Jumamosi, 9 Aprili 2016

     KAZI IFANYWAYO MWILINI KWA KULA MATUNDA 

  
Unapaswa kujua kuwa mwanaume uzito wake asilimia sitini 60% ni maji na mwanamke ni asilimia hamsini 50%, hii ni kutokana na mwanamke kuwa na sehemu kubwa ya kuhifadhi mafuta kuliko maji lakini la msingi ni kuwa kama unapendelea kula matunda na mbogamboga vitu hivi hurudisha kiasi kikubwa cha maji yaliopotea mwilini kutokana na shughuli zako au orodha ya hapo chini. 

Kumbuka kuwa katika mwili wa mwanadamu hupoteza kiasi cha 1.5lt lita moja na nusu kwa siku. Kwa kutumia matunda na mbogamboga hurudisha kiasi cha 600ml za maji hayo, kiasi kichobaki unalazimika kunywa kupitia maji.
 

Figo kwa siku utengeneza kiasi cha 600ml za mkojo hii inafaida kubwa sana kwa ajili ya kutoa sumu mwilini.
500ml za maji mwilini hupotea kupitia ngozi {jasho}
300ml hupotea kupitia mapafu yaani kwenye kupumua na
100ml kwenye haja kubwa.
 

Baadhi ya matunda na mbogamboga zina kiasi kikubwa cha maji kinacho kadiriwa kufikia 70% na mengine yamezidi kiasi hicho kulingana na maumbile yao km tikiti maji, dafu nk. Kutokana na kiasi kikubwa cha sukari, madini na vitamin vilivyoko kwenye matunda vimeonekana vyenye msaada mkubwa sana kwa mtu anaye harisha. Lakini matunda yanahusika na kuusafisha mwili na damu kwa ujumla wake, maana ndani yake kuna aina ya viinlishe vyenye kuamsha utendaji bora wa mifumo yote ya mwili.
 

FAIDA ZA MATUNDA NAUMUHIMU WAKE.
 

Matunda ni chakula kamili na dawa pia.
Matunda na mbogamboga zinaweza kufanya maajabu katika tiba ya magonjwa sugu yalioshindika kwa kila aina ya dawa. Kwa matumizi sahihi ya vitu hivi unaweza kuepukana na magonjwa yasio ya lazima. Kitaalamu tunasema hii ni njia sahihi ya asili yenye lishe na dawa. Matunda haya yana ladha nzuri, maji na utajiri wa vitamin na madini muhimu mwilini, alkali,tindikali ya asili, protein,mafuta na nyuzinyuzi; wakati mengine yana harufu nzuri yakuvutia unapokula hayakinaishi. Matnda hufanya kazi kubwa ya kutoa sumu na maozea mwilini.
 

Matunda yana 5-15% ya sukari, ambayo hufyonzwa moja kwa moja kuingia mwilini tofauti na vyakula vingine. Aina hii ya sukari hufyonzwa na kuingia kwenye damu bila ya msaada wa vimeng’enya, hivyo basi kwa kula matunda tunakula sukari ambayo imeshameng’enywa tayari.

 Hii huwasaidia sana watu wenye matatizo ya kumeng’enya chakula. Kwa asili matunda yana kiasi kikubwa cha alkaline ambacho hupunguza kiasi kikubwa cha tindikali ambayo haina faida mwilini. Hii hupunguza kiasi kikubwa cha kazi ambayo ingefanywa na mapafu,ini,figo nk. Faida nyingine ni kusaidia kwenye baadhi ya magonjwa kama vile pumu,bronchitis,pleuricy, homa ya manjano na figo. Usisahau kuwa ascorbic acid na alkaline iliopoko kwenye matunda huuwa bacteria na kuuacha mwili ukuwa huru mbali kabisa na maradhi.
 

Kwa sababu ya uchache wa protien na mafuta yalioko kwenye matuda umeng’enyeka kiraisi zaidi ukilinganisha na vyakula vingine.
Ni vyema kama utakwangua tunda kutoa ganda la juujuu tu maana kiasi kikubwa cha virutubisho vipo kwenye ganda haswa upande wa ndani. 


Tumia tunda likiwa freshi na kama ni juice usiongeze sukari labda kama inalazimu tumia asali au karoti alafu ni vyema kama hutatuchanganya matunda mabalimbali kwa pamoja. La msingi kulitambua ni kuwa matunda ni bora kuliko nafaka.




kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic,instagram.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni