Jumatano, 20 Januari 2016

Hizi ndizo sababu mimba kutunga nje ya mji wa  mimba(ectopic preginancy)



Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au Ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kuna watu wanaposikia na kusoma habari za mimba kutunga nje ya mji wa mimba wanachukulia ni kitu kisichowezekana na ni jambo la kutishiana.
Nikuhakikishie msomaji wangu kuwa hili ni miongoni mwa matatizo yanayowasumbua sana akina mama. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.
Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo.Katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kuna sehemu nyingi ambazo kila moja ina umuhimu wake ikiwa sehemu mojawapo itapata hitilafu husababisha athari katika mfumo wa uzazi. Miongoni mwa sehemu muhimu sana ni Ovari ambayo ndiyo sehemu mayai ya uzazi yanapotengenezwa.
Mayai haya husafiri kupitia mirija ya Fallopian. Kazi za mirija ya Fallopian ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji (ovary) mpaka kwenye mfuko wa uzazi (uterus). Utungisho wa yai la kike (ovum) na mbegu ya kiume (sperm) hufanyika kwenye mirija hii.
Mara baada ya utungisho, misuli inayozunguka mirija ya Fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyopo ndani ya mirija hii husukuma kiinitete au yai lililorutubishwa na kulipeleka kwenye Uterus. Yai lililorutubishwa au kiinitete, lifikapo kwenye Uterus hujipachika katika mojawapo ya kuta zake kwa ajili ya kuendelea kurutubishwa, kukua taratibu na hatimaye kufanya mtoto.
Inapotokea misuli hii kushindwa kufanya kazi au vinyweleo hivi kukosekana, kiinitete hushindwa kusafirishwa kuingia kwenye Uterus na hivyo hujitunga nje ya Uterus na kusababisha Ectopic Pregnancy. Karibu asilimia 1-2% ya mayai yaliyorutubishwa hutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.
λ Aidha, zaidi ya asilimia 95% ya mimba zinazotunga nje ya Uterus hutokea kwenye mrija wa Fallopian. Mimba zinazotunga kwenye mrija huo husababisha kiinitete Embryo kujipachika katika kuta zake na hivyo kusababisha mishipa ya damu inayopita karibu na mrija wa Fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema husababisha madhara zaidi na hata kifo.
Aina za Ectopic Pregnancy
Kuna aina kuu nne za mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi, nazo ni;
1. Mimba zinazotunga kwenye mirija ya Fallopian.
2. Mimba zinazotunga nje ya Uterus na nje ya mirija ya Fallopian.
3. Mimba zinazotunga ndani na nje ya Uterus kwa wakati mmoja.
4. Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa uzazi.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vIZURI ukafuatilia makala haya.
Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au Ectopic Pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.
Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo. Baada ya utangulizi huo tulia angalia aina za mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi.
Leo tutachambua aina hizo na sababu zake. Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian. Sababu kubwa inayopelekea mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian ni kushindwa kusafirishwa kwa kiinitete katika mirija hii hali inayotokana na mabadiliko katika hali ya mirija au uwezo duni wa mirija hiyo katika kusukuma kiinitete kuingia kwenye uterus kwa sababu ya ukosefu wa vinyweleo kutokana na magonjwa mbalimbali yanayoathiri muundo na maumbile ya mirija ya fallopian.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian huwa zina 
madhara makubwa zaidi kwa sababu eneo hili ni jembamba mno kuweza kuhimili ukuaji wa mimba na pia lina mishipa mingi ya damu inayopita karibu ambayo ipo hatarini kupasuka hivyo kupelekea mgonjwa kupoteza damu nyingi sana.
Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian
Baadhi ya mimba huweza kutunga kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai (ovary), kwenye shingo ya uzazi (cervix) au ndani ya tumbo (intra-abdominal). Aina hii ya mimba ni chini ya asilimia tano ya mimba zote zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi.

Mimba inayotungwa ndani ya tumbo (intra-abdominal) wakati fulani huweza kutoa mtoto aliye hai tofauti na aina nyingine za mimba zinazotunga nje ya uterus. Hata hivyo uzalishaji wake hufanywa kwa operesheni ingawa hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu suala hili mpaka sasa.
Madhara ya kutokea kwa upotezaji wa damu pamoja na maambukizi ni makubwa hivyo mara nyingi mimba za namna hii huitaji kushughulikiwa haraka ili kumuepushia madhara makubwa mama mjamzito.
Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja Wakati fulani, mayai mawili yaliyorutubishwa kwa wakati mmoja hutokea kupandikizwa sehemu

mbili tofauti. Moja likipandikizwa nje ya uterus na jingine ndani ya uterus. Katika aina hii ya • ectopic pregnancy, uwezekano wa yai lililotungwa ndani ya uterus kukua na kutoa mtoto ni mkubwa sana.
Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa Uzazi

Wakati fulani hutokea kuwa, hata baada ya operesheni ya kuondoa mimba iliyotunga nje ya kizazi kufanyika, baada ya muda fulani seli za kiinitete huendelea kukua na kujitengeneza tena kufanya kusanyiko la seli kama mimba nyingine. Hali hii huitwa mimba zinazoendelea kutunga
nje ya mfuko wa uzazi au persistent ectopic pregnancy.


Sababu za mimba kutunga nje ya mji wa mimba:
1. Matatizo katika mirija ya fallopian.

Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na:
• Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke (PID).
• Matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba (Intra-uterine contraceptive devices).
• Kuoteana kwa tishu za uterus kwenye viungo vingine vya uzazi au endometriosis.

2. Uvutaji sigara
Uvutaji sigara kwa mwanamke una uhusiano mkubwa na utungaji wa mimba nje ya kizazi. Imeonekana kwamba wanawake wanaopendelea kuvuta sigara mara kwa mara wana hatari ya kupatwa na tatizo hili mara tano zaidi ya wale wasiovuta kabisa. Hali hii husababishwa na ‘nicotine’ iliyomo ndani ya tumbaku. Kwa kawaida nicotine huchochea kusinyaa kwa mirija ya fallopian hali iletayo kuziba kwa mirija hiyo na hivyo kufanya kiinitete kushindwa kupita kwenye mirija kuingia kwenye uterus na kufanya mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian.
3. Upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani.

Operesheni yeyote inayohusu mirija ya fallopian inaongeza uwezekano wa mwanamke kutunga mimba nje ya uterus kwa vile mirija ya fallopian huwa imesinyaa kutokana na operesheni hiyo.
4. Matumizi holela ya baadhi ya dawa.

Matumizi ya baadhi ya dawa zenye homoni husababisha kupungua kwa uwezo wa mirija ya fallopian kusukuma kiinitete kuelekea kwenye uterus na hivyo kuleta uwezekano wa utungaji wa mimba nje ya kizazi. Dawa hizo ni kama dawa za kuzuia mimba zenye homoni za kike za progesterone, na dawa za kusaidia uzazi aina ya clomiphene.
Dalili za ectopic pregnancy

Katika wiki za mwanzo za ujauzito, mimba iliyotunga nje ya uterus huwa na dalili sawa na za mimba ya kawaida. Dalili hizi ni pamoja na mwanamke kukosa hedhi, kujaa kwa matiti, kichefuchefu, na uchovu wa mwili. Hali hii hufanya ugunduzi wa mimba iliyotunga nje ya uterus kuwa mgumu katika hatua zake za awali.
Hata hivyo dalili ya awali ya kuonesha kuwa mimba imetunga nje ya kizazi ni kuwepo kwa maumivu makali na damu kutoka ukeni. Maumivu yanaweza kuwa kwenye nyonga, tumbo au wakati mwingine kwenye mabega au shingo (iwapo kiwango cha damu inayotoka kwenye mirija iliyopasuka ni kingi sana mpaka kugusa kiwambo cha hewa).
Maumivu haya huweza kuwa makali na yanayokata kama kisu, na yanaweza kuwa upande mmoja zaidi wa nyonga ingawa si lazima yawe upande ulio na mimba.

Dalili nyingine
• Kizunguzungu na kuzimia kwa sababu ya kupoteza damu kwa wingi.
• Shinikizo la damu kuwa chini.
• Maumivu ya chini ya mgongo


kwa msaada zaidi na ushauri tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoani,

VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni