika Wa Bunge Job Ndugai Akubali Kuzifumua Kamati Za Bunge.....Zitto Kabwe Kurudishwa PAC, James Mbatia Kamati Ya Bajeti.

habari hizi zinaletwa kwako kwa hisani kubwa ya lupimo sanitarium clinic kwa matibabu mazuri ya afya yako, mawasiliano yetu 0769368546 au 0719097574 karibu sana


Baada ya malalamiko ya wabunge wa upinzani juu ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kuzipangua kamati hizo.

Taarifa za uhakika toka Bungeni mjini Dodoma zinasema, licha ya kuwapo kwa baadhi ya wajumbe walioomba kuhamishwa kwenye kamati walizopangiwa awali, kumekuwapo na mazungumzo kati ya Kambi ya Upinzani Bungeni na kiti ofisi ya Spika juu ya suala hilo.

Inaelezwa kati ya wajumbe watakaohamishwa kutoka kwenye kamati zao za awali ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe aliyekuwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Jamii na sasa atapelekwa  Hesabu za Serikali (PAC).

Naye Mbatia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, sasa atapelekwa kwenye Kamati ya Bajeti aliyokuwa akitumikia kwenye Bunge la 10.

Spika wa Bunge, alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo kupatikana.

Juzi Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bunge, Tundu Lissu, alisema wanafikiria kumpeleka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kwenye kamati ya PAC ili awe mwenyekiti wao.

“Wasipokubali (kubadilisha wajumbe) hatutakubali ungozi tutaacha, mimi mwenyewe sheria ndogo siendi, huko ni kupoteza muda kwa sababu hakuna kamati ya ovyo vile, nitaenda sheria na katiba na kushiriki mijadala, kura tu ndiyo sintopiga, hoja yoyote ya kisheria ikiibuka bungeni nitaibuka na watashangaa,” alisema Lissu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni