Lowassa Afunguka........Asema Kuitwa FISADI Kulimfanya Ajiondoe CCM Na Kuhamia Chadema
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Je umeshindwa kubeba mimba?
Je unauvimbe ndani ya mji wa mimba? Je unauvimbe kwenye ovari? Kutana na tabibu
bingwa wa tiba asilia ndugu John lupimo wa lupimo sanitarium clinic utatibiwa bila kufanyiwa
upasuaji, anazo dawa zinazotengenezwa kama tiba lishe, mpigie kwa namba
0742120577 au 0672666601.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Aliyekuwa
mgombea urais wa Chadema chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amesema kusakamwa kwa maneno ya kejeli,
vijembe na vitisho, kuitwa gamba na fisadi ndani ya CCM ndiko
kulikomfanya kukihama chama hicho na kwenda upinzani.
Lowassa
aliyekuwa na nguvu ya ushawishi ndani na nje ya CCM, alihamia Chadema
baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kumsaka Rais wa Tanzania,
katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana,
Lowassa alisema licha ya kuitumikia CCM kwa zaidi ya miaka 30 tangu
mwaka 1977, chama hicho kiliamua kutumia watu kumsakama kwa kila aina ya
maneno jambo lililomfanya achoke na kuamua kuondoka.
“Nakifahamu
Chama cha Mapinduzi, nakiheshimu kwani ndicho kilichonilea, lakini, kwa
hali tuliyokuwa tumefikia, inafika mahali unasema imetosha,” alisema Lowassa.
Alitaja
sababu nyingine iliyomfanya kuihama CCM kuwa ni kutaka mabadiliko na
aliamini mabadiliko ya kweli yatapatikana nje ya chama hicho tawala na
akisema hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alisema mabadiliko
yatatafutwa hata nje ya CCM.
Alisema
kwa namna yoyote, kamwe hana mpango na hawezi kurudi CCM na akasema
jukumu lililopo mbele yake kwa sasa ni kuijenga Chadema ambayo yeye ni
Mjumbe wa Kamati Kuu.
“Sina
mpango na wala siwezi kurejea CCM, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, na jukumu lililoko mbele yangu ni kukijenga na kukiimarisha
chama changu hiki kiwe imara tangu katika ngazi ya matawi,” alisema
na kuongeza kuwa kazi iliyoko mbele yake sasa ni kukiimarisha chama
hicho na wamejipanga kuzunguka nchi nzima kufanya kazi hiyo pamoja na
kuwashukuru wananchi kwa imani waliyoionyesha kwake na chama chake.
Lowassa
alidai kuwa kama si kura kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya
kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka
mabadiliko.
Alisema
kazi nyingine kubwa waliyonayo sasa ni kuhakikisha Katiba Mpya
inapatikana na Tume ya Uchaguzi inaundwa upya kwani iliyopo si huru hata
kidogo.
Alisema
kama isingekuwa busara na ukomavu waliouonyesha Ukawa, basi hata hali
ya siasa Tanzania Bara isingelikuwa shwari kama ilivyo sasa.
“Mara baada ya matokeo ya uchaguzi, niliwashauri vijana watulie, wasifanye fujo, nashukuru walinisikiliza.”
Alisema
katika uchaguzi huo yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa
matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.
“Nilishinda
na Ukawa ilishinda, kilichotokea kura zilichakachuliwa kwa kiasi
kikubwa… wao wanajua, Watanzania wanajua na kila mtu anajua, tulishinda
kwa kura nyingi sana na tulipokonywa ushindi wetu,” alisema.
Vijana wa Chadema kukamatwa
Alisema
miongoni mwa mambo yanayomuumiza na ambayo hatayasahau katika uchaguzi
huo ni kitendo cha polisi kwa maagizo ya watendaji wa Serikali
kuwakamata vijana waliokuwa wanakusanya matokeo na kuwadhalilisha ikiwa
ni pamoja na kuwaweka mahabusu.
Alidai
kuwa kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuvuruga kituo chao
walichokuwa wakijumuisha matokeo na kuacha kile cha CCM kilikuwa kibaya
na kilichoonyesha wazi kuwa hawakuwa tayari kukubali kuona wakishindwa.
Alisema: “Ni
aibu kubwa kwa Serikali kuwaumiza na kuwaweka ndani vijana wadogo
wasiokuwa na hatia eti kwa sababu tu walikuwa wakiunga mkono
mabadiliko."
Uhuru wa NEC
Lowassa
alisema miongoni mwa mambo yanayozorotesha chaguzi nchini ni NEC ambayo
alisema siyo huru na badala yake ni chombo kinachotumika na watawala.
Alisema chombo hicho hakitendi haki na kwamba ingekuwa mamlaka yake baada ya uchaguzi kwisha angekiondoa madarakani.
Alisema
wakati umefika kwa Watanzania kuungana kudai Katiba Mpya na tume huru
ya uchaguzi kwa maelezo kuwa bila Katiba mpya na tume huru kamwe
hakuwezi kufanyika uchaguzi ulio huru na wa haki.
Demokrasia bungeni
Akizungumzia mwenendo wa Bunge, alisema linakwenda vizuri lakini ni mapema kulizungumzia kwa sasa.
“Katika
Bunge hili wameingia vijana madhubuti bungeni, lakini hatua ya Serikali
kuzuia Televisheni ya Taifa (TBC) kurusha matangazo ya Bunge moja kwa
moja, hiyo ni dalili ya kuminya demokrasia.”
Alisema
ni aibu kubwa kwa Serikali kutumia polisi kuingia ndani ya Bunge badala
ya kujenga hoja na akasema hali hiyo ikiachwa ikaendelea italitia aibu
Taifa.
Alisema
moja ya mambo yaliyohimizwa na ambayo Watanzania waliachiwa na Mwalimu
Julius Nyerere ni utaratibu wa kujenga hoja na kutumia nguvu ya kushinda
na akaongeza kuwa kitendo cha polisi kuingia na kupiga wabunge ni
kuminya na kudidimiza demokrasia.
“Tanzania
tunasifika duniani kote kwa kuheshimu na kufuata demokrasia, lakini
Serikali imeamua kutumia polisi kuminya demokrasia, hii ni aibu kubwa
kwa Taifa… Watanzania tukiacha demokrasia ikaminywa tutalitia aibu
Taifa,” alisema.
Shukrani kwa Watanzania
Lowassa
anasema licha ya kupokonywa ushindi, anajivunia mafanikio makubwa
aliyoyapata kutoka kwa Watanzania walio wengi ambao walimuamini na
kumuunga mkono.
“Watanzania
waliniunga mkono kwa wingi sana, hali ile ilinipa faraja
kubwa…nilifarijika pia nilipowaomba watulie wakanielewa na kutulia…
nawashukuru sana Watanzania walionielewa na kutulia,” alisema.
Alitoa
wito kwa Watanzania kuilinda amani ya nchi huku akisema anasubiri Rais
Magufuli kutimiza siku 100 ndipo atoe tathmini yake kuhusu utawala wake.
“Marais wanapimwa kwa siku 100, nasubiri siku hizo, nitasema.”
Hali ya kisiasa Zanzibar
Akizungumzia
hali ya kisiasa ya Zanzibar na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
(ZEC), kutangaza kurejewa uchaguzi upya, Lowassa alisema suala hilo ni
zito na gumu na linahitaji maombi maalumu na umakini wa hali ya juu
katika kulitatua.
Alitoa
wito kwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na
Rais Magufuli kulishughulikia suala hilo mapema kabla ya Machi 20.
“Wasikubali tufike pabaya. Bado naamini tunaweza kulimaliza kwenye meza,” alisema na kuongeza:
“Nawasihi sana viongozi hawa wasilipuuze hili suala, jambo hili likiendelea litaleta shida kubwa kwa nchi yetu, magaidi wanaweza kulitumia na kuleta madhara makubwa, wasisubiri kufika pabaya, waanze kulishughulikia sasa.”
Alitoa
wito pia kwa wanaoshughulikia suala hilo kuvishirikisha na vyama
vingine badala ya kulifanya kuwa ni suala la CCM na CUF pekee.
Alisema
ni imani yake kuwa Watanzania ni wamoja na hakuna mtu wa kuwagawa kwa
namna yoyote na kuwa wasikubali uchaguzi huo wa marudio kuwa sababu ya
kuivuruga amani ya nchi,
xxxxxxxxxxxxxxx
kwa huduma ya kiafya kutana na tabibu bingwa john lupimo wa lupimo sanitarium, miko tunayopatikana ni hii hapa,
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni