Jumatatu, 11 Aprili 2016

LEO NIMEKULETEA HII YA MBEGU ZA TIKITI MAJI KUTUMIKA KAMA TIBA



Tikiti maji ni moja ya tunda ambalo linapendwa sana, lakini pia ni moja kati ya matunda yenye maji mengi na matamu  ndani yake.

Mbali na kuwa na maji yenye ladha nzuri  pia tunda hili linafaida kadhaa katika masuala ya afya hususani pale linapotumika ipasavyo.
Leo tutaangalia faida za mbegu za tunda hili ambapo ni miongoni mwa mbegu zenye kiwango kikubwa cha protini.
mbegu hizo zina vitamin B ambayo ni muhimu pia mwilini kwani husaidia kubadili chakula kuwa katika mfumo wa nishati.
  mbegu hizo zinauwezo mzuri wa kusaidia katika mmeng’enyo wa chakula pamoja na mfumo wa fahamu, huku zikisaidia pia kuimarisha afya ya ngozi kwa mtumiaji.
Tunda la tikiti maji likiwa na mbegu zake
 Pia mbegu hizi za tikiti zinasifa ya kuwa na kiwango kizuri cha madini ya ‘magnesium’ ambayo husaidia kuthibiti shinikizo la damu, hali kadhalika ndani yake kuna madini ya chuma, ‘zinc’, 'sodium' na 'manganes.’
“Mbegu zake zinapoliwa husaidia kushusha shinikizo la damu na zikikaangwa na kusagwa huwa ni dawa ya maumivu wakati wa kujisaidia,

mbegu za tikiti maji zikikaangwa na kisha kusagwa na mgonjwa akanywa huweza kutibu kifua kikuu  kwa mhusika endapo mhusika  atakuwa akitumia vijiko viwili kutwa mara mbili.
Kama unasumbuliwa na magonjwa sugu pia unaweza fika lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoani kwa matibabu zaidi.
 
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic,instagram.com/lupimoclinic.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni