Jumatano, 13 Aprili 2016

JINSI YA KUKABILIANA NA TATIZO LA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI.
kasemaje-com-jinsi-ya-kukabiliana-na-tatizo-la-kuziba-kwa-mirija-ya-uzazi-2_984d5edfec76ab95f996419f1ff73535c41d8122.jpg 

Leo naelezea  namna ya kukabiliana na tatizo la kuziba mirija ya uzazi ambalo limekuwa likiwasumbua baadhi ya watu na kusababisha washindwe kupata watoto.

CHANZO CHA TATIZO
  

Chanzo kikuu cha uzibaji huu ni maambukizi sugu ya kizazi ambayo kitaalam huitwa 'pelvic inflamatory Diseases' au kwa kifupi huitwa 'PID'
Maambukizi ya kizazi huambatana na maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na uchafu au majimaji ukeni yanayoambatana na muwasho au harufu mbaya. Maumivu haya ya chini ya tumbo husambaa kulia na kushoto hadi kiunoni.

Siyo vizuri kupatwa na tatizo hili mara kwa mara kama upo katika umri wa kuzaa, kwani utafiti unaonesha kwamba mwanamke ambaye tayari ameumwa hivi mara moja na akatibiwa na kupona yupo katika asilimia kumi na mbili ya kupata tatizo la kuziba mirija ya uzazi, ambaye ameshaumwa hivi mara mbili ana asilimia 23 ya kupata tatizo la kuziba mirija, ambaye ameshaumwa mara tatu ana asilimia 53 ya kupata tatizo hili la kuziba mirija ya uzazi.

Mirija pia inaweza kuziba kutokana na athari katika tabaka la ndani la kizazi. Vilevile mama anaweza kupata maambukizi ya kizazi baada ya kujifungua, iwe kawaida au kwa njia ya upasuaji na kusababisha mirija ya uzazi kuziba.
 

Dalili hapa ni kuendelea kuumwa na tumbo au chango kwa muda mrefu hata wiki tatu na zaidi baada ya kujifungua. Matatizo katika kidole tumbo pia huchangia hali hii.

Hali ya kushikamana kwa viungo vya uzazi siyo tu huziba mirija ya uzazi, mirija inaweza kuwa mizima lakini kutokana na hali hii mirija inabanwa na kushindwa kufanya kazi. Maambikizi yanayochangia tatizo hili la kuziba mirija mbali na utoaji wa mimba, magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende, HIV pia huchangia, mirija iliyofungwa kizazi ni vigumu kurekebisha hivyo inakuwa imeziba moja kwa moja.

UCHUNGUZI
Tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi kwa harakaharaka utaliona kama tatizo dogo lakini kwa undani lina changamoto nyingi. Vipimo vya kisayansi vinatakiwa wala siyo hisia na kudhania.


Mwanamke anatakiwa apimwe kujua nini kinasababisha kwa hiyo vipimo vya damu kuangalia maambukizi, vichocheo au homon vitafanyika, kipimo cha Ultrasound na kipimo cha Hysterosalpingogram vilevile Laparoscopy inaweza kufanyika. Matibabu ya maambukizi na kasoro nyingine vitafanyika baada ya uchunguzi.
kwa upande wa lupimo sanitarium clinic hatufanyi upasuaji bali tutakupima na vipimo vyetu vya mwili mzima baada ya hapo tutakupatia dawa za kwenda kuzibua mirija hiyo na utapata ujauzito bila shida



kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic,instagram.com/lupimoclinic
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni