ZIFAHAMU SABABU ZINAZOCHANGIA MIGUU KUVIMBA NA KUJAA MAJI
Si ajabu kusikia baadhi ya watu wakilalamika kuhusu tatizo la kuvimba miguu au kujaa maji na kuwa na muonekano kama vile uvimbe.
Kimsingi kuna sababu za uwepo wa tatizo hili ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo ambapo kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi zake vizuri, husababisha damu kushindwa kufika vizuri katika viungo vingine vya mwili ikiwemo miguuni.
Magonjwa ya ini nayo ni moja ya sababu ya miguu kuvimba hii ni kwa
sababu magonjwa hayo huchangia kupunguza uwezo wa utendaji kazi wa ini
ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa vitu muhimu vinavyopatikana katika
damu mfano protin (albumin).
Lakini pia tatizo hili la miguu kujaa maji huweza kujitokeza kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya mwili, mfano kina mama wajawazito huweza kupatwa na tatizo hili kutokana na miili yao kuwa na ongezeko la mahitaji ya damu ili kuweza kuutoshereza mzunguko mzima hadi kufika kwa kiumbe/viumbe walioko tumboni.

Hizo ni baadhi tu ya sababu za tatizo hili la kuvimba kwa miguu,
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni