Ijumaa, 8 Januari 2016

FAHAMU SABABU ZA MAUMIVU YA MGONGO NA TIBA YAKE ASILI 

Hali ya maumivu ya mgongo huwatesa watu wengi hasa wale wenye umri mkubwa jambo ambalo husababisha watu hao kutojisikia vizuri au kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako.

Moja ya sababu za maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama huchangia sana maumivu ya mgongo. 

Sababu nyingine ni ubebaji wa mizigo mizito usiozingatia afya ya mgongo na hata kulalia matandiko (magodoro) laini wakati wa kulala.

Uzito wa kupita kiasi (ujauzito, kitambi) huweza kusababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimama. 

Sababu nyingine ni pamoja na  magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo, lakini pia kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ajali  huweza kuwa sababu pia ya maumivu ya mgongo.

Mbali na sababu hizo pia umri wa uzeeni ni mojawapo ya sababu ya maumivu ya mgongo, kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabadiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa na misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.

Sasa baada ya kufahamu sababu hizo ambazo huchangia maumivu ya mgongo ni vyema ikafahamika kwamba kuna baadhi ya vitu asili huweza kutumika kutibu matatizo haya ya maumivu ya mgongo.

hizi ni baadhi tu ya sababu zinazopelekea maumivu ya mgongo na usipotibiwa mapema madahara yake ni makubwa ikiwemo ufanisi wa tendo la ndoa na kwa akina baba nguvu za kiume zinapungua na hata kuisha kabisa, tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoani
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni