Alhamisi, 14 Aprili 2016

     FAIDA LUKUKI ZA MAHARAGE YA SOYA

Maharage ya soya ni miongoni mwa vyakula maarufu nchini Tanzania, wengine wanavipenda na wengine hawavipendi, hiyo inatokana na mtu kujua au kutokujua umuhimu wa zao hili muhimu kiafya.

Nchini China, zao hili limekuwa sehemu ya mlo kamili wa wananchi wake kwa karne nyingi. Kama inavyojulikana, Soya ina faida nyingi za kiafya kutokana na kuwa na kiasi kingi cha protini na madini. Soya huweza kutumika ikiwa katika aina mbalimbali ya vyakula.

Soya ni zao lenye uwezo mkubwa sana wa kupambana na maradhi hatari mwilini, na inalifanya zao hili kuwa muhimu kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha mchanganyiko wa virutubisho vingi vya madini, vitamini, ‘flavoids’, ‘isoflavones’, ‘polyphenols’, ‘terpenes’, ‘saponins’, ‘phytosterols’ na ‘phytate’.
Faida zingine za Soya

Husaidia kuzuia mtu asipatwe na saratani zitokanazo na homoni za mwili, kama vile saratani ya matiti na tumbo. Vile vile Soya ina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa mifupa na matatizo ya wanawake baada ya kufikia ukomo wa hedhi (menopause).

Vyakula na vinywaji vyote vitokanavyo na soya vimethibitika kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta mabaya na kolestrol, hivyo kuwa chakula ama kinywaji chenye faida tupu kwa mtumiaji.

Kwa kawaida Soya hutumika kama zao la kuzalisha mafuta ya kupikia ambayo huwa ni mazuri sana kiafya. Soya imejipatia umaarufu kiasi hicho, baada ya kugundulika kuwa na madini, vitamini na virutubisho vingine vinavyopatikana kwenye samaki, nyama, mayai na maziwa. Kwa maana nyingine, mtu anayekula Soya ni sawa na yule aliyekula vyakula hivyo.

Virutubisho vya Soya aina ya protini na ‘isoflavones’ hushusha kiwango cha Kolestrol mbaya (LDL) mwilini, halikadhalika hupunguza ugandaji wa damu hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya mtu kupatwa na mshituko wa moyo au kiharusi. Vile vile Soya huboresha msukumo na mishipa ya damu mwilini.

Kumbuka kuwa, protini mwilini huongeza uwezo wa mwili kuhifadhi na kunyonya madini ya ‘calcium’ kwenye mifupa. Ni mlo safi kwa wagonjwa wa kisukari na wenye matatizo ya figo. Kamba lishe (fibre) iliyomo, hurekebisha kiwango cha sukari na uchujaji sumu wa figo.

Soya ni nzuri kwa watu wenye matatizo ya kuwa na macho mekundu, ukosefu wa choo na kusikia kiu kila wakati. Aidha tahadhari inatolewa kwa watu wenye matatizo ya kuharisha, tumbo kuuma, minyoo na kusikia kiuungulia, wasitumie Soya kwa wakati huo.

Kwa ujumla, Soya, iwe maharage au vinywaji vyake, ni muhimu kutumiwa mara kwa mara kwani ina faida nyingi katika kupambana na maradhi na kuimarisha afya zetu.




kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic,instagram.com/lupimoclinic
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni